CWT ilipeni Serikali gharama za kesi yenu ya mgomo Kwani Maji ukiyavulia nguo lazima uyaoge

ambagae

JF-Expert Member
Mar 2, 2009
3,241
1,301
CWT Sasa sijui mlijiandaa kwa lolote litakalotokea Au ndo alimradi upepomuvume. Ilipeni Serikali sasa
 
Mbona madaktari hawakuambiwa wailipe serikali??!! Hivi kuna uwezekano wa kuishtaki hii serikali kwenye umoja wa mataifa??!!
 
CWT Sasa sijui mlijiandaa kwa lolote litakalotokea Au ndo alimradi upepomuvume. Ilipeni Serikali sasa
Inaelekea hulitakii mema hili taifa, Kwa matokeo yaliyopita ya darasa la saba, wanafunzi zaidi ya 5000 waliingia sekondari wakiwa hawajui kusoma wala kuandika, matokeo ya kidato cha nne asilimia tisa(9%) tu ndio walifaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza hadi la tatu, asilimia tisini na moja (91%) walifaulu kwa daraja la nne na sifuri. Tutarajie nini huko tuendako kama tutaendelea kuwadhalilisha waalimu? vyuo vikuu tulivyojenga vitakua vinadahili wanafunzi kutoka nje ya nchi. hii nayo ni nzuri kwani itaipunguzia serikali usumbufu wa wanafunzi wanaodai ongezeko la fedha za mikopo ya elimu ya juu.
 
Mbona madaktari hawakuambiwa wailipe serikali??!! Hivi kuna uwezekano wa kuishtaki hii serikali kwenye umoja wa mataira??!!

Wakate rufani court of appeal. Mara nyingi hizi kesi za kushinikizwa na hukumu za kuipendelea serikali zikifika huko zinakuwa quashed. Kuna vitu vingi vina walakini ambavyo jaji amejipa madaraka kuviamua ambavyo havikuwa mbele yake. Hopeless.
 
na TISS imlipe DR Ulimboka,Kila kitu kipo wazi kuwa wanahusika.
Tukianza na Ramadhani I,wa TISS.
 
Sikujua, kumbe wewe ndie unaeitwa serikali maaana umejitahidi kukazia hukumu ya huyo jaji
 
.....matokeo ya kidato cha nne asilimia tisa (9%) tu ndio walifaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza hadi la tatu, asilimia tisini na moja (91%) walifaulu kwa daraja la nne na sifuri...

Mmmmh, hii kitu ni kweli mkuu??
 
Mmmmh, hii kitu ni kweli mkuu??
Nina uhakika sana yaani sio exactly ila ni hivi daraja la kwanza hadi la tatu 9.?% daraja la nne na sifuri ni 90.?% kwa hiyo ukikaribisha kimahesabu ndiyo inakuja vile, kama huamini rejea kwenye tovuti ya MOE utafute matokeo halafu unipe majibu, huwa napenda sana watu wanaofanya utafiti ili kupata fact
 
Back
Top Bottom