Chama cha Wananchi (CUF), kitafanya ziara ya awali ya siku 15, kuanzia keshokutwa, katika mikoa sita ya Tanzania Bara na Zanzibar, kwa lengo la kuwashukuru wapiga kura na kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kushindwa kuboresha maisha yao.
Ziara hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, itafanyika katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Pwani na kisiwani Unguja, itaanza keshokutwa. Itahitimishwa Aprili 2, mwaka huu.
Katibu wa Mwenyekiti wa Chama hicho, Thomas Mongi, alisema ziara hiyo imelenga mambo makuu matatu:
Jambo la kwanza; alisema ni kuwashukuru wapigakura kwa kuipigia kura CUF katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana. La pili; kuishtaki Serikali kwa wananchi kwa kushindwa kuboresha maisha yao na kusababisha kupanda kwa gharama za maisha.
Tatu; kuitaka serikali kuhakikisha mchakato wa kupata tume huru ya uchaguzi unafanyika mapema.
Nategemea kuanza kuwaona tena Wassira na Simba kwenye vyombo vya habari wakipinga uchochezi huu.