Uchaguzi 2020 Chini ya CHADEMA, elimu ya msingi itakuwa miaka tisa

Sisi kama nchi huru kuna mambo tunapaswa kujisimamia kama nchi kama tulivyojisimamia kwenye corona, sio research zifanyike Bangladesh na Nepal sisi tumeze tu kama dodoki.

Kafilipino kenye miaka 15 utafikiri kana miaka minne, sisi mtoto wa mika tisa keshaanza kuota chuchu, sio mtu aende kwenye kongamano unesco kwa wazungu atuletee kabrash tumeze, hapana.

Hawa chadema wasitake kujipendekeza kwa wazungu kuonyesha wana comply, hapana, lazima tutathimini mazingira tuliyo nayo, mtoto unakomaa nae Feza boys au Marian unatamani asome miaka minne amalize shule namna ada inavyokupeleka mchakamchaka.
Mkuu kwanza ungeangalia mfumo wa elimu wanchi kama India kwa nchi yetu naona unatufaa, kule elimu yao zaidi ya asilimia 70 yaelimu yao baada yamtu kuhitimu kidato cha nne nipractical tu.
 
..hao ni wale ma-GENIOUS.

..mtoto wa kawaida anakwenda hivyo nilivyokueleza.

..sisi miaka yetu watoto walikuwa wanaanza darasa la kwanza wakiwa na miaka 9.

..tulikuwa tunapimwa kwa kushika sikio; mkono wa kulia uguse sikio la kushoto ndipo uandikishwe shule.
Primary school ilikuwa miaka 8 yaani std 1 to std 8
Baadae iliondolewa std 8 ikabakia std 1 to std 7
Sababu ya kuondoa std 8 ilikuwa kuharakisha kijana kwenda secondary, pia kazi alizokuwa anafanya primary school leaver ziliwekwa kwa watu waliomaliza std 12 yaani form four.
Kindergarten haikuwa compulsory miaka hiyo,hivyo ndio kusema primary school ya miaka 9 imerudi.Ila sijui kwanini waongeze muda wa primary wakati dunia inazidi kupunguza muda wa primary.
 
Mkuu sera ya elimu is not a copy paste affair lazima ufanye utafiti ujiridhishe kwa kufuata falsafa na sera za nchi.

Elimu inapaswa kuwa zao la jamii na sera lazima zilireflect jamii husika.
Jambo kubwa tunalotafuta hapa au kuboresha katika elimu yetu nimna muhitimu anavyoweza kujiajili baada yakumaliza elimu yake, au muhitum anaajirika baada yakumaliza elimu yake?.

Kwa mfumo waelimu yetu naomba uniambie form five na six vinamsaidia vipi mwanafunz katika maisha yakawaida.Zaman shule kama mazengo mtu alikua aliingia form three anaachana na baadhi yamasomo ambayo ktk career yake hayatakua namsaida.
 
Hii ilani ya chadema kwa kila nyanja inasisitiza ushirikishwaji wa sekta binafsi, lakini kwenye Elimu hawajagusia kabisa ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye Elimu, nilitegemea wangekuja na idea ya kutoa ruzuku kwa shule binafsi ziweze kupunguza ada na kujiendesha kwa ufanisi kwani hawa private na public schools ni watoto wa baba mmoja Tamisemi.

Nilitegemea wangeongelea vyuo vikuu vya private kupatiwa ruzuku za maboresho hasa kuwasomeshea wahadhiri badala ya sasa ya kuvifungia kisa havina maprofesa, kwa maisha ya leo hakuna profesa anayezagaa mtaani labda awe mstaafu au chapombe au ziko tenge kidogo. Lakini hawajagusia kabisa. Sasa hiyo private sector integration and partnership ni kwenye madini umeme na biashara tu? kwenye elimu vipi?
 
Hilo pia tuwaulize ccm kwa nini wanashindwa kutoa ruzuku kwa private schools angalau washushe ada?.
 
Kwa hiyo shida ya elimu yetu ni idadi ya miaka?

Kwamba hao wanaohitimu msingi pasi kujua KKK wakiongezewa miaka miwili wanajua automatically tu!

Kuna utafiti wowote juu ya hili?
 
