Dan Cooper: Mtekaji ndege asiyefahamika kwa miaka 40 sasa

Yellescabar

Senior Member
Mar 19, 2017
107
246
Mwanaume mmoja alipanda ndege ya Shirika la ndege la Northwestern Airlines akiwa peke yake, akibeba bomu kwenye mkoba kwa urahisi kama ameshika faili la nyaraka za ofisi. Aliteka ndege hiyo na kutaka apewe dola 20mil na kisha kutoweka kwenye uso wa dunia.

Mpaka leo, hakuna mtu ulimwenguni anayejua ni wapi mtu huyo alienda, alipoishi au kama alikufa. Leo imekuwa ni kama hadithi tu ulimwenguni. DB Cooper ni jina lake na hii ni simulizi ya kweli. Kilichotokea ni kama unaangaliza tamthilia ya Avenger ama 'Loki' kwenye jukwaa la OTT na kama umewahi kuangalia utafahamu kuhusu jina laDB Cooper. Simulizi hii ina mwanzo, lakini haina mwisho.

Ilikuwa Novemba 24, 1971. Mwanamume mmoja alikata tiketi ya Shirika la Ndege la Northwestern iliyokuwa inasafiri kutoka Portland, Marekani hadi Seattle. Alilipa fedha ya tiketi mwenyewe kwa kutumia jina la Dan Cooper. Mpaka leo watu hawajui kama lilikuwa jina lake halisi au la uwongo. Lakini baada ya uchunguzi na uchunguzi wote, ilionekana kuwa hili halikuwa jina lake halisi.

Dan Cooper alikuwa nani, alitoka wapi, kulikuwa na mtu yeyote katika familia yake?

Haijawahi kufuatiliwa. Mpaka leo, kesi yake haijafika mwisho. Kulikuwa na washukiwa kadhaa lakini hakuna mshtakiwa aliyepatikana katika kesi hiyo. Utekaji nyara wa aina hii ulikuwa wa kawaida kwa wakati huo," alisema William Ratzac, rubani mwenza wa shirika la ndege la Northwest Airlines Boeing 727.

Wakati huo hapakuwa na sheria za usalama wa ndege za ndani au za kimataifa nchini Marekani. Unaweza kubeba bomu au bunduki na kwenda moja kwa moja ndani ya ndege.

"Wacuba wanaoishi Marekani walikuwa wanaweza kuteka ndege wakiwa wamewaelekezea bunduki na kutaka ndege iruke kuelekea nchini kwao. Ndege hiyo ikitua Cuba, abiria waliotekwa wanapewa kinywaji kizuri cha gharama Cuba na sigara za Cuba na maafisa wa uwanja wa ndege wa Cuba kama zawadi, na baadwe wangeruhusiwa kurudi kuendelea na shughuli zao," William alisema. .

Kila kitu kilikuwa cha kufurahisha ... hadi suala la utekaji wa Cooper lilipojitokeza. Kidogo aina ya utekaji wake ilikuwa tofauti. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mtekaji kudai kikombozi katika utekaji nyara huu. Cooper katika safari hiyo alivalia suti nzuri zinazovaliwa sana na wafabiashara akivaa na miwani nyeusi, alionekana mtanashati wakati akipanda ndege.

Alipopanda alimuita mhudumu kwa simu za ndege na kumkabidhi kikaratasi. Muhudumu huyo alidhani mwanaume huyo alikuwa akimtania. Kwa sababu tukio kama hilo la kupewa barua ama kikaratasi lilikuwa jambo la kawaida sana wakati huo.

Kwa sababu ya matangazo ya mashirika ya ndege ambayo yalikuwa yakufurahisha wateja zaidi kwa mfano tangazoi kama vile 'Angalia nguo za mhudumu wetu wa ndege', au 'Keti kwenye ndege yetu na ufanye ngono nami (bila shaka, mhudumu ni mzuri').

Kwa mtekaji Cooper nini kiliendelea?

