Commercial arcade gaming centre

Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,289
781
Salam wakuu,
mlioko mjini (dar), hivi wazo la kuwa gaming centre yenye machine za kisasa inaweza kulipa?
Tafadhali nijuzeni, kama kuna game centre yenye mashine za kisasa wanatoza bei gani (kwa saa,.au vinginevyo?). Pia nahitaji mawazo, ni mji gani tena unaweza kuwa na wapenzi wengi wa video games? Nisaidieni mawazo wakuu, miji ya wenzetu sehem kama hizi vijana na watu wazima wako adicted na wanajaa hasa kucheza games, nashikwa na tamaa lakn bado inantia shaka sana, hasa ukizingatia bei ya mashine zenyewe (6-10M/set), ukianza na set 10 hv, ukijumlisha pango na gharama zingine ni zaidi ya 150, ITALIPA KWELI?
Natanguliza shukrani

atvtrack.jpg needforspeed-underground.gif.jpeg
 
Mwanajamii Amoeba inalipa! Huwezi amini lakini nchi nzima watu wengi wamekuwa addicted na kamari na bahati nasibu!

Ni kupata location nzuri na usalama ndicho unachohitaji! Keep it up!
 
Amoeba,
mi nimekuwa nafuatilia sana uwezekano wa kufanya biashara hii ya games. kuna baadhi ya games itakuwa ngumu kulipa labda kama utakuwa na massive marketing campaigns ili watu wapate mwamko. watu wengi wanaopenda games ni rika ambalo halina kipato, lika lenye kipato wanajua pool table tu. mi nilijaribu kuweka mini soccer table maeneo flani haikulipa hata. sijui kama kuna video games ambazo zimetengenezwa kuruhusu michezo ya kibiashara (labda malipo kwa game moja ya soccer, au kombat), hiyo inaweza lipa maana inaweza kuwa na tija kutokana na kuwa na wapenzi wengi hata uswahilini.
 
hakuna wazo la biashara lislolipa... muhimu ni nia... kujua soko ... na juhudi tu!
 
Salam wakuu,
mlioko mjini (dar), hivi wazo la kuwa gaming centre yenye machine za kisasa inaweza kulipa?
Tafadhali nijuzeni, kama kuna game centre yenye mashine za kisasa wanatoza bei gani (kwa saa,.au vinginevyo?). Pia nahitaji mawazo, ni mji gani tena unaweza kuwa na wapenzi wengi wa video games? Nisaidieni mawazo wakuu, miji ya wenzetu sehem kama hizi vijana na watu wazima wako adicted na wanajaa hasa kucheza games, nashikwa na tamaa lakn bado inantia shaka sana, hasa ukizingatia bei ya mashine zenyewe (6-10M/set), ukianza na set 10 hv, ukijumlisha pango na gharama zingine ni zaidi ya 150, ITALIPA KWELI?
Natanguliza shukrani

View attachment 15360View attachment 15361

Ni Biashara inayolipa ukipata location nzuri...
 
..Kuna Mtu alijaribu kwa muda mfupi pale Langoni mwa kuingilia Ubungo Plaza upande wa kushoto lakini naona hakuchukua muda. sasa hivi kama sikosei pana ofisi ya Tours kama sikosei
 
Hailipi kuna mwingine alifunga pale mtaa wa Makunganya karibu na TNT na alikuwa na game za kila aina,lakini wapi ikaishia kuwa jumba la makumbusho
 
italipa,utahitaji location nzuri,lakini usitarajie ROI ya haraka,kwa mtaji wa mili150 nadhani itakuchukua miaka 4-5kurudisha faida.njia nzuri angalia uwezekano wa kuhama hama miji kila baada ya mwezi hivi,its like a circus-fete,walikuwa wanakuja kidongo chekundu ,pale mmnazi mmoja ,miaka ya 1984-1989 kulikuwa na mary go round,magari ya umeme etc,by then nilikuwa nalipa sh.100 per game,wakati huo nauli ya basi ilikuwa sh5,so unaweza kulinganisha thamani ya shilingi wakati huo.
ili ikulipe itabidi ucharge around 4-5,000 per game
 
Back
Top Bottom