LOWASSA ni sepp blatta na PINDA ni tenga! hakuna ulinganifu. upupa wa lowasa ni bora kuliko kutokufanya kitu kbs. pinda hana maamuzi....
Tatizo letu ni kupima utendaji kwa maneno na matendo ya jukwaani. Huyu bwana anayezungumziwa hapa hatakiwi kujadiliwa kabisa kwa jinsi alivyotumia maneno yake na kukaripia kwake ili kuwadanganya wananchi na matokeo yake ni wizi wa kutisha. Hakuna chochote kinachoweza kunasabishwa na Lowassa katika utendaji na kikawa kimefanikiwa. Hata hizo shule za kata ni initiative iliyosimamiwa na Pinda alipokuwa Tamisemi.
Hivi ule mradi wa ng'ombe aliouasisi alipokuwa waziri wa mifugo na kuwajengesha watu mabanda na kuwaahidi kuwakopesha ng'ombe ili walipe ng'ombe umeyeyuka kama mvua zake za Thailand? Hakuna aliyepata ng'ombe hata mmoja.