Dalili kuu za Uchawa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Habari zenu Wakuu,

Siku hizi kumekuwa na tabia ya watu kuwa machawa/upambe kwa watu maarufu, Wanasiasa au Matajiri.

Sasa leo nakuletea Dalili za kujitambua kama wewe ni Chawa ili kama ikiwezekana ukitumie kipaji chako ulichobarikiwa.

Dalili zenyewe ni hizi zifuatazo,
1) Kumsifia mtu kiasi kwamba unapitiliza sifa unazompa.

2) Kujipendekeza kwa mtu especially mwenye hela.

3) Kujihisi kuwa huwezi kuendesha maisha yako bila ya msaada wa mtu fulani.

4) Kutokuwa na aibu/haya mbele za watu.

5) Kuongea kupita kiasi.

6) Kuomba omba hela hovyo kama Matonya.

7) Kumchukia bila ya sababu mtu asiekusaidia kifedha.

8) Kupenda vya bure.

Kama unahisi una dalili moja kati ya hizo, nakushauri uungane na kina Mwijaku na Baba Levo kwenye Chama chao cha Machawa.

ASANTE.
 
5 inanihusu sana lakini mimi sio chawa kabisa

uongeaji wangu ni kwenye ubishani wa mpira
 
Back
Top Bottom