Jina la muhudu aliyepewa kikaratasi alikuwa anaitwa Florence Shatner. Cooper akamkabidhi barua, huku akiendelea kumtazama. Mtu huyu alikuwa tofauti na watu wengine wa kutaniana, pia alikuwa na sura tofauti. Alisema, "Fungua barua hiyo na uisome."

Alikabidhi barua hiyo kwa mhudumu mwingine hewa, Tina McClure. Tina akaifungua, barua hiyo ilisema, "ndege yako imetekwa, nina bomu, njoo uketi karibu yangu."

Tina ilibidi akubali kuketi karibu yake, Cooper akafungua mkoba wake, na kumuonyesha Tina kulikuwa kitu kinachoonekana kama bomu ndani. Kulikuwa na vijiti vya baruti (kiberiti), kulikuwa na betri na pia kulikuwa na nyaya nyingi. Alimwambia Tina kuwa akijaribu kufanya lolote atalipua ndege na hakuna mtu atakayepona. Na kwa urefu wa ndege ilipofika, ingedondoka kwa mlipuko isingekuwa rahisi kupona, hata kama mlipoko huo usingempata myu kwenye ndege hiyo.

Maramoja Tina alimpigia simu rubani kupitia simu za ndege na kumjulisha kuwa ndege hiyo ilikuwa imetekwa.

Lakini wakati huo rubani asingeweza fanya kitu, ndege ilikuwa imeshapaa na kufika umbali.

"Aliagiza kinywaji. Alikuwa akivuta sigara mara kwa mara na nilikuwa nimeketi karibu naye nikiiwasha sigara yake kwa sababu hakutaka kuondoa mikono yake kwenye kiwambo cha kurusha bomu.
Ndege iliyotekwa nyara na Cooper ilikuwa na Tina McClure kama mhudumu wake.

Baada ya kuketi na Tina, muda mfupi Cooper aliaanza kuandika anachokitaka kupitia kipande cha karatasi na kukituma kwa rubani. Baadae akakichukua kikaratasi hicho. Alichokua anataka ni dola milioni 20 pesa taslimu, parachuti 4 na lori la mafuta ya ndege baada ya ndege kutua Seattle, ili ndege hiyo ijazwe na aelekee kwingine alipopataka. Baada ya kupokea ujumbe wa mtekaji, rubani alipiga simu shirika la ndege la Northwestern Airlines, na kueleza hali ilivyo. FBI, shirika kubwa zaidi la uchunguzi wa ndani nchini Marekani, likapewa taarifa.

Safari kutoka Portland hadi Seattle ilichukua dakika 37. Rubani William Rattzack alianza kuzunguka hewani ili kuvuta muda wa maandalizi ya mahitaji ya Cooper. Mpaka wakati huo, abiria hawakujua kinachoendelea. Abiria waliambiwa kuwa wangechelewa tu kufika waendako kutokana na sababu za kiufundi. Ni hayo tu! "Nilimuuliza, 'Je, una hasira na shirika letu la ndege?' Alisema, 'Sina hasira na kampuni yako, lakini nina hasira sana,' anasema Tina.

Ndege hiyo ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Seattle saa 5:45 asubuhi. Pesa iliyotakiwa na DB Cooper, parachuti zikaja. Alipozishika pesa, aliruhusu abiria kushuka pamoja na wahudumu wawili kati ya watatu waliachiwa wakaondoka. Kwenye ndege akabaki marubani Harold Anderson, rubani mwenza William Rattzack na mhudumu wa ndege Tina McClough.

Cooper akawamabia anataka kwenda Mexico City. Rubani akamjibu kuwa ndege hiyo haikuwa na mafuta ya kutosha kuwafikisha huko, kwa sababu hiyo Cooper aliamuru ndege hiyo inapaswa kuelekezwa Renault katika jimbo la Nevada la Marekani.Ndege ikaanza safari kuelekea upande wa Rhino.

Bob Freeman ni wakala aliyestaafu wa FBI. Alikuwa mmoja wa maafisa wa kwanza kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Seattle baada ya kujua kwamba DB Cooper alikuwa ameteka nyara ndege hiyo. Baadaye alikuwa mmoja wa maafisa waliounda timu ya uchunguzi kuchunguza kesi hiyo.

