Daladala zilizochoka mpaka kuegemea upande mmoja zinahatarisha usalama wa abiria, kwanini zinaendelea kutumika?

Mawele

Member
Jul 25, 2023
30
116
Umewahi kukutana na daladala imejaza abiria halafu upande mmoja unakuwa umeelewa utafikiri inataka kuanguka?

images - 2024-03-30T201754.051.jpeg

Sijui nini kinasababisha hali hiyo na sina hakika iwapo hiyo ni salama kwa abiria, maana huwa nawaza likiyumba kidogo tu huenda likabinuka na kusababisha ajali.

Kwanini magri haya chakavu yanaendelea kutumika? Kama yanahitaji maboresho kwanini hayafanyiki? Trafiki hawaoni?

20240324_155401.jpg
 
Daradara za vikindu usiku zinaingia City Centre ni mwendo wa kusanya mwanzo mwisho!? Chombo imkata centre bolt na ina taa moja tu mwendo mdundo, na hakuna kujali.
 
Daladala nyingi huwa zinapakia abiria njiani kwahyo dereva akitaka kupakia abiria ule upande wa konda anaushusha chini afu ule upande wake unakuwa kwenye lami ndo mana daladala nyingi zinaegemea upande wa konda na sio upande wa dereva
 
kampuni la haipiki utaliii mlima kilimanjaro halilipi mishahara ya maportas na hudaiwa takriban milion 30 toka corona mpak sasa tunaomba msaada
 
Shida ni kwamba waliokasimiwa jukumu la vehicle inspection Wana agenda nyingine...... Na Sina uhakika na weledi wao kwa kazi hiyo, kama wamepitia mafunzo yahusuyo ujuvi wa gari na inavyofanya kazi na yapi makosa ya kuonya na yakuadhibu papo kwa papo??!!!

Nadhani Kuna haja ya kuzalisha Vehicle inspectors wakutosha Ili wawe wengi barabarani badala ya hawa watumishi wanaoamka kwenda kukusanya hela za vikoba au mchezo.

Ukitoka masaki to gongo lamboto, Jamaa wananyoosha mkono tu gari Inapita inasimama mbali kule wanaendelea na stori zao konda anashuka na 2000 chap anaenda kukabidhi kwa aloyenyoosha mkono anarudi mnaondoka..... (2000 msasani shule, 2000 moroko, 2000 magomeni hospital, 2000 kigogo round Abt, 2000 Msimbazi center na kamera juu, 2000 Daraja la Veta, 2000 vingunguti/jet, 2000 u/ndge au banana, 2000 goms kwenyewe.

Kama ilivyo ngumu ngamia kupenya tundu la sindano ni ngumu pia kupita walipo usipingwe mkono ........ Kwa mantiki hiyo unadhani madaladala mabovu yataisha

Nadhani jambo la msingi ni mafunzo sahihi lakini pia uelewa wa taratibu na Sheria za usalama barabarani kwa wasimamizi, sisi wananchi tunaenda na msimamo wa serikali, wakisimamia ipasavyo tutageuka ila wakiendekeza upatu tutacheza nao lakini maisha ya watu yanaendelea kuwa hatarini hususani abiria..

Wazo langu, nashauri wawe na cheki point Maalum za kukaa na pafungwe kamera zinazoungwa na na mabango ya matangazo kwa eneo Hilo mtu anayepita anaweza kushuhudia wanachofanywa .... Wakipokea tuwe tunaona, gari ikisimamishwa tuwe tunaona wanachokagua na endapo wanaingia ndani kuona hali ya daladala, huenda ikapunguza ubovu wa vyombo na Kisha upatu kuisha.
 
kampuni la haipiki utaliii mlima kilimanjaro halilipi mishahara ya maportas na hudaiwa takriban milion 30 toka corona mpak sasa tunaomba msaada
Andaa uzi wake ili watu wausome mnaweza kusaidiwa, huu ni wa daladala zilizoegama
 
Umewahi kukutana na daladala imejaza abiria halafu upande mmoja unakuwa umeelewa utafikiri inataka kuanguka?...
1. Serikali corrupt. Wahusika hujali matumbo yao tu. Hapo huwezi kuzikamata, kama si gari ya afande hiyo,basi mlungula unahusika

2. Kodi. Serikali inajali kodi tu. Mradi inalipwa poa. Hawana time na abiria. Aidha, ili kupata faida, mjasiriamali haoni haja ya kuingiza gari mpya maana hiyo mishipa inamuingizia hicho kidogo kwa siku kuliko kupoteza mamilioni kuagiza gari mpya

3. Upumbavu wa watz ambao wapo tayari kufanywa lolote wakidai Mungu kapanga. Wanaweza pia kusifu serikali ya mama kwa kuwawezesha kupanda gari chakavu na kufika uswahilini kwao salama.

Hilo la mwisho ndiyo mbaya zaidi
 
Pia kuna gari nyingi zimekata CENTER BOLT! Ukipishana na gari ya hivyo inakua kama inataka kukugonga hivi iko kushoto kulia ani haieleweki ni tabu tupu ila ziko barabarani na matraffic wanaziangalia tu... Na ndiyo mtaji wao wa pesa za bia na nyama choma utafanyaje sasa..
 
Back
Top Bottom