Crazy things you did in secondary school

Form One wengi walikuwa wametoka vijijini hasa hasa vya kulenga huko hakuna.

Pia wengine walikuwa wametoka MIJINI ambako hakuna vya kulenga.

Pana wakati baada ya kuishi sana Nchi za watu, nilikwenda Uturuki mjini Istanbul.

Kufika Airport Ataturk, tukaenda kupanda ndege kwenda Mikoani kwenye uwanja wa Domestic.

Kufika pale nikaona vyoo vya kuchuchumaa, nilicheka sana. Ila hata Dubai vipo.
Sikonge wewe ni noma, kumbukumbu yako sio mchezo.
Kuna kipindi magazeti yanaadimika kabisa, inakulazimu kuchana daftari la mtu.

Form I walikuwa wanakera maana walikuwa wanashindwa kulenga shimo. Ndama wengine wakiingia wanapanga magogo hadi mlangoni. Hapo inabidi mtu uingie chaka.
 
Sec raha bwana nakumbuka mshkaji alikuwa kasimama na msichana anapanga mambo yake, nikapita karibu yao na kumgusa mbavu kama kumtekenya jamaa akaachia upepo yaani aibu alinifukuzaje
 
Thanks man,
Willy Martin namkumbuka sana, si alikuja sajiliwa simba? Moshi tech napakumbuka sana, pale ndio ilikua kiwanja chetu kipindi cha UMISETA. Kuna kioja kimoja nakikumbuka hadi leo hii kilichotokea wakati tukiwa Moshi tech wakati wa UMISETA. Wakati wa kula yakaletwa mapoti ya ugali kwanza, wakati tunasubiri mboga, akaanza jamaa mmoja kudonoa ugali kama vile kuonja, mara mwingine akadonoa, mwingine kadonoa tonge kubwa kidogo, mara sereka likafumuka kila mtu akajikuta ameshika ugali wake mkononi, utamu ulikuwa pale mboga ilipoletwa na ilikuwa ni mchuzi, jamaa aliyebeba dish anatokea tu mlangoni watu wakamvamia, nyama ilikuwa haina mpango siku hiyo kwa kuwa kila mtu alikuwa anajitahidi tu angalau aloweke kipande chake cha ugali kwenye lile dishi la mchuzi!
Ahahahahahhahahahahahahhahahajajajajhajaha
 
Zile dansi za kunatana ziliniadhiri mzee mzima. Baada ya ukame mrefu wakaja mabinti kutoka Weruweru.Nikampata binti mrembo anaitwa Amina. Baada ya kunatana kwa muda kukiwa na kagiza kidogo, taa zikawashwa.Nilipatwa na uvimbe kwenye suruali yangu nikashindwa kurudi kwenda kukaa. Nikavunga kuingiza mikono mifukoni. Picha ilishaungua ikabidi nipewe pole.
Ha ha ha ha ha umetisha mkuu
 
Kuna mkurya mmoja wa kuitwa chacha tupo bafuni tunaoga kwa kawaida unatakiwa bodi(makalio)yawe ukutani sasa jamaa kajichanganya bodi kaliacha penye korido so kainama anajisugua huku kajipaka sabuni usoni kuna mshkaji wangu kaona huu upuuzi si akaenda kumgusa kwa kidole jirani ya tigo.

Jamaa akastuka na kujifuta sabuni kuangalia nyuma akamkuta jamaa yangu kaushika mpini wake yule chacha kwa hesabu za haraka akajua kagusishiwa mpini dah walitoana nje uchi mbio jamaa kaenda kumkamatia DH mbaya zaidi ilikuwa mida ya lunch mademu kibao.subiri part 2.
 
