wakimataifa
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 942
- 167
baadhi matawi mameneja wanakaa sana wengine hawana elimu ya umeneja kwa mfano tawi la dodoma meneja huyo huyo toka ilipoanzishwa bank hiyo
Hapo kwenye RED ngoja nimpigie simu Charles Kimei kama ni kweli!Hii benki mwanzoni nilikuwa nikisiakia watu wanailaumu naona kama ni majungu ila nimekuja kuprove kwamba CRDB huduma zao sio nzuri kabisa, Nimefuatilia ishu ya simu benking wiki nzima sasa na wakati najaza fomu niliambiwa ni masaa 48 na kibaya zaidi ni uongo wa wafanya kazi wao kila kitu wanasingizia systeam ilikuwa mbovu, hata kalamu ikiisha wao ni systeam ilikuwa mbovu.
Unajaza fomu wanapoteza inabidi tena ujaze upya fomu, kwa kweli wajirekebishe.
Sikumbuki kama nilijaza form ya kuomba kuunganishwa na simbanking, nakumbuka niliomba tu kwa simu na nikawapigia simu wakanipa maelezo kidogo hadi leo natumia simbanking na mwisho wa mwezi natumiwa statement kwa mail kuonyesha jinsi mpunga ulivyoteketea. Mtoa mada nakuomba ujaribu kuwasumbua kwa simu, achana na mambo ya kwenda kuonana nao face to face, naamini utafanikiwa ndani ya muda mfupi.
Kaka huu ni mwaka wa sita napokea pesa kwa njia hii... wire transfer haihitaji chochote zaidi ya jina la account, account namba jina la mtu mwenye account, adress yake, jina la bank na branch yake, swift code ambayo kwa CRDB ni CORUTZTZ...wanachelewesha sana hela hawa ni uzembe wa kitengo kinachopokea hizo transfers...hivi kwa miaka sita yote details za account yangu zimekosewa????
Wanapitia wakati mgumu sana sasa ivi kifedha (nikimaanisha liquidity) sio wanaishiwa ktk ATM ni wanamanage liquidity yao kihuni hawana maana. Haiwezekani ATM nyingi kiasi hicho zinakosa hela kila j2 haijalishi mwanzo wa mwezi au lini.Kwangu mimi wanachoniboa ni kutokuwepo hela kwenye ATM siku za weekends. Yaani siku ambazo watu tunakwenda shambani tunahitaji hela, wenyewe utakuta ATM zao hazina hela. Huwa nakereka sana.
Ila kwa huduma nyingine naona wanajitahidi, though NBC kwa sasa imeanza kufanya vizuri in terms of huduma hasa baada ya kukimbiwa kwa kasi na wateja.
Mkuu hata mm niliuna e statement na Sim banking siku hio hio bila kujaza form,ila ilikua zamani sahivii ndo kamawasemavyo wadau uzembe mwingi na steps nyingi pia...ishu mfano ya ATM card unaambiwa urudi kwa branch ulofungulia sasa si ujinga huuu??
Huenda hujajaribu NBC ukaona ubovu wa huduma uliokithiri zaidi mno.
As to me, CRDB ni benki yenye huduma bora na nzuri pengine kuliko benki nyingine zozote hapa nchini...
Wote mmeongea point ila nimependa hii ya wooden flag, kwa jumla CRDB kiaina wanajitahidi kwa viwango vyetu vya kibongobongo kwa kufanya comparison na wengine hasa kwa sie wananchi wa kawaida tusioweza kufungua a/c Bank M. Hiyo issue ya simbanking mbona wengine ilikuwa faster mno na information tunapewa kupitia kwenye email na huduma kama balanceKuwa na huduma bora kuliko nyingine haimaanishi kuwa ina huduma nzuri, utajilinganishaje afya yako na mgonjwa?
mkuu kiukweli sijakuelew kwa upande wangu banki inayoongoza kwa huduma nzuri Tanzaniaf Crdb na hili halina ubishi yaani ni kama vile kujiuliza umevaa nini wakati. upo bafuni unaoga
Mkuu Eddy,
Changamoto zote hizo ni kwa kila Bank, ninachojua kuna idara tofauti tofauti na kila moja ina majukumu yake. Kuna idara inahusika na ufunguaji na account tu. Kuna idara ya Credit, inajishughulisha na mambo ya mikopo na kuna idara ya customer service, wanahusika na kuwaelekeza wateja wapi waende kujipatia huduma kutegemeana na hitaji lake. Hilo la Tellers kujihusisha na whatsup sina uhakika sana, ila ninachojua kuna miamala ya Mpesa, tigopesa nk. Kama kweli lipo inabidi management wawazuie haraka sana.
Hapo sikuuingi mkono. Corporate wa Bank M ni wa kuhesabu. Ukienda Citibank ndiyo kabisa RM mmoja anaweza kuwahudimia. Hata staff wenyewe hawaruhusiwi kuwa na account wanapofanyia kazi. Bora ulinganishe corporate customers wa NBC,NMB na CRDB.
Hii benki mwanzoni nilikuwa nikisiakia watu wanailaumu naona kama ni majungu ila nimekuja kuprove kwamba CRDB huduma zao sio nzuri kabisa, Nimefuatilia ishu ya simu benking wiki nzima sasa na wakati najaza fomu niliambiwa ni masaa 48 na kibaya zaidi ni uongo wa wafanya kazi wao kila kitu wanasingizia systeam ilikuwa mbovu, hata kalamu ikiisha wao ni systeam ilikuwa mbovu.
Unajaza fomu wanapoteza inabidi tena ujaze upya fomu, kwa kweli wajirekebishe.
And vice versa is true@ChashaPoultryFarm hakuna bank inayotoa huduma nzuri kama Crdb trust me jaribu kuingia Nmb au Nbc uone mziki utajuta
And vice versa is true@ChashaPoultryFarm hakuna bank inayotoa huduma nzuri kama Crdb trust me jaribu kuingia Nmb au Nbc uone mziki utajuta
NMB mimi sina acaunt kule nazungumzia enki ambapo ninaingia mara kwa mara, But runk benk zote Tanzania na si CRDB, NMB na NBCAnd vice versa is true@ChashaPoultryFarm hakuna bank inayotoa huduma nzuri kama Crdb trust me jaribu kuingia Nmb au Nbc uone mziki utajuta
Aisee, nilifikiri ni mimi tu walinifanyia hii kitu, kumbe ni kawaida yao. Sijui kwa nini wanafanya haya madudu au ndo mwendelezo uleule wa wabongo kubweteka baada ya kupata mafanikio kidogokitengo cha FOREIGN TRANSFERS, au wanaopoke international money transfers ni wababaishaji sana....kawaida Telegraphic Money Transfer, kama umetumiwa kutoka nchi nyingine let's say Uingereza inapaswa pesa kuonekana kwenye account yako baada ya masaa 24 lakini hawa CRDB kwa sababu nisizozifahamu wanashikilia sana pesa za watu kabla ya kuwawekea kwenye account husika... Mimi nashangaa wanashikilia pesa za wateja kwa sababu gani? Ukienda mapokezi wanakwambia eti Value date bado.....huu ni wizi kabisa. Bank inanufaika kutokana na fees itakayokatwa kweny pesa zilizopokelewa hawana uhalali kabisa kushikilia pesa za mteja kabla ya kuzi release kwenye account yake. Sisi tunaolipwa kutoka nje tunapata shida sana unakuta pesa zimetumwa zaidi ya wiki hujazipata wakati ni kitendo cha masaa tu...