Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,578
- 19,463
Mkuu kama kweli umeshindwa kutofautisha mgogoro wa Eastern Congo (Rwanda/Uganda) na ule wa Crimea (Ukraine/Russia) then EMT anapoteza muda wake tu hapa.
Unfortunately kama huoni similarity hiyo basi unahitaji miwani yenye nguvu sana. Kudai kuwa Crimea ilikuwa ni sehemu ya Urusi zamani kwa hiyo Urusi wana haki nayo leo ni upungufu mkubwa wa maoni; walikuwa na haki kabisa kuichukua Crimea tena mwaka 1991 wakati walipovunja muungano wa USSR na kugawana mipaka upya, lakini hawakuichukua, na badala yake wakaandikiana mktaba mwaka 1994 kuheshimu mipaka ya Ukraine kama ilivyo sasa pamoja na Crimea ikiwa ni sehemu ya Ukraine. Kwa hiyo madaia kuwa Crimea ilikuwa sehemu ya Urusi siyo kweli na wala hata Putin hajavamaia kwa kudai kuwa ilikuwa ni sehemu ya Urusi zamani.
Putin alisema kuwa ameingia pale kwenda kuwalinda watu wenye asili ya Urusi. Kwa hiyo basi iwapo swala ni watu wenye asili ya Urusi, hakuna tofauti kabisa na Rwanda/Uganda kuvamia kongo kwenda kulinda watu wenye asili ya Rwanda na Uganda walioko Kongo. Inawezekana wewe umesikia taarifa tofauti kuhusu sababu za Putin kuingia pale.
Panuka akili uachane na njia za mkato mkato kwenye mijadala.