Kuna mkurya mmoja wa kuitwa chacha tupo bafuni tunaoga kwa kawaida unatakiwa bodi(makalio)yawe ukutani sasa jamaa kajichanganya bodi kaliacha penye korido so kainama anajisugua huku kajipaka sabuni usoni kuna mshkaji wangu kaona huu upuuzi si akaenda kumgusa kwa kidole jirani ya tigo.
Jamaa akastuka na kujifuta sabuni kuangalia nyuma akamkuta jamaa yangu kaushika mpini wake yule chacha kwa hesabu za haraka akajua kagusishiwa mpini dah walitoana nje uchi mbio jamaa kaenda kumkamatia DH mbaya zaidi ilikuwa mida ya lunch mademu kibao.subiri part 2.
Hahaha duh hiyo trial hatari kabisaa

Haya malizia part 2
 
Saturday was my special day nilipokuwa Old Moshi.

Nikishafua viguo vyangu inabidi nivisimamie hadi vikauke manake kuna warugaruga walikua wanaiba hadi chupi! Napanda kitandani napiga horizontal kiaina (kusomea kitandani) huku nikisubiri bati (kengele ya msosi), bati likiliita naenda na plate mbili coz mshkaji wangu mtoto wa mama wikiendi lazima aende kwao akanyonye, table leader akiniuliza namwambia "namchukulia mshkaji kenda town!" kiulaiiini najikombea double share japokuwa wengi walikuwa wanajua kuwa na 'forge'.

Baada ya kula najua siku hiyo Ushirika leo inacheza kwenye ligi kuu, siwezi kuikosa hii gemu kwa kuwa vijana walikuwa wanatisha (David Rogers, Venance Mwakalukwa, Often Martin, Martin Mahimbo, etc), nashuka zangu Shengena mbio kumuwahi mshkaji kilema kwenye wheelchair ili nipate kuingia bure uwanjani, mama wee! nakuta washkaji wameshamuwahi walee wanashuka korongoni, inabidi niende nikapande juu ya mti au ukuta, akipigwa bao mtu wakati polisi nao wanashangilia hapo ndo unaruka ndani!

Baada ya mpira ni lazima kutakuwa na harusi, mimi na masela wangu tunaenda kupiga misele kwenye kumbi za ushirka kuangalia uwezekano wa kuzamia, tukishindwa tunaenda zetu kwenye hall la wanachuo kuanagalia TV(KBC tu!), mara jamaa wanatutoa baru. Hatuna jinsi tunaingia kitandu kula mbege, mitumbo inajaa na mikojo kibao, tunaamua kwenda red house kumalizia na gongo ili tuwake vizuri!

Ukirudi school saa 4 usiku unaona washkaji wanashika pua tu, soon unagundua kuwa 'pamenuka', Mdudu mwenguvu amepiga roll call ya nguvu bila kutarajiwa na jumatatu darasani kutakuwa hapakaliki! Monitor ni mshkaji ananitonya usiwe na wasiwasi 'nilikutiki'!

Umbwe,
Siku moja na mamitungi yangu narudi school toka uswekeni, bwii na giza vikanifanya nisione kilichokuwa mbele yangu, kumbe lilikuwa ni jopo la maticha nao wametoka kuutwika! Si nikagongana na mmoja wao uso kwa uso? jamaa akaning'ang'ania na maticha wengine wote wakanirukia huku wakinilazimisha niseme mimi ni nani, I was quite famous and popular! Nikawa nafight niwatoke huku nikiongea kishwahili cha lafudhi ya kichaga na kujitetea kuwa mimi sio mwanafunzi! Nilikuwa nimevaa ki OPP nikawa nakisikia kinachanika taratibu jinsi songombingo linavyoendelea, nilifanikiwa kuponyoka na kuwaacha na kiOPP, nikatoka na moto mkubwa hadi school na ponapona yangu umeme ulikuwa umekatika, giza ndilo lililoniokoa siku hiyo otherwise ningetemwa school.
After one week napita kwenye nyumba za maticha nakaona kaflana kangu mlangoni kwa ticha mmoja anapigia deki, mii kimyaaaaa!

Katika shule zote nakumbuka jinsi ambavyo mabafu yalikuwa yakijaa baada ya debe (disco) kuisha usiku! Wee nanihii nakujua huogagi kabisa, kulikoni huku bafuni saa hizi usiku huu wa manane na kirevola chako mkononi? Blues zilikuwa zinatutesa sana na kutuchafulia suruali kwa kiwango kikubwa!
Mkuu sijui bado upo...kwenye jukwaa...? Kwakwel hii post na ya jamaa wa vita ya Kagera ni vitu ambvyo uwa vnaniondlea stress dah....shule raha bhana....
 
