Daily News (TSN) taabani kifedha

cobstev80

Member
Aug 14, 2013
5
0
Taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa Kampuni ya Magazeti ya Serikali yaani TSN ina hali ngumu sana kifedha na kama hatua madhubuti zisipochukuliwa na Serikali kuinusuru Kampuni hiyo, huenda ikafilisiwa na wadeni wake kwani uwezo wake wa kulipa wadeni hasa wanaosambaza malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa gazeti na huduma nyinginezo.

Kwa sasa madeni ya Kampuni yanakaribia 2 bilioni Shilingi za kitanzania huku pesa iliyopo kwenye akaunti zao mbalimbali inafikia kiasi cha 15,000,000.00 Shilingi za kitanzania. Hali hii imesababisha baadhi ya masuala muhimu yahusuyo uendeshaji wa Kampuni hiyo kuhairishwa na mengine kusitishwa kabisa bila kujali umuhimu wa masuala hayo kwenye utendaji wa Taasisi hiyo nyeti.

Inasemekana kuwa Uongozi wa Kampuni hiyo sasa unafanya mpango wa kupata OVERDRAFT kutoka katika moja ya benki zake ili angalau iweze kuendesha shughuli zake kwa kulipa madeni yahusuyo mambo muhimu ya uendeshaji wa Kampuni hiyo.

Jambo la kusikitisha ni kuwa toka kuondoka kwa aliyekuwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa mwanzo mnamo mwezi wa Desemba 2012 mambo yalianza kwenda mlama, hii imesababishwa na uzembe kwenye kusimamia makusanyo ya fedha kutoka kwa wadeni wa Taasisi hiyo na pia nidhamu ya matumizi imekuwa sio nzuri.

Kwa sasa Kampuni hiyo haina Uongozi kwani Afisa Mtendaji Mkuu wake bado ni kaimu na Bodi haijateuliwa toka mwezi Machi mwaka huu 2013 ambapo Bodi ya wakurugenzi iliisha muda wake.
 
Na wale wa magazeti UHURU,MZALENDO wanapata mshahara?magazeti ya CCM lazima yafe hakuna mtanzania anayetaka uongo wa maisha bora
 
Taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa Kampuni ya Magazeti ya Serikali yaani TSN ina hali ngumu sana kifedha na kama hatua madhubuti zisipochukuliwa na Serikali kuinusuru Kampuni hiyo, huenda ikafilisiwa na wadeni wake kwani uwezo wake wa kulipa wadeni hasa wanaosambaza malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa gazeti na huduma nyinginezo.

Kwa sasa madeni ya Kampuni yanakaribia 2 bilioni Shilingi za kitanzania huku pesa iliyopo kwenye akaunti zao mbalimbali inafikia kiasi cha 15,000,000.00 Shilingi za kitanzania. Hali hii imesababisha baadhi ya masuala muhimu yahusuyo uendeshaji wa Kampuni hiyo kuhairishwa na mengine kusitishwa kabisa bila kujali umuhimu wa masuala hayo kwenye utendaji wa Taasisi hiyo nyeti.

Inasemekana kuwa Uongozi wa Kampuni hiyo sasa unafanya mpango wa kupata OVERDRAFT kutoka katika moja ya benki zake ili angalau iweze kuendesha shughuli zake kwa kulipa madeni yahusuyo mambo muhimu ya uendeshaji wa Kampuni hiyo.

Jambo la kusikitisha ni kuwa toka kuondoka kwa aliyekuwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa mwanzo mnamo mwezi wa Desemba 2012 mambo yalianza kwenda mrama, hii imesababishwa na uzembe kwenye kusimamia makusanyo ya fedha kutoka kwa wadeni wa Taasisi hiyo na pia nidhamu ya matumizi imekuwa sio nzuri.

Kwa sasa Kampuni hiyo haina Uongozi kwani Afisa Mtendaji Mkuu wake bado ni kaimu na Bodi haijateuliwa toka mwezi Machi mwaka huu 2013 ambapo Bodi ya wakurugenzi iliisha muda wake.
 
Huu ni ujinga tena wa kutupwa.Daily News ni moja ya magazeti yanayoongoza kwa kupata matangazo tena ya bei ghali kweli!! Daily news pia ni moja ya magazeti ya Kiingereza yanayosomwa sana! Mbaya zaidi hao Daily news wanapata ruzuku ya serikali kama shirika la umma!!!

Kuna uzi wa @MM Mwanakijiji leo unazungumzia jinsi tunavyolipa gharama za uzembe wa CCM sasa!! Kulindanalindana kihuni ndio kunatufikisha hapa!!

TSN inaendeshwa kisiasa ndio maana ubadhirifu na uzembe wa management umeifikisha hapo.Daily news linasaidiwa tu na ukongwe wake lakini si ubunifu wa management.
 
Back
Top Bottom