Chiku Abwao akipiga JALAMBA Vijijini

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,305
33,924
Mheshimiwa Chiku Abwao amekuwa kwenye Ziara ya kutembelea vijijini kuhamasisha Uhai wa CHADEMA na kuelezea umuhimu wa kuhesabiwa kwenye Sensa inayotarajiwa kufanyika mwaka huu. Kwenye mikutano hiyo Mheshimiwa Ametembelea Migoli kwenye Jimbo la Isimani na Ibofwee Jimbo la Kilolo.
 

Attachments

  • 100_5446.JPG
    100_5446.JPG
    427.3 KB · Views: 1,094
  • Chiku.JPG
    Chiku.JPG
    642.2 KB · Views: 841
Chiku Abwao (Mwenye Kombati Nyeusi) Akikagua ujenzi wa Ofisi ya CHADEMA Kata ya Migoli ambayo inajengwa kwa kujitolea na wanachama wa eneo hilo. Mheshimiwa Abwao alichangia ujenzi wa ofisi hiyo.

attachment.php
 
Dah!migoli ndo ngome ya chadema kwa Iringa vijijini,ni kijiji mji chenye vijana wanaojitambua!wamejitolea kujenga ofisi kubwa sana ya chama bila woga!!CCM wakae mkao wa kula mamluki kama Babu Nzwaga,Alex Ndilwa,lenard Mlongwa ni mamluki wa Lukuvi asiyewasaidia chochote hata ada ya watoto!MIGOLI twende twende msiachwe nyuma
 
Huyo chiku kwenye makalio mmmmh, ngoja nikanywe maji kwanza nimepata kiu ghafla.
 
Well done Chiku, maana umegundua kuwa CCM imekuwa ikizoa kura sana huku vijijini. Mkifanya jitihada kama hizi kwenye vijiji vyote hapa Tanganyika, hakuna wa kuwazuia kutinga ikulu 2015. Kule zenji mngewaachia wenye nchi yao, maana dalili za katiba mpya zinaonyesha kuwa Tanganyika itakuwa nchi huru baada ya katiba mpya kupitishwa.
 
attachment.php

Hapa alikuwa anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Ibofwee (25/05/2012) Kata ya Ilole Wilaya ya Kilolo kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya na Umuhimu wa kuhesabiwa kwenye sensa inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.
 
Big up wana Migoli. Yaani hawa wanakijiji wameonyesha mfano wa kuigwa hata na sisi wana wa mjini. Kwa kweli chama chetu kinatakiwa kiwe na ofisi ambazo ni modern kwa mijini na vijijini.
 
NAENDA KUHAMASISHA KIJIJINI KWETU MDAWI TUJENGE OFISI KUBWA KULIKO HIYO.

big up shemeji zangu.
 
nimeshasema huko nyuma, ikiwa kila mbunge wa chadema atafanya kama huyu mama basi nchi hii itabadilika. Chiku ni jembe la nguvu hasa katika mikoa ya kanda ya kati. hongera sana kamanda chiku abwao kwa kuendeleza harakati ya ukombozi nchi hii.
 
Back
Top Bottom