Chadema ni wababaishaji tu, kila mtu akisimama jukwaani utasikia, "Risasi 16" mara risasi 64 bado zingine zimo kiunoni, yaani maajabu tu. Jana mke wa mgombea wao kasema tena huku anatoatoa vimachozi mambo hayo hayo ili wananchi wamuhurumie!! hakuna kura za huruma hapa, mtu ukae ulaya upangwe na mabeberu kuja nchini kutaka kubaka kura kwa kigezo cha huruma
Huna point, unadandia dandia tu angalia usije ukadandiwa
 
Nimeisoma ilani ya CHADEMA sura ya tano ibara ya saba kifungu "e" nimekiambatanisha hapa chini, kinasema ili kuboresha elimu shule ya msingi itakuwa miaka tisa, binafsi ningependa shule ya msingi iwe miaka mitano, lengo la shule ya msingi kama lilivyo ainishwa na Friedrich Froebel ni kumuandaa mtoto kuanza maisha ya elimu na sio kumpa stadi za maisha.

Halafu kifungu "f" wanasema wata integrate na elimu ya ufundi yaani mwanangu anapenda kuwa daktari unaanza na kumfundisha uchomeleaji vyuma, naona sio sawa. Hebu tuiache elimu kama ilivyoasisiwa na akina Friedrich Froebel na Johann Friedrich Oberlin. Pamoja na kasoro ndogondogo ilani ina mambo mazuri pia ni bora wakatumia muda wao kuyaelezea.View attachment 1556345
Uchaguzi mwepesi sana huu
Tunatakiwa tuchague vitu na maneno matupu
 
Primary school ilikuwa miaka 8 yaani std 1 to std 8
Baadae iliondolewa std 8 ikabakia std 1 to std 7
Sababu ya kuondoa std 8 ilikuwa kuharakisha kijana kwenda secondary, pia kazi alizokuwa anafanya primary school leaver ziliwekwa kwa watu waliomaliza std 12 yaani form four.
Kindergarten haikuwa compulsory miaka hiyo,hivyo ndio kusema primary school ya miaka 9 imerudi.Ila sijui kwanini waongeze muda wa primary wakati dunia inazidi kupunguza muda wa primary.
Mfumo ule ulikuwa wa mwingereza ambao hata Kenya wanatumia.

Ulifanyiwa marekebisho kidogo ili kuendana na mabadiliko lakini ni ule ule.

Tulichofeli sisi na mfumo wetu kuna sababu nyingi tu ikiwemo utekelezaji mbovu wa sera,
Raslimali watu ambayo haitoshi hasa walimu, taaluma sahihi kwa walimu pia ilikuwa changamoto, miundo mbinu duni na kushindwa kuendana na technology.
 
Jambo kubwa tunalotafuta hapa au kuboresha katika elimu yetu nimna muhitimu anavyoweza kujiajili baada yakumaliza elimu yake, au muhitum anaajirika baada yakumaliza elimu yake?.

Kwa mfumo waelimu yetu naomba uniambie form five na six vinamsaidia vipi mwanafunz katika maisha yakawaida.Zaman shule kama mazengo mtu alikua aliingia form three anaachana na baadhi yamasomo ambayo ktk career yake hayatakua namsaida.
Lengo la secondary education siyo kuzalisha wachuuzi na mafundi michundo kama unavyotaka kupropose hapo juu.

Elimu ya form six ni kupanua ufahamu na kuweka msingi wa elimu ya juu.

Tertiary education ndiyo kuzalisha sasa hao mafundi michundo.

Elimu ya degree duniani kote lengo kuu ni kutengeneza watu wenye uwezo wa kufikiri ndiyo maana wanatoka universities mara nyingi wanafanya managerial activities popote.

Suala la kukazia ni relevancy ya mitaala yetu katika mazingira ya sasa.

Tunajikita kwenye kutazama quality bila kukuuliza relevancy ya kinachofundishwa kinafit kwenye mazingira tuliyonayo ?
 
Chadema ni wababaishaji tu, kila mtu akisimama jukwaani utasikia, "Risasi 16" mara risasi 64 bado zingine zimo kiunoni, yaani maajabu tu. Jana mke wa mgombea wao kasema tena huku anatoatoa vimachozi mambo hayo hayo ili wananchi wamuhurumie!! hakuna kura za huruma hapa, mtu ukae ulaya upangwe na mabeberu kuja nchini kutaka kubaka kura kwa kigezo cha huruma
Kila mmoja anapewa haki ya kutoa mawazo yake na kupata taarifa.
 
Mfumo ule ulikuwa wa mwingereza ambao hata Kenya wanatumia.

Ulifanyiwa marekebisho kidogo ili kuendana na mabadiliko lakini ni ule ule.

