Daftari la kudumu la Wapiga Kura: Kuna sababu ya msingi ya kutoboreshwa?

Mpui Lyazumbi

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,856
371
Hakuna ubishi kwamba tunangia kwenye uchaguzi mdogo katika majimbo ya IGUNGA na ARUSHA mjini. Igunga ni wazi jimbo lile liko wazi na kule Arusha CHADEMA imewatimua madiwani wakaidi. Kwa maana hiyo chaguzi ndogo hazikwepeki katika maeneo hayo.

Rai yangu kwa tume ya Taifa uchaguzi, watendeeni haki watanzania wa maeneo hayo wanao-qualify kupiga kura kwa kuwaingiza kwenye daftari husika na ondoeni wasiofaa.

Mtakumbuka Rev. Mtikila aliibua changamoto kubwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Tunduru baada ya kufariki kwa aliyekuwa mbuge wa jimbo hilo Juma J. Akukweti.

Tujifunze kutokana na makosa na ondoeni hisia za uchakachuaji mapema iwezekanavyo.

Nawasilisha.
 
Na Rorya pia wafanye hivyo hivyo haraka iwezekanavyo kwani tumemchoka mbunge yule ambaye hata siku moja hajawahi kukohoa bungeni!
Na hizi kata tatu tunapiga kura 02/10/11
1. Nyahongo
2. Mkoma na
3. Nyamtinga.
 
bila kusahau kule maswa. kwani jimbo lile linatakiwa lirudi
 
Dodoma mjini pia hakuna mbunge,toka bunge limeanza sijawahi msikia kabisa.
 
Kwa tabia yetu... hilo daftari litafanyiwa maboresho tukikaribia sana uchaguzi
 
Naunga mkono hoja! Mimi nimejiandikisha Dar na sasa nipo Arusha, kwa hiyo nipewe haki yangu kwa kuboresha hilo daftari niweze kupiga kura!
 
Hata mbeya mjini tunahitaji NEC iboreshe daftari kuna umhimu wa kuwa na Uchaguzi mdogo jimbo la Mbeya Mjini
 
Hata mbeya mjini tunahitaji NEC iboreshe daftari kuna umhimu wa kuwa na Uchaguzi mdogo jimbo la Mbeya Mjini
<br />
<br />
Nililenga maeneo ambayo mpaka hayana wawakilishi kutokana na sababu mbalimbali. Hata hivyo naona kuna haja ya kuwa na utaratibu mzuri wa kufanya hivyo mara kwa mara.
 
Naunga mkono hoja kwa daftari hilo kuangaliwa mapema watu wapate haki zao .
 
Na Rorya pia wafanye hivyo hivyo haraka iwezekanavyo kwani tumemchoka mbunge yule ambaye hata siku moja hajawahi kukohoa bungeni!
Na hizi kata tatu tunapiga kura 02/10/11
1. Nyahongo
2. Mkoma na
3. Nyamtinga.
Huku Iringa kuna Madiwani pia WALIGOMA KULA- kata zao nazo ziko wazi.
 
Ni zaidi ya mwaka mmoja toka ku update daftari la kudumu la wapiga kura , kwa kuwaondoa waliofariki na kuwaingiza wapya.
Ndani ya mwaka mmoja kuna mabadiliko mengi yametokea ndani ya Igunga, je! Serikali wame update daftari la wapiga kura? Kuna vijana wengi mwaka jana walikuwa under 18, leo hii wemeshatimiza miaka 18, vipi haki yao ya kupiga kura?
Kuna wapiga kura wengi wamefariki, vipi majina yao?
Vipi kuhusu wakazi wapya?
 
serikali yetu bana inakwenda tu,haiangalii hayo mambo.Mimi nadhani tanzania bado haijakua kisiasa.
 
Wadau ninashangazwa& ninakerwa na tume ya uchaguz kutoboresha hil daftar au ndio ukandamizaj wa waz wa demokrasia? Hakuna waliokufa? Waliohama? Waliotimiza miaka 18 mwaka huu?
 
u even ask urself hawa watu wanafanya nn basi na wana kila kitendea kazi? nadhani ni maksudi
 
Back
Top Bottom