Dar es Salaam Giza Masaa Nane kwa siku

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Je! Hii si hujuma za TANESCO? Siku chache zilizopita kulikwa na malumbano kati ya TANESCO na kampuni ya DOWANS kuhusiana na serikali kutaka kununua mitambo ya umeme kutoka kampuni hiyo. TANESCO walitishia kwamba nchi itakumbwa na giza. Na sasa mkwara huo umetimia. Mimi hainiiingii akilini? Hii ni hujuma inabidi serikali ifanye utafiti wa kina kujua uhalali wa DAR kuwa gizani masaa nane kwa siku. Je wanajamii forum mna maoni gani?

Nawatakia kila la heri katika wakati huu mgumu wa kuwa gizani masaa nane kwa siku. Hii itakuwa ni baraka kwa vibaka hasa maeneo ya Manzese, Tandale na kwa Mtogole. Kufa kufaana.
 
Sasa, nimeelewa, nchi hii haina mwenyewe. Nchi ya wanamtandao hiyo. Hata la kuendelea kusema sina. Tishio la Dr. Idris wa Tanesco liko bayana. Si muda mrefu Boss wa Maji naye akasema vivyo hivyo. Si umeme ndiyo nguvu ya kusukuma maji. Wana-JF, haya!!!
 
details please!

- Kwanini?

- Saa ngapi mpaka ngapi?

- Kama ni tatizo, litatatuliwa baada ya muda gani?

- e.t.c
 
Eh Mola,
Tunaomba roho za watakatifu ziintervene haya mambo yanayoendelea kwetu sisi wenye mwili.

Eh roho ya Moringe,eh roho ya Mwalimu,eh roho ya Rupia,eh roho ya Mzee Tambaza,eh roho ya Mzee Dosa Aziz,eh roho ya Mzee Aziz Ally.Mlijitoa maisha yenu ya kimwili ili sisi tupate maisha bora. MBONA MNAANGALIA TU HAYA..........YANATOKEA.MNAKUBALI MATESO NA SHIDA MLIZO PATA ziwe hazina MAANA(were all in vain)

Watu wameanza KUHOJI WAZEE WETU kama mlikuwa sahihi kujitoa maisha yenu na familia zenu kwa ajili ya UHURU WETU.
 
Hata maji hamna karibu maeneo yote ya wilaya ya kinondoni tangu jana eti mitambo inatengenezwa.
 
Huu ni ufisadi hamana hata cha kuhoji hapa!! Ee mola tusaidie na ufisadi tanzani!!
 
Eh Mola,
Tunaomba roho za watakatifu ziintervene haya mambo yanayoendelea kwetu sisi wenye mwili.

Eh roho ya Moringe,eh roho ya Mwalimu,eh roho ya Rupia,eh roho ya Mzee Tambaza,eh roho ya Mzee Dosa Aziz,eh roho ya Mzee Aziz Ally.Mlijitoa maisha yenu ya kimwili ili sisi tupate maisha bora. MBONA MNAANGALIA TU HAYA..........YANATOKEA.MNAKUBALI MATESO NA SHIDA MLIZO PATA ziwe hazina MAANA(were all in vain)

Watu wameanza KUHOJI WAZEE WETU kama mlikuwa sahihi kujitoa maisha yenu na familia zenu kwa ajili ya UHURU WETU.

...waache Mw'Mungu awarehemu huko walikolala. Hapa hata Mwenyezi Mungu halaumiki. Wazee walijitolea mhanga, nasi tumepewa akili tufikirie.

Wakulaumiwa ni hao wapiga kura 1670 wa CCM, ambao JMK alizoa kura zao 1072, dhidi ya kura 476 za Dk. SAS, na kura 122 alizoambulia Prof. MM.

Kama haitoshi, wakajitokeza wapiga kura 9,123,952 au 80.28% ambao pia hawakuuzingatia msemo,

"domo la mzee linanuka lakini halisemi uongo!"...

Maneno ya JK Nyerere yanaturudia, kuwa Ikulu si mahali pa kukimbilia, na jamaa hawa hawafai! Shime 2010 hiyo inakuja, sanduku la kura litasemaje? au ndio heri ya jini likujualo?
 
Je! Hii si hujuma za TANESCO? Siku chache zilizopita kulikwa na malumbano kati ya TANESCO na kampuni ya DOWANS kuhusiana na serikali kutaka kununua mitambo ya umeme kutoka kampuni hiyo. TANESCO walitishia kwamba nchi itakumbwa na giza. Na sasa mkwara huo umetimia. Mimi hainiiingii akilini? Hii ni hujuma inabidi serikali ifanye utafiti wa kina kujua uhalali wa DAR kuwa gizani masaa nane kwa siku. Je wanajamii forum mna maoni gani?

Nawatakia kila la heri katika wakati huu mgumu wa kuwa gizani masaa nane kwa siku. Hii itakuwa ni baraka kwa vibaka hasa maeneo ya Manzese, Tandale na kwa Mtogole. Kufa kufaana.

Hii ni ile hujuma alisema yule wanamuita daktari sijui daktari wa nini vile . Oh nimeambiwa ni daktari wa umeme yuko Tanesco kwamba tusipopata umeme tusimlaumu maana tutapata ugonjwa unaitwa giza.
HUJUMA TUPU. Yaani wadanganyika tunadharaulika? Yaani yule Daktari alitwambia live na amefanya na sisi tunamuangalia tu??
 
Mnaoishi Dar hebu tupeni hiyo taarifa ya umeme! Lakini kabla ya kughadhabika, hebu mnaojua taarifa za umeme, tupeni hali halisi ya umeme wa dar es salaam kihistoria. Je kuwa na mgao wa umeme ni jambo la kawaida? Kama ndio, huwa mgao huo unakuja msimu gani na sababu yake nini nini? Mgao huo huwa unatabia zipi, yaani masaa mangapi, maeneo gani yanathirika zaidi na unadumu kwa muda gani. tukipata hayo majibu ndio tutaelewa kama ni njama ama ni hali halisi!
 
Hakuna cha taarifa mambu ni giza tu ,ila kutokana na evolusheni wabongo siku hizi wanaona hata kwenye giza wamedevelop some habit flaniflani katika macho yao ,inabidi waende na maisha yalivyo.
 
Niko mu giza lakini monitor yangu naiona :):(:confused:

Mimi naona Watanzania wote ni vikojozi (samahani wale ambao walishakana uraia). Kwani Madagascar wanatuzidi nini? Au sisi tuliumbiwa kwenye sayari nyigine tena Pluto ambapo kila kitu kilishapoteza uhai??
 
Back
Top Bottom