Dar: Philip Mangula aanguka gafla, alazwa ICU. Rais Magufuli amjulia hali

Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumamosi Februari 29, 2020 amemjulia hali makamu mwenyekiti wa CCM- Bara, Philip Mangula aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kuanguka ghafla jana

======

PHILIP MANGULA AANGUKA GHAFLA, ALAZWA. RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA

Rais Magufuli leo Februari 29, 2020 amemjulia hali Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kuanguka ghafla jana

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Mangula amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU)
View attachment 1372999
Watu wasiotenda haki kwa wengine hawana faida yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapakuwa na haja ya kutoa statement kuwa alianguka

Viongozi kadhaa huanguka na husalia siri

Ingetosha kusema anaumwa
Kunradhi Comrade Mangula

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko Mbowe anakatwa mitama na green guard ya polisi wa ccm bila hatia,huku Mwenyezi Mungu mweza wa yote,Muumba wa mbingu na dunia anashughulika na majemedari wa ccm,sijui nani ataibuka mshindi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za sasa hazimfai Mangula. Maamuzi haya ya wakati huu, kwa vyovyote hayaendani na falsafa ya chama enzi za akina Mangula.

Yaweza kuwa ni maradhi tu lakini pengine ni matokeo ya msongo wa mawazo unaotokana na mawazo ya mtu mmoja yanapolazimishwa yawe yenu wote, hata msioafiki.

Mungu mwenye huruma amjalie uponywaji, na kisha amrejee mola wake, ajitenge na uovu.
 
Natamani kuandika ila nakosa nguvu. Natamani kusema pumzi zinaniisha.

Ila nataka kusema Mungu hakuwahi shindwa kwa watu wanatenda mema nakusimamia hak kwa hata kwa damu.

Nataka kukumbusha sala ya muinjilisti mmoja maarufu sana ambaye kwa sasa ni marehemu, Moses Kulola. Maombi yake juu yako ni baraka zake kamwe hazijakuacha. Umejaribiwa kwa kiwimbi ila sunami itawatafuna mchana kweupe.

Tunajua kila silaha kuanzia za kuonekana na za kichawi. Ila mnitukane na kuniona tapeli ikiwa silaha hizo zitashinda.

Utakapo toka ICU watarudi wao ICU. Wasali sana, huruma ya Mungu iwakumbuke la sivyo...

Mungu ibariki Serikal ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wetu Dr John Pombe Magufuli bila kuwasahau wazee wote ktk tai hili.

Amen
 
Back
Top Bottom