CUF: Baadhi ya askari Geita wanafanya ‘ujambazi’

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Ijumaa, Agosti 24, 2012 05:41 Na Victor Bariety, Geita

CHAMA cha Wananchi (CUF) wilayani Geita, mkoani Geita, kimewafananisha baadhi ya askari polisi na majambazi wanaotumia sare na bunduki kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Katibu wa CUF Wilaya ya Geita, Seveline Malugu.

Alisema matendo ya unyang’anyi yanayofanywa nyakati za mchana na usiku na baadhi ya askari polisi katika mkoa huo kwa kupora mali za wananchi, zikiwamo simu za mkononi, fedha na mawe ya dhahabu kwa wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji wa dhahabu ni ya kinyama.

Alisema baadhi ya vitendo vinavyofanywa na baadhi ya askari polisi katika mkoa huo havina tofauti na majambazi na ndiyo sababu wanadiriki kuvizia wananchi kisha kuwapora vifaa vyao.

“Nimekuwa nikipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa mji wa Geita na nje ya Geita kwamba askari waliopewa dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao sasa wamekiuka ajira yao na kuwa ni askari wa kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

“Kitendo kinachofanyika muda wa usiku ni cha kinyama, kwa kuwa wananchi wanaojishughulisha na shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu hapa Geita hawana amani na wanaona askari kama adui zao, kwa sababu wamekuwa wanyang’anyi wa mali zao kwa kutumia sare za askari na bunduki za nchi na wanashindwa kuwatofautisha askari wa doria usiku na majambazi yanayovamia na kunyang’anya wananchi mali zao je?

“Wananchi wanafukuzwa wanapokuwa wanaendesha pikipiki na wakiwa na mizigo na gari za polisi zinapowakimbiza zinawabana barabarani kiasi cha kuwapatisha ajali wananchi, kwa mfano kuna mchungaji aitwaye Ngwanzalima wa Church Of God wa Kitongoji cha Kisesa alipata ajali kwa kubanwa na gari la polisi barabarani, baadaye alitelekezwa eneo la ajali wakiwahi mawe yaliyokuwa yamepakiwa katika pikipiki,” alisema Malugu.

Alisema suala hilo limekuwa la muda mrefu na inapotokea baadhi ya wananchi kwenda kuwaripoti polisi hao kwa wakubwa wao hujikuta wakibambikwa kesi za kuingia kwa jinai mgodini bila kulalamikiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita.

Alilitaja gari linalotumiwa na askari hao kupora mali za raia kuwa ni lenye namba za usajili mbili tofauti ambalo nyuma linasomeka T407 AQW, mbele ni T 601.

Akielezea tukio lililotokea Juni 18, mwaka huu, usiku, alisema gari hilo likiwa na askari saba liliwavamia na kuwapora mawe ya dhahabu pamoja na simu vijana wawili, Emanuel Mahugi na mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la George na kupigwa.

Kutokana na hali hiyo, ameandika barua yenye Kumb.Na.CUF/DS/GTD/COR/POL.3/114 kwenda kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paul, kumweleza dhuluma inayofanywa na askari hao.

Akizungumzia hali hiyo, Kamanda wa Operesheni Mkoa wa Geita, Chimacula Enock, alikiri askari wake kujihusisha na uporaji mawe ya dhahabu na kusema ameshapiga marufuku tabia hiyo, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali wale watakaobainika kufanya vitendo hivyo.

“Hii tabia ipo, ila ninachotaka kukueleza ni kwamba nilichoanza nacho ni kupiga marufuku askari kunyang’anya wananchi mawe ya dhahabu na kuwapora mali zao na nimetangaza vita dhidi ya askari wenye tabia hiyo, wakibainika sitowaonea aibu, huwezi kumpora mawe mwananchi huku ukijua amehangaika kuyapata na sisi polisi hatujafundishwa hivyo,” alisema Enock.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
hii ndio kazi ya chama cha siasa kuwasemea wanaodhulumiwa, kuonewa. safi sana CUF.
 
Inatisha kama Somalia? The only solution to these situations is administration change. Believe me!
 
Back
Top Bottom