TANZIA Christian Atsu apatikana ndani ya kifusi Uturuki akiwa amefariki dunia

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Christian Atsu amepatikana ndani ya kifusi siku 12 baadaye baada ya tetemeko la ardhi kuikumba Uturuki na Syria.

Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa na wakala wake anayeitwa Nana Sechere

Pia soma
- Mchezaji wa kimataifa kutoka Ghana anaswa kwenye vifusi nchini Uturuki

====

Nana Sechere ambaye ni Wakala wake amethibitisha kupitia Twitter kuwa mwili wa Atsu umepatikana leo asubuhi ikiwa karibu Wiki 2 tangu aliporipotiwa kutoweka baada ya kutokea Tetemeko la Ardhi Nchini humo.

Christian Atsu kutoka Ghana, aliwahi kucheza na timu za Ligi Kuu ya Uingereza (Everton, Chelsea na Newcastle) baadaye alijiunga na Hatayspor ya Uturuki Septemba 2022 na kufunga bao la ushindi kwenye mechi ya Super Lig, siku 1 kabla ya Tetemeko.

Awali, Klabu ya Hatayspor iliripoti kuwa Mchezaji huyo aliokolewa na kukimbizwa Hospitali lakini siku moja baadaye ilikanusha. Matetemeko mawili yenye kipimo cha Richa 78 na 7.6 yalizipiga Uturuki na Syria Feb. 6, 2023 ambapo hadi sasa Vifo vimepita 45,000.

atsu Family.jpg

Christian Atsu akiwa na Familia yake enzi za uhai wake
BBC
 
Inasikitisha sana. Halafu unaambiwa alikuwa ndiyo yuko hatua za mwisho kabisa kuondoka Uturuki, ili kwenda kutafuta malisho sehemu nyingine! Ila mwisho wa siku, tetemeko limemuondoa duniani!
 
R.I.P

Kuna mtu alianzisha uzi akisema alipatikana mzima kumbe zilikua tetesi tu
Ilikuwa uongo pia, soma hapa

Sechere was told that Atsu was in the hospital and stable, but had not heard from him. On Wednesday, February 9 Hatayspor announced that he was still missing.
 
Back
Top Bottom