#COVID19 Corona: Maiti za Waafrika zitatapakaa mitaani – Melinda Gates

hamis77

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,643
19,018
MELINDA GATES, mke wa bilionea Bill Gates wa Marekani, ameonya kwamba iwapo dunia na hususani Afrika haitachukua hatua za haraka za kukabiliana na janga la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, maiti za Waafrika zitatapakaa katika kila mitaa ya Afrika mijini na Vijijini.

Bi Gates ametoa onyo hilo akizungumza na shirika la habari CNN la Marekani, kuhusu athari kubwa itakayozikumba nchi masikini duniani hususani Afrika.

Alisema moyo wake uko Afrika na kwamba ana wasiwasi mkubwa kwamba bara hilo huenda likashindwa kukabili madhara makubwa ya virusi hivyo.

“Litakuwa janga la kutisha katika nchi zinazoendelea. Baadhi ya sababu zinazoonyesha kwamba idadi haijafikia hali mbaya Afrika, ni kwa kuwa watu wengi hawapimwi kutokana na Afrika kukabiliwa na uhaba wa vifaa vya kupima na hata pale watu wanapopimwa mamlaka za Afrika zimekuwa zikificha baadhi ya taarifa na kuripoti takwimu za visa vya Corona chini ya kiwango. Kinachotokea Ecuador ni kwamba maiti zinatupwa mitaani. Jambo hili litatokea katika nchi za Afrika hivi karibuni,” amesema Melinda Gates.

Melinda ameongeza kuwa kama Afrika itaendelea kutochukua tahadhari zenye tija ni wazi kwamba mwezi May, June na July zitakuwa ni nyakati ngumu na mbaya sana kwa vifo na maambukizi yatokanayo na COVID-19.

"Nafuatilia kila kinachoendelea Afrika, natazama na kusoma kila kinachofanyika Afrika katika kupambana na Corona Virus. Ninasikitika kusema hapa kwamba Afrika bado inafanya mzaha kwenye janga hili" ameongeza Melinda.

Melinda ambaye ni mwenyekiti-mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates, ana wasiwasi hali itakuwa mbaya zaidi barani Afrika kutokana na mifumo duni ya tiba na ukosefu wa misaada ya kibinadamu.

Kwa mujibu wake, kitu muhimu alichokishuhudia ni pale China ilipoamua kuwaweka watu wake wengi chini ya karantini.
Aliongeza kwamba amewahi kutembelea miji na vitongoji vingi masikini barani Afrika na sasa anajiuliza ni vipi watu wa bara hilo watalikabili janga hili? Kwani si rahisi kuishi katika mazingira ya usafi na afya katika maeneo hayo.

Melinda ametumia fursa hiyo kuionya Afrika iache kuficha takwimu halisi za visa vya maambukizi ya Corona Virus na vifo. Amesema ni muhimu matukio hayo kutangazwa kama yalivyo ili yawezeshe si tu wananchi wengine kujua hali halisi na hatari ya janga hili ili waongeze tahadhari bali pia amesema uwazi wa hali ya COVID-19 barani Afrika utawezesha Mataifa tajiri na mashirika kufikiri namna ya kuisaidia Afrika.

Aidha Melinda amezitaka Serikali za Afrika kuwekeza zaidi katika kununua vifaa vya kukabiliana na COVID-19 ikiwemo ununuzi wa mashine za oksijen "Ventilators" na vifaa vya maabara ili kuongeza kasi ya upimaji.

NOTE: Onyo hili kutoka kwa Melinda Gates linakuja siku chache tu baada ya maonyo kama hayo kutolewa na Marekani, Shirika la Afya Duniani (WHO) na Bill Gates.

Mimi nadhani badala ya Afrika kuwachukia wanaotuonya ni vema tukafanyia kazi maonyo wanayotupatia.

Nami naamini kuwa Afrika hatupo serious hadi sasa. Mfano wakati tunapiga kelele ili mikusanyiko yote ipigwe marufuku, leo naona tangazo kuwa kumeandaliwa maombi ya kitaifa hapa Tanzania.

