chezzea kichapo cha skuli eeh

gwenivia

Senior Member
Feb 22, 2014
118
20
tupia kistori kifupi kilichokufanya uchapike skuli kisawasawa
kuna siku nliingia staff nkanywa chai na chapati za tcha wa mathe alinitandika bakora ishirini na tatu mpka wenzangu walinishuku nimemtembelea mchina kwa jins makalio yalivovimba
 
hahaha nakumbuka nilivyokuwa la kwanza wiki tatu toka nianze shule sikuelewa kengele nini kila wakiigonga mimi maswali kibao why inagongwa na watu maalum kwanini isiwe mimi
mwishowe siku ya siku baada ya kuruhusiwa saa tano hiyo
nikachukua kibegi changu hadi kwenye mti wa kengele nikabeba kinyundo cha kugongea nge nge nge nge nge aiseeeeeee baada ya kuona wanafunzi wanatoka madarasani nikaanza mbio kumbuka naishi karibu na shule aiseeee nilikimbizwa na wanafunzi wote baada ya mwalimu mmoja kusema mkamateni hawakunipata hadi home usitake kujua nini kilitokea
 
nakumbuka nilitoroka shule yaani kufka njiani nkakutana na mama oooooh kilichofuata nyumbani ilikuwa ni balaa
 
hahaha nakumbuka nilivyokuwa la kwanza wiki tatu toka nianze shule sikuelewa kengele nini kila wakiigonga mimi maswali kibao why inagongwa na watu maalum kwanini isiwe mimi
mwishowe siku ya siku baada ya kuruhusiwa saa tano hiyo
nikachukua kibegi changu hadi kwenye mti wa kengele nikabeba kinyundo cha kugongea nge nge nge nge nge aiseeeeeee baada ya kuona wanafunzi wanatoka madarasani nikaanza mbio kumbuka naishi karibu na shule aiseeee nilikimbizwa na wanafunzi wote baada ya mwalimu mmoja kusema mkamateni hawakunipata hadi home usitake kujua nini kilitokea

Unaakili wewe, ulicho waza ni logical.
 
nilikamatwa na seconf madter kati ya shamba la mahindi mabichi na nmekoka mota kilicho endelea unajua
 
Kwa bahati nzuri shule yetu ilikua na shamba la miwa....siku ya siku baada ya kutoka shule na ile njaa ya mchana tukapita katika shamba la shule tukiwa kama watu 6 hivi tupate miwa ili safari ya kwenda nyumbani iwe fupi kidogo......tukiwa njiani si tukakamatwa na mwalimu wa zamu....akaturudisha shumbani tukakata miwa mingi zaidi na kurudi tena mpaka shule...akatuambia tule ile miwa mpaka iishe isipokwisha mtajua kwanini nyani akifa miti yote hutereza.......kilicho fuata hapo ilikua ni historia iliyojiandika automatically kichwani mwangu mpaka kesho....!!
 
hahhaha duuhhhh
 
Tulikua wajeuri darasa la saba hadi siku mkuu wa wilaya alipotembelea shuleni alipewa historia yetu akaja darasani na kutafuta kijisababu basi wote tuliokua na nywele ndefu tulitolewa nje ile adhabu tulioipata kamwe siwezi kuisahau unasimama kibarazani kuegemea ukuta kisha unashuka na mgongo kama unakaa chini ukifika katikati kama umekaa kwenye kiti kwa muda wa lisaa limoja ukinyoosha mguu tu fimbo 15 zinakungoja
 
tupia kistori kifupi kilichokufanya uchapike skuli kisawasawa
kuna siku nliingia staff nkanywa chai na chapati za tcha wa mathe alinitandika bakora ishirini na tatu mpka wenzangu walinishuku nimemtembelea mchina kwa jins makalio yalivovimba

nakumbuka siku moja tulifanya mtihani wa historia katika kutoa kugawa mitihani,ulipofika mtihani wangu akasems kwanguvu eti alipomaliza kusahihisha mtihani alikunywa panadol kutokana na mwandiko mbaya wangu ilimbidi apate maimivu ya kichwa
 
cwez sahau 2liandikwa wapiga kelele darasa tukachapwa tangu saa 6 mchana mpaka saa 9 mchana na walimu wote staff yani ilikuwa balaa
 
