Dar: Magari 8 yateketea kwa moto katika kituo cha mafuta cha OIl COM kilichopo Boko magengeni

bizzle for shizzle

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
1,010
736
Moto uliozuka usiku WA kuamkia Leo alfajiri mida ya SAA 8 usiku umeteketeza Magari 8 katika kituo cha mafuta cha OIl COM kilichopo Boko magengeni Barabara ya ( bagamoyo road )
Chanzo cha moto huo ni NISSANI CIVILIAN inayofanya shughuri za kubeba abiria maarufu kama daladala kupata hitilafu ya umeme iliyopelekea kupiga shoti na kuzuka kwa moto mida hiyo ya usiku ikiwa imepack katika kituo hicho cha mafuta na kupelekea Magari 8 kuungua ila Magari 6 ndiyo yaliyoungua zaidi na mawili kuungua kidogo tofauti na mengine kiukweli moto ulikuwa mkubwa sana lakini juhudi za madreva boda boda wanaokesha kwa kubeba abiria wakishilikiana na walinzi walihangaika kuuzima moto huo lakini baadae likaja gari LA kikosi cha uokoaji cha fire na kuanza kushirikiana na wananchi hao katika kufanikisha kuuzima moto huo kamanda WA zima moto badae kulipo pambazuka alifika eneo LA tukio na kutoa onyo kwa Magari yanayopack katika kituo vya mafuta na kuwataka madereva na wamiliki kuacha kupack Magari kwenye vituo vya mafuta kwani ni hatari inaweza kupelekea maafa makubwa zaidi
IMG_20180919_092553_6.jpg
IMG_20180919_084159_2.jpg
 
hahahaa namuachia Mungu naona limeungua "... kaazi kweli kweli "..binafsi hakuna kitu nachokihofu kama mafuta ", ya petrol " yaani nikilionaga lile gari lenye tank tu huwa napatwa hofu "
 
Na usishangae kusikia Magari yote hayo Wamiliki wake hawajayakatia ' Bima '. Hata hivyo nawapa pole sana wenye hayo Magari na kwa Mkasa mzima.
 
Hapo boko magengeni kuna nini? Miezi mitatu iliyopita ile fuso ilizoa watu kama 10 kwa kukosa breki....
Poleni sana
 
Back
Top Bottom