Kwa wale waliopita Lutengano miaka ile ya themanini na ushee, najua watakumbuka kituko cha mwalimu mmoja ambaye siku hiyo alikuwa zamu na alikuwa akiwaita wale waliokosekana kwenye roll-call ya jana yake ili awapatie adhabu. Hata alivyomaliza kuwaita, wanafunzi kwa pamoja walipiga kelele kwa kusema.
"Mwalimu acha ujiko"

Kwa rafudhi ya nyanda za juu na kifua mbele mwalimu huyo alijibu.
"Na huyo Ujiko apite mbele...!"
Ha ha ha bila shaka unaijua hii mito mkuu, kala na kipwela pia vitafunwa ni vibama
 
~Ulitengeneza water heater kwa kutumia spring za vitanda. Usiku wa manane unachemsha mahindi ya shamba la shule. Container la kuchemshia mahindi ni plastic la nje la chupa ya chai iliyoondolewa flask yake, inashikiliwa upside-down, i.e mfuniko ndo unakuwa base, na bottom yake inafunguliwa kuwa ndo mdomo wa 'sufuria' lako. Heater inawekwa kwanza katikati, then mahindi yanakatwa vipande na kupangwa around the heater.

Ukimaliza kuchemsha unarudisha waya wa umeme juu ya dari ambako ndiko connection ilikofanyika, kwani ni marufuku kutumia umeme wa socket!
Ila tulikuwa na ujasiri wa ajabu. Hizo heater ukiziangalia namna zilivyo zingeweza kuunguza mabweni kabisa
 
Mi nakumbuka primary bhana... n'na peni nyingii lakini zote za kuiba! Enzi hizo peni deal... ukiiba tu, fasta unaenda kuifikia kwenye mchanga manake unajua mwenyewe akishituka tu, wa kwanza kukaguliwa ni wezi maarufu wa peni darasani! Wakija kukukagua, holaa kumbe kitu kime-rest in sand!

Soo likitulia, hatua inayofuata ni kunyonya wino kuhamishia kwenye peni nyingine! Sometimes usipokuwa smart, unakuta peni imejaa wino hadi unachungulia-- wino wa peni tatu kwenye peni moja wapi na wapi!

Kama huna peni ya kuhamishia wino, bado sio issue! Natafuna bomba tu... la ndani(mrija) na la nje. Ukishamaliza bomba la nje unalisugua kwenye sementi-- kudadadeki, hata kama peni ilikuwa mpya inaonekana ya zamaaani!

Sema, kama uliyempiga ni mbishi mwenzako hapo hesabu atakuwa anakulia mingo tu.... ukitoka nje anakufuata nyuma nyuma manake keshakuhisi unafuata mzigo wake! Asipokufuata nyuma nyuma basi anakulia timing hadi unarudi! Unashangaa ile unarudi tu, jamaa hawa hapa wanataka wakupige search mara ya pili! Ndo pale unakuta umesachiwa mara ya kwanza ulikuwa na peni 4 lakini mara ya pili; mara eh... una peni 5! Kama alikuwa hakuzikariri lazima apate shida kufahamu yake hasa ni ipi manake ilisha-undergo evolution!

Nishakwiba sana peni no wonder passion yangu ni kuandika!
 
Nilianzishaga kamali shuleni,kwa kuanza kucheza tshs 50 na rafiki yangu badaye wanafunzi wengi wakajiunga tukawa tunacheza kwa group la watu 10-15 kwa elf 2 mbili kisha kugawana baada ya kubakia wawili.

Siku zikaenda watu wakanogewa watu prepo wakawa hawakeendi, siku moja second master kabamba watu,kila mtu akaambia aindike mwanzilishi na washiriki 10 jina langu liliandika mara 2 mbili na kila mtu
 
Back
Top Bottom