Comparing: Lowassa vs Pinda

anajifanya mtu wa kanisa

Hapo una maana gani mkuu!au ni ile issue ya kuomba msamaha kanisa?kama ni hivyo basi wewe una matatizo na ukristu,ukristu ulikuwepo,upo na utaendelea kuwepo hata mfanye nini hamtoweza kamwe kuutokomeza ukristu.Mnapoteza muda wenu bure!!
 
munamuonaje PINDA-si mchapa kazi, anajiliza, analalamika maofisa kununua magari ya bei juu,hapingii rushwa kivitendo,ni ndumila kuwili (leo A kesho Z),anajifanya mtu wa kanisa,mtoto wa mkulima (bora angekuwa mtoto wa bilionea) anayechekelea nchii ikiangamia,

LOWASA-ni mchapa kazi anayeogopwa na maofisa wenzake serikalini (sifa muhimu),ana ujasiri na kujua maana ya cheo chake ni fisadi kivitendo (hana tofauti na PINDA asiyeupinga ufisadi).

hapa ni bora nchi kuwa na lowasa fisadi mchapakazi, kuliko PINDA mpalilia ufisadi asiyechapa kazi?

Well said! Big UP!
 
Kuna mtu aliuliza kwanini tunamlinganisha Lowassa na Pinda,why not Lowassa and Magufuli; Lowassa and Mwakyembe: Lowassa and Sitta??

Magufuli and Mwakyembe;Magufuli and Sitta;Sitta and Mwakyembe????yaani its like nasoma the same thread every week.....hivi akiwa marehemu by 2015???? Lets talk about other options basi???ni mtizamo tu jamani!
 
Tuko boti moja!Naona hoja hapa ni yupi bora kati ya MWIZI MCHAPAKAZI LOWASSA na MPOLE MDHAIFU PINDA..Mie kwa upande wangu ni bora Mpole Mdhaifu Pinda!
ni bora jambazi kuliko RPC (POLISI BOSI MKOA) anayeelekeza vikosi vya usalama vielekee mashariki mwa mji ili majambazi yapore magharibi mwa mji baadae apate mgao wake kutoka kwa majambazi. JAMBAZI KILA WAKATI TUTAMKWEPA ILA RPC TUTAMKIMBILIA KUMBE ATATUTEKETEZA

 
Kalale naona umechoka. Utaachiwa nchi hii jangwa na mashimo. Fisadi hana huruma na mtuu bidii yake kuchumia tumbo anatumia cover ya hard work kuharalisha ujambazi wake. Fisadi hafai ndg yangu, hapo umechemsha usimfagilie mwizi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Jaman hapa ni PINDA vs LOWASA tu na si wengineo.Hivi kama PINDA anatetea Dowans utamtofautishaje na Lowasa?Hivi kuua au kujaribu kuua ni makosa tofauti yasiohukumika na vifungu vinavyofanana?

 
Pinda anajua ukweli wote na nimchapa ila anashindwa kutekeleza tokana na kuzidiwa na mafisadi

nincho mshangaa kwa nn haachii ngazi?
Maana kweli anaumia jinsi mambo yanavyo endeshwa na mkwere.........

Kwanza unajua kuwa pale sumbawanga pinda hatakiwi kabisa baada ya mafisadi kumtuma akampitishe mmbunge wa sumbawanga kwanjia za panya........toka that day wanachi walimchukia kabisa
 
Hapo una maana gani mkuu!au ni ile issue ya kuomba msamaha kanisa?kama ni hivyo basi wewe una matatizo na ukristu,ukristu ulikuwepo,upo na utaendelea kuwepo hata mfanye nini hamtoweza kamwe kuutokomeza ukristu.Mnapoteza muda wenu bure!!
mwanzilishi wa hii sredi ni mimi marytina ni mkristo , EL ni mkristo wote tunajua ,inaelekea wewe uko tayari kumpa kura mtu wa dini yako hata kama ni mchafu MBONA UNAMAWAZO YA UDINI UDINI sana. ANAJIFANYA MTU WA KANISA NAMAANISHA ANAJIFANYA MTU WA MATENDO MASAFI ( wote twajua viongozi wa makanisa wanavyojitahidi kuwa na matendo masafi)

 
Kwa anaye mjua yule legwainani yule!!atakubaliana na mimi kwama EL nimchapa kazi uwezi kumlinganiha na pinda japo kila mmoja anamapungufu yake!!Kwanza anayekumbuka sakata la mnazi mmoja,sakata la city water hivyo niujasiri kwanza akiwa waziri wa mifugo na maji aliwawekea wananchiwake maji,Mabwawa yakutosha hakuna shida ya maji,akiwa waziri mkuu akawawekea mjiwao kwenye mazingira safi,rami,miradi,Na alikuwa na mipango yakupitisha barabara hadi serengeti kupitia monduli,Shule za kata ndo usiseme the guy is :A S thumbs_up:
 
Hivi nanyi ni majuha? Mnajadili bora Lowasa bora pinda bora lowasa bora pinda!..Lowasa ni mwizi,fisadi,mshirikina,Mnafiki, pinda ni Mnafiki,mvivu kutimiza wajibu,mwoga,Hafai! ..Wenye ufahamu watanielewa.
 
Kuna mtu aliuliza kwanini tunamlinganisha Lowassa na Pinda,why not Lowassa and Magufuli; Lowassa and Mwakyembe: Lowassa and Sitta??

