Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 401
Ndugu zangu,
Mojawapo ya udhaifu wa kiongozi wetu wa sasa ni kitu tunachoita ulimbukeni. Kwa wasio wachunguzi wa mambo ni vigumu kuamini nachosema. Lakini rais wetu ni limbukeni tena haswa. Anajisikia, analinga na kwa lugha ya wenzetu akina dada anajishaua. Kwa sisi tuliobahatika kuwa karibu nae, tunamfahamu. Tabia yake hiyo ni 'unique', inamtofautisha sana na marais waliopita. Ni limbukeni ambaye urais kwake ni fahari na ndiyo maana pamoja na gharama yake kubwa, safari za nje haziishi. Ebu fikiria kiongozi wa nchi akiwa kwenye ziara za kiserikali katika nchi ya kigeni anapataje muda wa kubembea na mkewe kama watoto wa chekechekea na mbaya anakubali hata kupigwa picha!!! Hata iweje, Mzee Mkapa hawezi kufanya jambo hilo kamwe.
Ndiyo maana nasema tatizo ni ulimbukeni, upenda majivuno, kujisikia na ku-pretend kujua kila kitu. Anapokuwa anajadiliana na surbodinates hujifanya kila kitu anajua. Kwa tabia hiyo, anakosa mawazo mengi mazuri kutoka kwa wasaidizi wake. Kuna rafiki yangu mmoja ambaye mpaka sasa bado ni waziri aliwahi kuniambia kwamba wanapokuwa kwenye vikao vya baraza la mawaziri ambavyo yeye huwa ndiye mwenyekiti, huwa wanakuwa na fursa finyu sana ya kuchangia mawazo yao hata kama suala linalojadiliwa linahusu sekta fulani ambayo waziri wake yupo. Muda mwingi anaongea mwenyekiti tena basi bora hata maongezi yenyewe yangekuwa ya maana. Huyo waziri anasema walikuwa wanamfurahia sana Dr. Shein anapoachiwa uenyekiti wa kikao kwani yeye hakuwa mwongeaji sana na alikuwa anatoa fursa kwa waziri mwenye sekta kuelezea jambo na kutoa mapendekezo yake. Na walikuwa wanatumia muda mfupi zaidi kujadilia masuala mengi na ya msingi.
Ndugu zangu rais wetu ana udhaifu mwingi lakini huu wa ulimbukeni nao umechangia kuyumba kwa nchi yetu kiuongozi. Wito wangu kwenu ni kama kichwa cha thread hii kinavyosema 'tusidiriki tena kuchagua kiongozi mwenye tabia ya ulimbukeni'. Badala ya kukaa na kufikiria matatizo ya wananchi na namna ya kuyatatua, yeye atakuwa anafikiria ni suti ipi atakayovaa kesho kwenye hafla fulani au atembelee nchi gani (kwa kisingizio cha kuomba misaada). Tukifanya hivyo, tutaliwa tena.