Nikiwa msingi nilikataa kupitia deli la ice cream za mwalimu, mwalimu aliponiuliza nikamwambia mie nimechoka kubeba kila siku awambie na wengine, nikaitwa staff nikajibu vile vile, nikachapwa kidogo walimu wakaniamuru nilifuate, dadeq! Nikaenda home ckurudi ng'oo, kesho take nikakuta zigo la fimbo linanisubiri, we Nouma xanaaaaa usiombee, nilitandikwa mpaka niliona vinyulinyuli
 
hahaha nakumbuka nilivyokuwa la kwanza wiki tatu toka nianze shule sikuelewa kengele nini kila wakiigonga mimi maswali kibao why inagongwa na watu maalum kwanini isiwe mimi
mwishowe siku ya siku baada ya kuruhusiwa saa tano hiyo
nikachukua kibegi changu hadi kwenye mti wa kengele nikabeba kinyundo cha kugongea nge nge nge nge nge aiseeeeeee baada ya kuona wanafunzi wanatoka madarasani nikaanza mbio kumbuka naishi karibu na shule aiseeee nilikimbizwa na wanafunzi wote baada ya mwalimu mmoja kusema mkamateni hawakunipata hadi home usitake kujua nini kilitokea

Huo ulikuwa Udadisi haswaa...
 
cwez sahau 2liandikwa wapiga kelele darasa tukachapwa tangu saa 6 mchana mpaka saa 9 mchana na walimu wote staff yani ilikuwa balaa
Ebwana eeh! Nilikuwa darasa la tatu...nikiwa kilanja wa darasa wengine wamwita 'monita'...ilikuwa issue hiyo hiyo ya kelele..kuandika wapiga kelele.

Niliwaandika wapiga kelele matata we acha tu....ilikuwa hivi" yapata asubuhi mvua inanyesha...wanafunzi wanapiga kelele kushinda kelele za mvua iliyokuwa inanyesha juuu ya paa (mabati) ya darasa...na darasa letu lilikuwa karibu na ofisi ya Mwalimu mkuu...nilikuwa tayari ninao wapiga kelele saba maarufu kwenye orodha. Karatasi ya majina hayo niliweka kwenye madaftari yangu. Jamaa sijui wajipinduaje walichomoa karatasi ya majina wakongeza jina langu kinyemela na kurudisha karatasi hiyo kwenye daftari langu.

....mara ghafula mwalimu mkuu akaingia darasani...akauliza monita wapi majina ya wapiga kelele...mimi bila hata kuangalia nikachomoa karatasi yenye majina ya wapiga kelele na kumpa...akaaza kusoma majina hayo ...jina la kwangu likawa la mwisho kusomwa,...kwa mshituko nilioupata wala siweza hata kujitetea, nikaweka rekodi ya kuwa monita wa kwanza kutamkwa hadhari kuwa mpiga kelele...mwalimu mkuu wala hakufanya ajizi akaniita mbele.. na kuanza kutushushia fimbo za "mwanzi"... mimi aliniongezea zaidi kipigo huku akisema..."uendelee hivyo kwa kuwa muungwa na mkweli maishani mwako..."
 
sito sahau mara ya kwanza na ya mwisho nikiwadearasa la nne nilichora kiungo cha siri na kuandika jiana lake (u..bo.o) nikamtupia rafiki yangu kile kikaratas (ili aone uhodari wangu ktk fani ya uchoraji) daah jamaa direct kakipeleka kwa mwalimu mbele...Moyo wangu ukaanza kudunda ,ghafla nikaitwa mbele
mwlimu -'akaita jina langu'
mimi -"naam!!" nikaenda mbele
mwalimu- akauliza "hiki nini umechora"
mimi- kimyaaaaa!!
mwalimu -kwa kufoka akauliza "HIKI NINI NAKUULIZA"
MIMI-"nimechora UBAO mwalimu"
mwalimu-"huu ubao...hapa umeandika ubao?"
mimi-nikaanza kulia maana nikajua hizi stiki tuu isitoshe karibu nusu ya darasa zima tumetoka kuchezea sticks kwa sababu ya ya kutokujua tEBO
mwalimu-akauliza baba yako yupo?
mimi-hapana kasafiri
mwalimu -kamuite mama yako
mimi -mama naye hayupo kalazwa ana wiki mbili
mwalimu...akauliza darasa et anachokisema huyu ni kweli?
darasa -zikasikika saut za watu km wa3 hivi hapanaaaaaa
weweeeeeeeee.....MWALIMU-"haya piga magoti anza kuita mvua alafu akaagizwa C/monitor akalete mzigo wa fimbo ofisini"(kilicho endelea sikumbuki maana lile darasa tulikuwa na tabia mbaya mwenzetu akliwa anaadhibiwa bakora watu wanashangilia ) nilichezea stiki za kushindwa kuimba tebo + na zakuchora matus
ila toka siku hiyo hadi leo hii nipo chuo sikuwahi kufanya kosa la kumwita mzazi zaid ya vikao rasmi na ndipo mwalimu yule,mimi na mzaz tukaanza kufahamiana hadi naingia std 5/6 alikuwa mwalimu wangu wa darasa kutokana na kufnya kwangu vizur ktk somo lake nikapewa UClass-monitor na uprefect wa shule..
 