Tulichofeli sisi na mfumo wetu kuna sababu nyingi tu ikiwemo utekelezaji mbovu wa sera,
Raslimali watu ambayo haitoshi hasa walimu, taaluma sahihi kwa walimu pia ilikuwa changamoto, miundo mbinu duni na kushindwa kuendana na technology.
Ukweli wakati wa waziri mkuu Lowasa ulitokea mzozo kati ya chama cha wenye shule binafsi na serikali, waliomba ufadhili wa world bank fedha za maboresho ya shule wakati huohuo serikali iliomba fedha kwa ajili ya mradi wa MESS world bank waliomba approval ya serikali kwani haifanyi kazi na jumuia mojamoja inafanyakazi na serikali au mradi ulio idhinishwa na serikali.

Kwa kuwa bwana mkubwa alijiandaa kumrithi swahiba wake aliutupilia mbali mradi wa private school na kuendelea na mradi wa mess kwa jina maarufu sekondari za kata. Ni ngumu sana kuboresha elimu pasipo kushirikisha sekta binafsi, africa ya kusini shule binafsi hupewa ruzuku na serikali ili ada ishuke na watoto wa masikini wapate elimu sawa na watoto wa matajiri, uingereza nssf huwalipia watoto wa wanachama wao ada, sweden ada hulipwa na serikali hata kama usome private ila wenzetu watoto ni wachache kuliko watu wazima, sisi vitoto ni lundo utaboreshaje?

Matatizo ya Elimu Afya na Ajira ni multiplier effects hayana mwisho, kinachofanyika nikuyadhibiti yasizidi uwezo, na serikali peke yake haiwezi,
 
una miaka 4 uko chekechea???? mtu ana miaka 16 ashaanza kupokea mshahara mbele, wengine washasajiliwa mpaka club kubwa! kwan mna kwama wap cdm
acha uongo ....eti kusajiliwa na club kubwa ....kwa hiyo kusajiliwa club kubwa ni zao la mfumo wa elimu moja kwa moja basi ...hayo ni matokea ya Kipaji ....hapo chini ni jedwali linalezea mfumo wa elimu wa marekani na miaka inaonekana . halafu nini kinakusahangaza mtu kuwa chekechea akiwa na miaka minne

There is considerable variability in the exact arrangement of grades, as the following table indicates.

Continuing education
Higher education
Compulsory education
CategorySchool Grade LevelAge
Preschool educationPre-kindergarten3-5
Elementary
school
Kindergarten5-6
1st grade6-7
2nd grade7-8
3rd grade8-9
4th grade9-10
5th grade10-11
Middle
school
6th grade11-12
Junior high
school
7th grade12-13
8th grade13-14
High
school
Freshman/9th grade14-15
Senior high
school
Sophomore/10th grade15-16
Junior/11th grade16-17
Senior/12th grade17-18
College
(University)
Undergraduate
school
First year: "freshman year"18-19
Second year: "sophomore year"19-20
Third year: "junior year"20-21
Fourth year: "senior year"21-22
Graduate school
(with various degrees and curricular partitions thereof)
22 and up
Vocational school18 and u
 
Lengo la secondary education siyo kuzalisha wachuuzi na mafundi michundo kama unavyotaka kupropose hapo juu.

Elimu ya form six ni kupanua ufahamu na kuweka msingi wa elimu ya juu.

Tertiary education ndiyo kuzalisha sasa hao mafundi michundo.

Elimu ya degree duniani kote lengo kuu ni kutengeneza watu wenye uwezo wa kufikiri ndiyo maana wanatoka universities mara nyingi wanafanya managerial activities popote.

Suala la kukazia ni relevancy ya mitaala yetu katika mazingira ya sasa.

Tunajikita kwenye kutazama quality bila kukuuliza relevancy ya kinachofundishwa kinafit kwenye mazingira tuliyonayo ?
Unazungumzia katika uhalisia waelimu namna unavyotakiwa kuwa lakini unasahau hapa tunazungumzia namna yakumsaidia muhitimu aweze kuajilika kwa urahisi au kujiajiri.

Mfano watu wengi wanaojariwa na TANESCO katika kada ya uhandisi niwatu waliopita kwanza diploma wakafanya kazi kisha wakaenda kujiendeleza na degree.

Sasa Mimi naposema practical zaidi nikwasababu nchi yetu kwa sasa inahitaji watendaji zaidi na sio wasimamizi. Ndio graduate wengi katika tasinia ya uhandisi wanalia kukosa kazi kwa sababu vyuo vimewazalisha kuwa wasimamizi badala ya watendaji kazi+wasimamizi.

