Dalili mbaya kwa CCM kutokubalika katika hili

Panctuality

JF-Expert Member
Jun 11, 2019
726
1,044
Habari wanajukwaa

Chama cha MAPINDUZI ni chama dola kwa sasa,wananchi bado wana imani kubwa sana na chama hiki mathalani kwa wananchi wa daraja la chini kabisa namaanisha wakulima ambao kipato chao hukipata kwa jasho na damu huku wakikabiliana na changamoto lukuki za kijiografia, kibaiolojia, asili na za kibanadamu.

Tanzania hii inawakulima wa zao la tumbaku mamilioni kwa mamilioni mathalani Tabora, Chunya, Katavi na maeneo mengine, ni zao ambalo huwaingiza wakulima hao mamilioni ya fedha na tozo kedekede kwenda serikalini na ushuru kwa Amcos ndio maana mpaka sasa vyama vinaendelea kujiendesha.

Mama Samia ashukuriwe kwa kuongeza makampuni ya ununuzi wa zao hilo tena mno,mateso wayapatao wakulima kisaikolojia kabla ya tarehe 30 Jun mwaka huu 2023 ni kuambiwa kuwa mwisho wa masoko ni tarehe hiyo na baada ya hapo itakuja kampuni nyingine kununua kama makinikia(bei za kutupa) licha ya kuwa makampuni yaliopo hayajatimiza na hayatatimiza kukamilisha makisio yao kufikia deadline hiyo, chonde chonde wakulima walipigwa chenga la macho mbolea za ruzuku vyamani, leo hii pembejeo iko juu mno bado wanaambiwa kuwa watauza kama bei ya makinikia kufikia tarehe hiyo,ni mwaka gani ilitokea tumbaku zikaisha kununuliwa kufikia jun 30?

Hali ya hewa nchini kote inafanana mpaka tumbaku zote ziwe zimechumwa,kugrediwa na kuuzwa sawa? Kama kampuni zenye mikataba bado zinahitaji tumbaku za makisio yao iweje mlete kampuni ya kuumiza wakulima?

Serikali moja kwa moja inaonekana kuumiza wakulima wa zao hilo,siasa nyingi kwenye kilimo,Bashe na Mama Samia mnataka kuua vyama,mnajua athari gani itatokea kwa vyama?

Madeni ya benki mtalipa nyinyi,na vipi kuhusu malipo ya wakulima?
Uacheni ushirika uongozwe na tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania TCDC na sio hayo matamko ya majukwaani.

Hivi mnajua idadi ya wakulima wa tumbaku Tanzania, kama hamjui waulizeni Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) hapo ndio mtajua mtakuwa mmepoteza kura mamilioni mangapi!!!

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,mkiona itafaa Basi futeni kilimo cha tumbaku licha ya baadhi yenu kusoma na kulipwa mishahara kwa mauzo na kodi za makampuni ya Tumbaku!

Tafakarini,chukueni hatua,naona wabunge hawasemei bungeni kwa kuwa kiongozi wa juu kabisa unajihusisha katika fungu la 11 na kumpa kiburi Mh. Bashe.

Kilimo ni uchumi na sio siasa.
 
Mkuu unaifahamu tumbaku na suruba zake,umewahi Kaa nje na ndoa more than 5 months without your wife? Hili zao hapana,unaanza kazi mwezi August na kupokea fedha September ya mwaka mwingine,halafu watu wanaleta siasa katika hili
NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
 
Habari wanajukwaa

Chama cha MAPINDUZI ni chama dola kwa sasa,wananchi bado wana imani kubwa sana na chama hiki mathalani kwa wananchi wa daraja la chini kabisa namaanisha wakulima ambao kipato chao hukipata kwa jasho na damu huku wakikabiliana na changamoto lukuki za kijiografia, kibaiolojia, asili na za kibanadamu.

Tanzania hii inawakulima wa zao la tumbaku mamilioni kwa mamilioni mathalani Tabora, Chunya, Katavi na maeneo mengine, ni zao ambalo huwaingiza wakulima hao mamilioni ya fedha na tozo kedekede kwenda serikalini na ushuru kwa Amcos ndio maana mpaka sasa vyama vinaendelea kujiendesha.

Mama Samia ashukuriwe kwa kuongeza makampuni ya ununuzi wa zao hilo tena mno,mateso wayapatao wakulima kisaikolojia kabla ya tarehe 30 Jun mwaka huu 2023 ni kuambiwa kuwa mwisho wa masoko ni tarehe hiyo na baada ya hapo itakuja kampuni nyingine kununua kama makinikia(bei za kutupa) licha ya kuwa makampuni yaliopo hayajatimiza na hayatatimiza kukamilisha makisio yao kufikia deadline hiyo, chonde chonde wakulima walipigwa chenga la macho mbolea za ruzuku vyamani, leo hii pembejeo iko juu mno bado wanaambiwa kuwa watauza kama bei ya makinikia kufikia tarehe hiyo,ni mwaka gani ilitokea tumbaku zikaisha kununuliwa kufikia jun 30?

Hali ya hewa nchini kote inafanana mpaka tumbaku zote ziwe zimechumwa,kugrediwa na kuuzwa sawa? Kama kampuni zenye mikataba bado zinahitaji tumbaku za makisio yao iweje mlete kampuni ya kuumiza wakulima?

Serikali moja kwa moja inaonekana kuumiza wakulima wa zao hilo,siasa nyingi kwenye kilimo,Bashe na Mama Samia mnataka kuua vyama,mnajua athari gani itatokea kwa vyama?

Madeni ya benki mtalipa nyinyi,na vipi kuhusu malipo ya wakulima?
Uacheni ushirika uongozwe na tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania TCDC na sio hayo matamko ya majukwaani.

Hivi mnajua idadi ya wakulima wa tumbaku Tanzania, kama hamjui waulizeni Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) hapo ndio mtajua mtakuwa mmepoteza kura mamilioni mangapi!!!

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,mkiona itafaa Basi futeni kilimo cha tumbaku licha ya baadhi yenu kusoma na kulipwa mishahara kwa mauzo na kodi za makampuni ya Tumbaku!

Tafakarini,chukueni hatua,naona wabunge hawasemei bungeni kwa kuwa kiongozi wa juu kabisa unajihusisha katika fungu la 11 na kumpa kiburi Mh. Bashe.

Kilimo ni uchumi na sio siasa.

Nani wa kumtoa ccm Hapa Tanzania
 
Back
Top Bottom