Kulikuwa na ukimya ndani ya ndege. Tina aligundua kuwa Cooper alikuwa amekasirika, lakini hakuchukua hatua yoyote, wala Cooper hakufanya chochote tofauti. Harold Anderson na William Rattzack waliambiwa na Cooper kwamba wanapaswa kurusha ndege kwa urefu wa futi 10,000, isiwe umbali wa juu sana wala chini sana.


William Rattzack alikuwa rubani wa ndege iliyotekwa na Dan Cooper

Boeing 727 ilikuwa ikisafiri kwa kasi ya kilomita 400 kwa saa. "Baadae tuligundua kwamba alikuwa anakaribia kuruka kutoka nje ya ndege," alisema Harold. Kwenye ndege ya Boeng kuna ngazi. Lakini katika miaka ya sabini, ngazi hiyo haikuwa na mfumo ambao haungeweza kufunguliwa wakati ndege inaruka. Cooper alitaka kufungua ngazi na kuruka chini. Mlango wa kutua kwa dharura unapaswa kufunguliwa. Hata hivyo Cooper alimzuia Tina kufanya hivyo, aligundua kuwa asingeufungua Tina akiwa pale.

Akamchukua Tina na kumpeleka kwenye chumba cha rubani. Baada ya kumpeleka akarudi na akafungua kwa nguvu mlango wa kutua kwa dharura, upepo ukingia na kupuliza kwa nguvu kutokana na kasi ya ndege, na king'ora kilisikika. Rubani aliiona heka heka hizo kupitia kwenye skrini.

Baada ya sekunde chache ndege hiyo ilianguka . "rafiki yako karuka chini," William alisema akiwatazama wengine. Inaonekana mahali fulani katikati ya Seattle na Rhino, Cooper aliruka kwa parachuti kutoka kwa ndege iliyokuwa ikitembea umbali wa futi 10,000. Harold, William na Tina walisalimika na kufika Rino salama. Mpaka sasa hakuna mtu ulimwenguni ambaye ameshuhudia kumuona mtu anayeitwa Dan Cooper kwenye ndege.

Msako wa Jinai

Tukio la utekaji nyara lilikuwa limekwisha, lakini mojawapo ya shughuli kubwa zaidi za utafutaji katika historia ya Marekani ilikuwa imeanza. FBI, polisi wa eneo hilo, na kitengo cha jeshi walikuwa wakimtafuta DB Cooper, hata watoto wadodo wa skauti nao walihusishwa kumtafuta. Walikadiria muda ambao Cooper aliruka kwa parachuti kutoka kwenye ndege, wakachora ramani ya mahali ndege hiyo ilipo, na kuanza upekuzi wa mita za mraba themanini.

Wakati ndege inatoka Seattle kwenda Reno, na Cooper kuruka na parachuti ilikuw ainaendeshwa na rubani, Harold Anderson.

Wengi walikisia kwamba huenda Cooper hakunusurika kwenye ajali hiyo. Lakini kama alikufa kwanini basi hata kitu kimoja kisipatikane kumuhusu yeye, au mabaki yake? Cooper hakuacha chochote kwenye ndege. Wakati anataka kuruka kutoka kwenye ndege alivua shati na tai yake, na kulikuwa na sigara chache ambazo alikuwa amevuta. Baadaye zilipotea kwa FBI.

Aliruka akiwa na barua yake ya kuteka, barua yake ya madai na kikombozi, mkoba wake, parachuti mbili na begi la pesa. Msako huo uliodumu kwa muda wa miezi tisa, haukupata kitu chochote, hakuna kitu kilichopatikana eneo hilo, hata kipande cha nguo au kamba kutoka kwa parachuti ambayo aliruka nayo.

Cooper alienda kwa nani?