Yani tunasema mikusanyiko ipigwe marufuku, lakini serikali inakusanya watu kufanya maombi.

Ni lini Tanzania itafahamu na kukubali kwamba janga la Corona Virus ni tatizo la kisayansi zaidi kuliko kiroho (maombi)? Hebu tujitofautishe kidogo na KINJEKITILE Ngwale. Hizi mbinu za KINJEKITILE katika kukabiliana na Corona Virus itatuletea msiba mkubwa. Afrika iikabili Corona Virus kwa kutumia mbinu za kisayansi.

Ni lini Afrika itaukubali ukweli kuwa Corona haijui mikusanyiko ipi ni ya lazima na ipi siyo ya lazima? Corona haijui tofauti ya mikusanyiko ya maombi, Makanisani, Misikitini, vilabu vya Pombe, minada wala masoko na wala haigopi maeneo hayo.

Afrika ifahamu na kukumbuka kuwa waliotuletea taarifa Kanda Corona Virus ni wanasayansi na wala sio Wachungaji, mitume, manabii na wanasiasa. Afrika ijiulize je ni kwa nini tumewaamini wanasayansi kwamba Corona ipo na inaua haraka sana, lakini hatuwaamini na kufuata mbinu za kujikinga na kuishinda Corona Virus wanazotuelekeza? Sikiliza wataalamu, fanya vile wasemavyo ndiposa uombe Mungu. Kumbuka kuwa hata Mwinjilisti Luka Mtakatifu alikuwa Daktari na alikuwa Mwinjilisti lakini aliwatibu wagonjwa kwa dawa kwanza kabla ya maombi.

Hawa wachungaji feki, manabii na mitume wa UONGO wa leo huo unabii kuwa Corona inaweza kutoweshwa kwa maombi tu wao wameutoa wapi?

Maombi ya siku tatu tumeona matokeo yake, namba inasoma 254, tungoje haya maombi mengine ya kitaifa kama namba haijasoma 500+.

Hatukatai maombi ila sayansi iheshimiwe na ipewe kipaumbele. Serikali ikanunue ventilators za kusaidia upumuaji za kutosha zisambazwe nchi nzima na pia maabara za kupima Corona Virus zisimikwe kila Kanda na kila mkoa.

Pesa zichukuliwe kutoka mfuko wa majanga na kutoka hizi zinazochangishwa achilia mbali zile za mwenge na Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
FB_IMG_1587531300536.jpeg



 
I swear . Magufuli hawezi kununua ventilators. Zilizopo hizo hizo, na yupo radhi hio pesa amzawadie Makonda best wake kipenzi.

Kama tu aliambiwa afunge mipaka very early late Feb. akapuuza na mwezi wa tatu akakimbilia kijijini unategemea kuna rais hapo tena?
Hakuna plan. Hakuna maono. Hakuna kuangalia mbele. Hakuna kungalia madhara. Aisee. Na MATAGA pumbavu zao wanasifia tu.

Ventilators zinunuliwe za kutosha Tanzania, zisambazwe hadi hospitali za wilaya na vituo vya afya.
Tusipuuze maonyo yanayotolewa na tusifiche taarifa ee Tanzania.
 
Hili suala la takwimu na maombi yanayofanyika vinakinzana sana, either huyu mama atafungwa mdomo na muujiza wa Mungu au anayosema yatatimia na hapo sijui misimamo ya dini ya watu wengi itakuwa wapi sasa.
 
Covid19 kwa Waafrika sio inshu kubwa,tatizo litakuja hapa:- virus vitaisha huko dunian ila Afrika tutabaki navyo bila kutuua na hao wazungu wakiwa wanakuja huku watakuwa wanaambukizwa na baadae wataacha kuja kabsa Afrika na sisi hatutaruhusiwa kwenda huko kwa watu weupe.
 
Back
Top Bottom