COMPARE & CONTRAST: Turkish vs Chinese Infrastructure (SGR) loan to Tanzania

baadaya hizi porojo zote reli haitojengwa kenya watatupiga gap inchi itaendelea kuwa nyuma sie tutaendelea kunywa gahawa kipaji chetu watanzania
 
Mkuu jifunze kuwaheshimu wenzio unaojadiliana nao. Tabia ya kujifanya unawaita trolls si nzuri na si ya kiungwana.

Tukija kwenye hoja unayoleta mezani na kulazimisha kuuaminisha umma kuwa una data za kutosha ni kuwapotosha bila wao wenyewe kujua.

Nimeona unawakandia waliopropose gharama za ujenzi bila sababu za msingi. Zaidi umeweka bla bla na stori za kuunga unga.

Kwa ufupi hoja kuwa Mh. alijifungia na kusoma documents ina madhaifu mengi nit
Threads za CCM na CHADEMA nyingi ni za TROLLS na zimeshusha sana heshima ya JAMBO FORUMS
Hapa nazungumza kama veteran. Wabatuharibia focus kwenye mambo ya maana ya nchi.
 
Mimi ni mmojawapo wa watu ambao huwa sichelei kumpinga Magufuli pale anapokosea.Lakini huwa pia silazi damu " kwenda naye maili mbili" pale anapofanya vitu vya kutukuka.Kwa hili la Wachina kama ni kweli kutaka kupiga pesa kwenye suala la SGR namuunga mknono kama kweli ameshitukia dili! Serikali ya JK ama kweli imetufanya tuishi kama konokono" ! Hivi kweli kweli JK alikuwa Raisi(chip) au Rahisi(cheap)?
MKUU PUNGUZA CHUKI NA KWA RAISI ALIYEPITA, huu mradi ni jk ndo alosaidia kuleta wazo na kuleta wachina kama facilitators, hakufanya chochote zaidi ya kuweka momerandom of understanding nao! So issues za negotiation na uzabuni zilikuwa zinafanywa kipindi hiki na awamu ya tano! wamekuja kupigana chini kwenye zabuni ya ujenzi, waturuki wamekuja na gharama ya chini kuliko wachina watoa pesa! kwa kanuni za ki tenda unampa ambaye ana gharama za chini kwa kazi hiyo, so inaelekea Serikali imevutiwa na gharama ya waturuki! wachina wamegoma kutoa pesa kwamba how comes pesa nikupe mimi penzi utoe kwa mwingine?? hizi zingine zooote ni porojo!
 
HNIC,

..ninavyokumbuka RWANDA ndiyo walipewa jukumu la kuitisha tender ya reli ya Dsm Isaka Keza Kigali Musongati.

..tena hata ukifuatilia kwenye mtandao utaona walishafikia hatua wame-short list wakandarasi kama 6 toka China, Russia, Turkey, ...

..Je ina maana sasa Rwanda hawahusiki na zoezi la kutafuta/kuchagua mkandarasi wa mradi?

..vilevile uelewa wangu ni kwamba reli itajengwa kwa kiwango cha standard gauge mwanzo mwisho. Nimeshtuka kidogo unaposema standard gauge ni kutoka Isaka kwenda Kigali/Rwanda na Musungati/Burundi.

..Pia kuna tawi la reli kuelekea KIGOMA. Naomba utueleze kuhusu kipande hicho cha reli.
 
Threads za CCM na CHADEMA nyingi ni za TROLLS na zimeshusha sana heshima ya JAMBO FORUMS
Hapa nazungumza kama veteran. Wabatuharibia focus kwenye mambo ya maana ya nchi.
Nimeupdate hoja zangu kama hutojali zipitie na utupatie feedback. Yapo kwenye post uliyoquate.

Pili nisisitive weka maoni yako bila kuwadharirisha wengine, humu GT kibao ila wakati mwingine wanajifanya wehu.
 
Fisadi Lowasa ndiyo anahusika na saga zima la Tanesco!
Lowasa kaingiaje kwenye hii mada? Hadi mda huu hakuna jina la aliyehusika kusaini aliyetajwa. Huwezi kusubiri hadi mleta mada akafikia tamati ili tuanze kumbana kwa maswali?
 
Hapo ndio ninapoipenda jamii forums,watu wanalete habari za uchambuzi na kwa kina.Si mambo ya kishilawadu.Hata mi nilikuwa nashangaa hii ishu ilivyokuwa inakwenda.Wakati wa awamu ya 4 hasa Marehemu Sitta alipopewa wizara ya miundombini tulisikia wachina ndio watajenga.Na kama sikosei walijunga kama 2 km maeneo ya Soga Pwani.
tukaambiwa serikali inaongea na Rothschilds kuhusu kufainensi huu mradi.hatujui waliishia wapi.Kaka hebu pumzika jipange tuletee vitu vilivyojaa
Maana watu wameshaanza kulaumu kuhusu hii ishu.Naamini JPM kuna siku atakuja kuzungumza kwa undani hii ishu.
 