Nchi yetu ilipofikia kwasasa au makampuni mengi hayana shida nawasimamizi wanashida na watendaji kazi. Kwahio lazima elimu yetu kwa sasa ilenge huko, kwa wale wanaosoma uhandisi kuna wanaosoma bachelor of engineering, bachelor of science in engineering nawatu au makampuni mengi yanaprefer watu waliosoma bachelor of engineering ,kwasababu wao wamejikita atleast 50% practical .

Lazima elimu yetu ijikite katika utendaji kazi halisi Kisha baada yahapo managerial system itafaata. Ndio maana mtu alieoita diploma baada yakumaliza form four akaenda kutafuta ujuzi akaachana na elimu ya form five na six, baada yakuhitimu diploma akafanya kazi kidogo ,Kisha akaomba degree anakuwa naujuzi mkubwa hasa katika managerial na utendaji kuliko aliepitiliza moja kwa moja.

Wahitimu wakada ya uhandisi wengi wanafaham, au wajaribu kufanya sampling yakuwauliza wengi wangetaka mfumo gani wa elimu utumike.
 
Mfumo ule ulikuwa wa mwingereza ambao hata Kenya wanatumia.

Ulifanyiwa marekebisho kidogo ili kuendana na mabadiliko lakini ni ule ule.

Tulichofeli sisi na mfumo wetu kuna sababu nyingi tu ikiwemo utekelezaji mbovu wa sera,
Raslimali watu ambayo haitoshi hasa walimu, taaluma sahihi kwa walimu pia ilikuwa changamoto, miundo mbinu duni na kushindwa kuendana na technology.
Mtu wa kumlaumu hasa alikuwa Viongozi wetu,mimi nikiwa darasa la 7 sote Kenya,Tanzania, Uganda tulikuwa na syllabus mmoja hata mitihani ikifanana,vivyo hivyo O level hadi A level ilikuwa British Syllabus kutokea Cambridge University.
Kilichofanyika watawala wetu wakabadirisha kila kitu hadi leo tumezama.Rudisha Cambridge tuondokane na ujinga.
 
acha uongo ....eti kusajiliwa na club kubwa ....kwa hiyo kusajiliwa club kubwa ni zao la mfumo wa elimu moja kwa moja basi ...hayo ni matokea ya Kipaji ....hapo chini ni jedwali linalezea mfumo wa elimu wa marekani na miaka inaonekana . halafu nini kinakusahangaza mtu kuwa chekechea akiwa na miaka minne

There is considerable variability in the exact arrangement of grades, as the following table indicates.

CategorySchool Grade LevelAge
Compulsory education
Higher education
Continuing education
Preschool educationPre-kindergarten3-5
Elementary
school
Kindergarten5-6
1st grade6-7
2nd grade7-8
3rd grade8-9
4th grade9-10
5th grade10-11
Middle
school
6th grade11-12
Junior high
school
7th grade12-13
8th grade13-14
High
school
Freshman/9th grade14-15
Senior high
school
Sophomore/10th grade15-16
Junior/11th grade16-17
Senior/12th grade17-18
College
(University)
Undergraduate
school
First year: "freshman year"18-19
Second year: "sophomore year"19-20
Third year: "junior year"20-21
Fourth year: "senior year"21-22
Graduate school
(with various degrees and curricular partitions thereof)
22 and up
Vocational school18 and u

skuelewi ata na jedwali lako but mwanafunzi miaka 9 primary , thats a no!!!
 
Mtu wa kumlaumu hasa alikuwa Viongozi wetu,mimi nikiwa darasa la 7 sote Kenya,Tanzania, Uganda tulikuwa na syllabus mmoja hata mitihani ikifanana,vivyo hivyo O level hadi A level ilikuwa British Syllabus kutokea Cambridge University.
Kilichofanyika watawala wetu wakabadirisha kila kitu hadi leo tumezama.Rudisha Cambridge tuondokane na ujinga.
Ipo haja ya shule za private kutumia mitihani ya cambridge, kea sasa nadhani isamilo school mwanza na Moshi international school wanatumia hiyo mitihani waachane na Mambo ya kibabaishaji
 
Ipo haja ya shule za private kutumia mitihani ya cambridge, kea sasa nadhani isamilo school mwanza na Moshi international school wanatumia hiyo mitihani waachane na Mambo ya kibabaishaji
Tungefanya Cambridge kama syllabus mbadala.
Baada ya miaka 10 Tanzania itabadirika kabisa.
 
Back
Top Bottom