Ushahidi wa kwanza ni kwamba Cooper aliomba pesa lakini hakutaja pesa hizo zilipwe katika noti gani. Kwa kutumia fursa hii, FBI walimpa fedha hizo kwa noti za dola ishirini ishirini, zote zikiwa kwenye mfuko. Hakuwa na mshikio wa kushika begi, wala kamba ya kulishika begani.

Mfuko huo ulikuwa na uzito wa kilo 10. Sasa unaweza kujiuliza, ilikuwa rahisi kiasi gani kuruka kutoka kwenye ndege na kitu chenye uzito wa kilo 10? Hata nguo za Cooper hazikufaa kurukia kwa parachuti angani. Mtu yeyote anayejua anataka kuruka parachuti, kwa nini asijiandaa kwa kuvaa nguo hata moja? Kuruka kwa parachuti ni kazi ya ustadi sana, maana yake itafunguka kwa upana ambao inapokuwa angani mrukaji hatakufa.

Parashuti aliyopewa Dan Cooper iliandaliwa na mtu anayeitwa Kos. Anasema kupitia filamu ya National Geographic ya 'Robbery in the Sky' siku hiyo nilifunga aina mbili za parachuti, NB8 na ile ya michezo, Cooper alichagua NB8. Hii aliyoichagua kamba zake hazifunguki haraka, usipoipata kwa wakati unaweza kushindwa kuifungua parachuti."

Cooper aliporuka nje ya ndege kutoka umbali wa futi 10,000. mvua ilikuwa ikinyesha sana na kulikuwa na baridi kali. Hakuna ubishi kwamba mpaka anafika chinikuna uwezekano kwamba alikuwa nusu mfu kwa baridi

Ushahidi unaochanganya

Uchunguzi uliendelea kwa miaka mingi lakini hakuna kitu halisi kilichopatikana. Wakati huo FBI iliwahoji mamia ya watu waliokuwa wanashukiwa.

Ulifika wakati wa kukamilisha uchunguzi lakini siku moja muujiza ulitokea.

Miaka tisa baada ya uhalifu huo, mnamo Februari 1980, familia moja ilikuwa ikiokota kuni kwenye kingo za Mto Columbia. Mmoja wao mvulana mdogo anayeitwa Brian Ingram aliona mabunda matatu ya noti zilizooza yakiwa yamefukiwa ardhini.


Hizi zilikuwa noti zile zile ambazo alipewa DB Cooper kama kikombozi wakati wa utekaji wa ndege. Namba za utambuzi za fedha hizi zilifuatana.

Pengine miaka kumi baadaye, uhalifu huo huenda ungepata utatuzi. FBI ilipekua eneo hilo, lakini hawakupata chochote isipokuwa vifurushi hivyo vitatu. Hakuna pesa, hakuna ushahidi mwingine.

Maelezo haya yaliibua maswali mengi kuliko majibu. Fedha hizo chache zilipatikana kilomita thelathini hadi arobaini mbali na eneo ambalo Cooper aliruka kutoka kwneye ndege na parachuti na kutafuta mita za mraba themanini.

Vidokezo hivi vimefikaje hapa?

Kuna kuchanganya kiasi, kwenye kutafuta ushahidi , aliruka mbali kabisa upande wa chini wa mkondo wa mto na sehemu ambayo noti zilipatikana ilikuwa juu ya mkondo. Je, zilipanda kukinzana na mkondo wa maji? Ni kama zitoke chini zipande ghorofani.
View attachment 2402333
View attachment 2404891
 
Stori kama hz kupata wa changiaji ni ishu ila ninachoweza kusema zama za cooper kulikuwa na watu vichwa kweri kweri
 
Nakumbuka season ya kwanza movie ya " prison break" Dan Cooper alionyeshwa kama miongoni mwa wafungwa wa fox river na baadae pesa yake ikaanza kugombaniwa na akina Michael, Theodore Bagwell na wengineo...kumbe hii ndio story yake, very interesting.....naamini siku za karibuni mystros wa hacking na technology wizards wana uwanda mkubwa wa kutufurahisha, nyakati zinaongea sana...kongole Kwa cooper, wizi unalipa.
 
Back
Top Bottom