Nakumbuka nikiwa darasa la 5 nilikuwa na kioo kidogo, nikiona msichana kasimama nakitupia chini naendelea kuchek muvi na rafk zangu, cku moja kama kawaida nikakitupia chini kuchek yule dada chupi yake imechanika kitu laiv kinaonekana, c nikawaita rafk nao waone ile kuona wakaanza kucheka na kufanya raia kuongezeka c mhusika akashtuka, akaenda moja kwa moja kwa dingi alikuwa mwalimu, ile kutokeza tu wakanitaja, akaita njemba nne wakaninyanyua juu kwa kunishika mikono na miguu af mshua kashika fimbo za mpera, nakumbuka wiki nzima ckuweza kukaa kwenye koch
 
Ebwana eeh! Nilikuwa darasa la tatu...nikiwa kilanja wa darasa wengine wamwita 'monita'...ilikuwa issue hiyo hiyo ya kelele..kuandika wapiga kelele.

Niliwaandika wapiga kelele matata we acha tu....ilikuwa hivi" yapata asubuhi mvua inanyesha...wanafunzi wanapiga kelele kushinda kelele za mvua iliyokuwa inanyesha juuu ya paa (mabati) ya darasa...na darasa letu lilikuwa karibu na ofisi ya Mwalimu mkuu...nilikuwa tayari ninao wapiga kelele saba maarufu kwenye orodha. Karatasi ya majina hayo niliweka kwenye madaftari yangu. Jamaa sijui wajipinduaje walichomoa karatasi ya majina wakongeza jina langu kinyemela na kurudisha karatasi hiyo kwenye daftari langu.

....mara ghafula mwalimu mkuu akaingia darasani...akauliza monita wapi majina ya wapiga kelele...mimi bila hata kuangalia nikachomoa karatasi yenye majina ya wapiga kelele na kumpa...akaaza kusoma majina hayo ...jina la kwangu likawa la mwisho kusomwa,...kwa mshituko nilioupata wala siweza hata kujitetea, nikaweka rekodi ya kuwa monita wa kwanza kutamkwa hadhari kuwa mpiga kelele...mwalimu mkuu wala hakufanya ajizi akaniita mbele.. na kuanza kutushushia fimbo za "mwanzi"... mimi aliniongezea zaidi kipigo huku akisema..."uendelee hivyo kwa kuwa muungwa na mkweli maishani mwako..."

We jamaa umenifanya nicheke kwa sauti barabaran hadi watu wananishangaa, mi nakumbuka story inayofanana na hiyo wkt niko o level, darasa letu lilikuwa na most stubborn students ever happened in this world, watu walikuwa na kelele hao balaaa bas siku ya siku tumejisahau na kelele zetu za kufa mtu mara vuup secondmaster huyu apa babako si ameshtukiza ghafla akamwambia monitor ampe majina ya wapiga kelele kama kawa monitor akazama kwenye makabrasha yake akatoa kikaratasi akamkabidhi second master nae bila ajiz akaanza kuita, kumbe yule monitor alikuwa na tabia ya kuwaandika wapiga kelele in advance incase akija ticha anamkabidhi majina, basi second si akaanza kuita jina moja baada ya jingine mbaya zaidi majina mawili ya kwanza yalikuwa ya washkaj flan wamepigwa suspension kama siku mbili zilizopita weee! Watu si wakaanza kubisha pale 'sir the list is not current' wengine "sir the list is not up to date' bas second akaamua amtie bakora monitor peke yake,jamaa alichezeshwa stiki nyingi sanaaaa na baada ya tukio hilo kila mtu alikuwa na adabu manake monitor alikuwa na hasira ya kufanya revenge ya fimbo alizokula, tabia ya kelele zisizo na msingi ikawa imekoma kwenye darasa lile, fimbo nomaaa!
 
..... kumbe yule monitor alikuwa na tabia ya kuwaandika wapiga kelele in advance incase akija ticha anamkabidhi majina, basi second si akaanza kuita jina moja baada ya jingine mbaya zaidi majina mawili ya kwanza yalikuwa ya washkaj flan wamepigwa suspension kama siku mbili zilizopita weee! Watu si wakaanza kubisha pale 'sir the list is not current' wengine "sir the list is not up to date' bas second akaamua amtie bakora monitor peke yake,jamaa alichezeshwa stiki nyingi sanaaaa na baada ya tukio hilo kila mtu alikuwa na adabu manake monitor alikuwa na hasira ya kufanya revenge ya fimbo alizokula, tabia ya kelele zisizo na msingi ikawa imekoma kwenye darasa lile, fimbo nomaaa!
Aha ha haa..! Kweli huyo 'monita' kanipiku.
 
Back
Top Bottom