Yaani mtu mmoja tu kajifungia akatoka hapo akapiga chini recommendation za wataalam wengine wengi walioshiriki kudraft huo mradi?

Kwani huo mradi haujawahi kuwa briefed ktk baraza la mawaziri na wakakubaliana ufanywe na mchina?

Kwani ni mangapi tumejaribu kuyafanya tofauti na awamu iliyopita halafu baadae tukakaa chini na kugundua kumbe kwa mujibu wa mazingira yetu kumbe ni uamuzi sahihi ulikuwa umechukuliwa?
 
Mkuu jifunze kuwaheshimu wenzio unaojadiliana nao. Tabia ya kujifanya unawaita trolls si nzuri na si ya kiungwana.

Tukija kwenye hoja unayoleta mezani na kulazimisha kuuaminisha umma kuwa una data za kutosha ni kuwapotosha bila wao wenyewe kujua.

Nimeona unawakandia waliopropose gharama za ujenzi bila sababu za msingi. Zaidi umeweka bla bla na stori za kuunga unga.

Kwa ufupi hoja kuwa Mh. alijifungia na kusoma documents ina madhaifu mengi nitaeleza jambo moja kwa kifupi sana kuhusiana na hii dhana kuwa gharama zimekuwa inflated:

1. Unapotuambia kuwa Mh. Rais alikaa na kujifungia weekend nzima kupitia gharama halisi bila kuhitaji ushauri wa kitaalam, hili ni ajabu linapatikana Tanzania tu. Ni jambo la ajabu sana kwa kuwa kwanza Mh. Rais si QS wala Engineer kuweza kufanya kazi hii. Natambua italetwa hoja dhaifu ya kuwa ana experience na wizara ya ujenzi. Hoja ni dhaifu zaidi kwa sababu tatu kubwa:

  • Mtu mmoja hawezi kureview kazi ya QS na kurukia kuwa kuna makosa au ipo sawa ndani ya weekend moja. Ukizingatia ukubwa wa kazi yenyewe hili jambo haliwezekani kufanywa na mtu mmoja (labda tutafute robot lenye super computer kichwani)
  • Uzoefu wa wizara ya ujenzi hapa hauna nafasi. Hapa unajenga reli sio barabara na sio tu unajenga reli, unajenga reli ambayo Tanzania haijawahi kuwepo na hatuna experience nayo. Design ya reli, engineering, costing na project nzima ni tofauti sana na ile ya barabara na si tofauti ndogo. Hapa panahitaji mtaalam mbobezi kwenye masuala ya Railway engineering.
  • Tatu mabadiliko ya gharama ( kwa ukubwa huu) hayawezi sababishwa na upigaji pekee, tena sio kwa project kubwa kama hii ya reli. Mabadiliko yanaweza kusababishwa na financing structure, design ( reli inaweza kuwa ile ile ila baadhi ya vitu vikapunguzwa ikiwamo terminals na supportive structures) , aina ya contractor, management structure mradi ukikamilika n.k
Taifa hili linatakiwa kuendeshwa kwa misingi ya kitaalam wala sio hisia. Naamini wataalam wote wa mwanzo ( waliofanya feasibility studies) walitoa project costs tuwekee hapa tuangalie variations.

Hii tenda ilishatangazwa na mshindi alishapatikana ( nanukuu taarifa ya ZZK), tupatie taarifa za waliobid na viwango walivyoweka ni vema kuzingatia hata hawa hawakuweka gharama zote za mradi. Hili litatusaidia kujua kama gharama zilikuwa inflated. Mtu mmoja hatoshi kuconclude kuwa tumepigwa ignoring wataalamu wa serikali ya awamu iliyopita, 4 feasility consultants na contractors waliobid.

Yes, Mh. Jakaya hapendwi na watu kadhaa ila tusimhukumu kwa bila ushahidi wa msingi.


Sasa CHADEMA trolls wanapokuja kujadili rangi ya shati la waziri January inasaidia nini kwa JAMIIFORUMS members?
Sasa CCM trolls wanapokuja kujadili Dr Silaa anatembea na nani inasaidiaa nini JAMIIFORUMS members?

Issue yangu ni Trolls wanatuharibia quality ya mijadala humu JF na kwa hilo i won't apologise for calling them out
 
Sasa CHADEMA trolls wanapokuja kujadili rangi ya shati la waziri January inasaidia nini kwa JAMIIFORUMS members?
Sasa CCM trolls wanapokuja kujadili Dr Silaa anatembea na nani inasaidiaa nini JAMIIFORUMS members?

Issue yangu ni Trolls wanatuharibia quality ya mijadala humu JF na kwa hilo i won't apologise for calling them out

Hili tuachane nalo; Je would you shade some light kwa kujibu hoja zetu?
 
Back
Top Bottom