Magufuli and Mwakyembe;Magufuli and Sitta;Sitta and Mwakyembe????yaani its like nasoma the same thread every week.....hivi akiwa marehemu by 2015???? Lets talk about other options basi???ni mtizamo tu jamani!
I concur with u.
 
hata kama ni MWIZI always LOWASSA amekuwa mchapa kazi na ni mtu mwenye maamuzi bila kuogopa


Wezi wote huchapa kazi...kwa hiyo Lowasa aendelee kuiba tu, hamna shida, ila uongozi asahau kwa kweli.....
Tena siku hizi hata yeye amekata tamaa, juzijuzi alionekana Billila Lodge anatetemeka mikono kwa kubwia maWhisky mengi ili kupunguza msongo wa mawazo! Ama kweli pesa haileti raha kamwe!
 
Nakuunga mkono Marytina.

Hata hizi shule za kata wanazojivunia CCM, na ambazo mamia ya maelfu ya wanetu wanasoma huko pamoja na mapungufu yake, ni 101% kazi ya Lowassa.

Katika kuchagua mashetani wawili kwa kweli nitamchagua Lowassa...

two wrongs don't make right!hao wote ni sawa na pipa na mfuniko...na hizi post za hivi anzianzisahga nani??oops mi mwenyewe nimeshachangia ...smtmz ni kuziignore tu
 
Kwa anaye mjua yule legwainani yule!!atakubaliana na mimi kwama EL nimchapa kazi uwezi kumlinganiha na pinda japo kila mmoja anamapungufu yake!!Kwanza anayekumbuka sakata la mnazi mmoja,sakata la city water hivyo niujasiri kwanza akiwa waziri wa mifugo na maji aliwawekea wananchiwake maji,Mabwawa yakutosha hakuna shida ya maji,akiwa waziri mkuu akawawekea mjiwao kwenye mazingira safi,rami,miradi,Na alikuwa na mipango yakupitisha barabara hadi serengeti kupitia monduli,Shule za kata ndo usiseme the guy is :A S thumbs_up:

Haha, Monduli hakuna hata maji ya kunywa unasifia uongo huu?
Mie nilienda Monduli juu kuna shida sana: wanachi na ng'mbe , punda na mbwa hunywa , huoga na kufulia kwenye mabwawa machafu sana. Amini nikwambialo, huwezi kunywa yale maji weqwe kama si mwenyeji!
Ila jamaa anawajulia wamasai sana: Huwa anawachomea nyama na yakila tu, utayasikia yanavyoruka na kumsifia! Jamaa ni fisadi, period, na hilo linamwondolea sifa zozote alizokuwa amebakiza.
Kumsifu Lowasa kuwa ni mchapa kazi, ni sawa na kumsifu Maddof, aliyeyeendesha Wall Street kwa weledi mkubwa wa kitapeli kwa miaka mingi. Lakini , wazungu husema , Crime does NOT pay in the long run: Si umeona Economic crisis ya dunia? Mwanzilishi wa ushenzi huu mnaouita uchapa kazi ni Maddoff. Sasa hivi ananyea ndoo kwenye jela za Marekani, na ni aibu mtu kulitaja hata jina lake. Hata watoto wake wanaona aibu kwamba huyo ndiye baba yao, aliyeyumbisha uchumi wa dunia.
Ni udhaifu mkubwa wa akili kujaribu kumsifu mwizi kwamba ni mchapa kazi. Ujasiri huu umeutoa wapi?
Lowasa ,ni mtu wa kutia shaka, na mahali pekee anapoweza kupewa uongozi ni gerezani.....
 
IFUATAYO ni hotuba fupi aliyoitoa Waziri Mkuu Edward Lowassa katika Bunge mjini Dodoma leo (Alhamisi Feb. 7, 2008) asubuhi, wakati wa mjadala wa Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi "Richmond Development Company LLC" ya Huston, Texas, Marekani mwaka 2006:

"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.



Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli.



Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice".

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.
Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.


Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.


Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.

Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.


Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?


Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.


Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.


Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili.

Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawshukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.


Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru
Nimejiuliza na kutafakari, ni mtanzania gani mwenye uwezo wa kuachia utamu baada ya kutuhumiwa? kitendo cha Lowasa kujiuzulu kilikuwa ni cha kiungwana, kila mtu angetake responsibilty kama Lowasa nchi hii ingekuwa mbali, Bravo Lowasa, you are the Man to beat come 2015
 
mimi sipo hapa kujua yupi bora kuliko mwingine ninachojua ni kuwa any QUESTION DESCRIBES HOW INTELLIGENT A MAN IS na the ANSWER GIVEN DESCRIBES HOW WISW A MAN IS. kwa maana hiyo kila mmoja ana mapungufu yake, ila kiukweli ya pinda yamezidi lowassa was much better though he's a cruke. :kev:
 
si kweli,wengi wanaojua mambo na kuyaangalia katika upeo na ukweli wake watakubaliana nami kuwa Lowasa ni kiongozi na mtawala mchapa kazi wa kweli kuliko kiongozi yeyote nani ya CCM,wengi ni wanafki ila Lowasa sio mnafki na alitolewa mbuzi wa sadaka ndio hapo matatizo yalipoanza,CCM wakimsimamisha Lowasa kugombea Uraisi 2015 japo hawatashinda lakini wataisumbua CHADEMA kuliko kumsimamisha JUHA mwingine yeyote

Narudia tena, mwizi si mchapa kazi, mwizi ni criminal na sehemu yake ni jela.
 
Back
Top Bottom