Costa Mahalu awaaambia waandishi wa habari wasome Zaburi 17 kwenye Biblia

Mahalu ukweli unaujua wewe. mimi sina shaka uliliibia taifa hili. Nafsi yako itakusuta mpaka kaburini. Unanukuu vifungu vya biblia wakati unajua fika uliiba. Mahakama zetu hazina ukweli ukiondoa Court of appeal na kidogo high court. Kisutu ndio bure kabisa, we unajua! Weka hukumu tukupe mapungufu yake! Unajua!!

Kama inakuuma si ungekuwa wewe hakimu sio wenzio wanatoa maamuzi sahihi we unaumia. Huna hata haya mtaalam wa kukosoa hukumu za wengine yakwako yamekushinda. Huwezi kujiuliza atawezaje Balozi kuhujumu uchumi bila waziri wa mambo ya nje(wakati huo Kikwete) kuhusika?
 
Mstari wa 13-14 ameshamaliza kuwaombea adui zake jinsi ya kutendwa. " Arise O Lord, dissapoint him, cast him down, deliver my soul from the wicked, which is thy sword"
 
Mi ndio maana nina mashaka kama kweli Mungu wetu ni mmoja kwa sisi binadamu wote,

Mtu "anapiga" mshiko halafu bila hata hiyana anasingizia vitabu vya mungu "comfortably"
 
Jamani namfahamu mahalu kwa ukaribu,mshiko aliiba kajenga jumba masaki kipindi hicho balaa
 
Kama inakuuma si ungekuwa wewe hakimu sio wenzio wanatoa maamuzi sahihi we unaumia. Huna hata haya mtaalam wa kukosoa hukumu za wengine yakwako yamekushinda. Huwezi kujiuliza atawezaje Balozi kuhujumu uchumi bila waziri wa mambo ya nje(wakati huo Kikwete) kuhusika?

We binti kuwa na ka akili kidogo. Kikwete was not indicted in that sabotage, it will be unfair for me to talk about Kikwete in my posting. You must be a relative of mahalu or his co-accused.
 
Alipoulizwa maoni yake kuhusu hukumu ya mahakama dhidi ya mashtaka aliyokabiliwa nayo..Prof.Costa Mahalu aliwaomba waandishi wasome zaburi 17...(very powerful verse)

Zaburi 17

1 Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila.
2 Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya adili.
3 Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku, Umenihakikisha usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,
4 Mintarafu matendo ya wanadamu; Kwa neno la midomo yako Nimejiepusha na njia za wenye jeuri.
5 Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, Hatua zangu hazikuondoshwa.
6 Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu.
7 Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kuume Uwaokoe nao wanaowaondokea.
8 Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
9 Wasinione wasio haki wanaonionea, Adui za roho yangu wanaonizunguka.
10 Wameukaza moyo wako, Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.
11 Sasa wametuzunguka hatua zetu, Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.
12 Kama mfano wa simba atakaye kurarua, Kama mwana-simba aoteaye katika maoteo yake.
13 Ee Bwana, usimame, umkabili, umwinamishe, Kwa upanga wako uniokoe nafsi na mtu mbaya.
14 Ee Bwana, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
15 Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.

Hio loss nani atailipa? Jibu kwanza ndio ulete mafungu!
 
Mi ndio maana nina mashaka kama kweli Mungu wetu ni mmoja kwa sisi binadamu wote,

Mtu "anapiga" mshiko halafu bila hata hiyana anasingizia vitabu vya mungu "comfortably"

Kama ni kweli atakuwa alitubu kwa Mungu wake ndio maana maombi yake ya mesikika, ila ushauri wa bure asidaifidia asamehe saba mara sabini, akabizi kila jambo kwa Mungu wake.
 
14 Ee Bwana, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao.
Hii inawafaa sana mafisadi wa CCM
 
Unajua hapa tunaingizana mkenge tu, hii hukumu maana yake ni;

1)Aidha hela "haikupigwa" kabisa,
2)Ilipigwa but sio na Yeye
3) Ilipigwa na yeye but under ruhusa ya mkuu
 
Costa Mahalu ni fisadi mkubwa bahati nzuri kuna kundi la wajinga linamuona shujaa wao mkubwa...kichekesho kingine Pro-Chadema wengi humu JF wapo nyuma yake wanamtetea tena wamejenga hoja eti anataka kuonewa...Pro-Chdema JF mafisadi wao ni Rostam Aziz, Chenge, Jeetu Patel, lakini Costa Mahalu mtukufu.
 
Back
Top Bottom