Cheyo: Magufuli ni Rais aliyesubiriwa tangu Tanzania ipate Uhuru

Dom vurugu zake zilikuwa kubwa sana pale 84 club na wapenda ukweli wanasema alikuwaga anapenda kulala na wawili, kivumbi kilikuwa alivyopigwa laptop yake wezi hao wa jinsia ke walitafutwa pasipo mafanikio, ahame chama atafutiwe nafasi, Japo najua hawezi kukubali kuacha uenyekiti Japo haulipi, wanaokaa karibu na magogoni, vip benchi la wageni lipo full kama enzi za mkwere au, maana huyu hataki memo wala madalali
 
Na: Lilian Lundo-Maelezo

Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amesema kuwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni Rais aliyesubiriwa kwa muda mrefu tangu kuanza kwa Uhuru.

Cheyo ameyasema hayo alipokuwa akielezea juu ya utendaji wa Rais Magufuli tangu ameingia madarakani Novemba, 2015.

“Utendaji wa Rais Magufuli umewashtusha watu wengi kwani hawakutegemea kwa muda mfupi aliokuwa madarakani kama angeweza kuchukua hatua kubwa kama vile kupambana na mafisadi, jambo ambalo limekuwa likiongelewa na viongozi waliopita lakini kulikuwa hakuna matunda ya moja kwa moja,” alifafanua Cheyo.

Ameendelea kwa kusema kuwa Rais Magufuli amekuwa na adhima ya kupambana na Mafisadi na kutatua kero za Taifa tangu akiwa kwenye kampeni huku akisimamia kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

Vile vile Cheyo amesema kuwa kero ambazo amekuwa akizitatua Rais Magufuli zikiwemo ufisadi, uchumi tegemezi, mapato madogo na ukosefu wa vifaa mahospitalini ni kero ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na kambi ya upinzani kwa muda mrefu.

Hivyo kuingia kwa Rais Magufuli madarakani kumeleta utatuzi mkubwa kwa kero hizo ambazo zimekosa utatuzi kwa muda mrefu kutokana na viongozi waliopita kutozichukulia uzito mfano Rais Magufuli alivyoweza kutatua tatizo la vitanda hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kipindi kifupi ambapo hivi sasa hakuna mgonjwa anayelala nchini katika hospitali hiyo.

Akielezea suala la ufisadi nchini, Cheyo amesema kuwa ufisadi ni ugonjwa wa muda mrefu ambao umepoteza fedha nyingi za nchi kutokana na mikataba mibovu iliyokuwa ikisainiwa na viongozi wa juu.

Aidha amempongeza Mhe. Rais kwa kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na kuona tatizo hilo lishughulikiwe kisheria na kwa njia maalum ili kukomesha ufisadi nchini.

Cheyo amewataka watanzania kugeuza mawazo yao na kuchukia rushwa kwa kukataa kupokea na kutoa rushwa kwani rushwa ni adui wa haki na inarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Kwa Hisani ya MPEKUZI
Hivi amaanisha nini anaposema tangu kupata UHURU?
 
SAFI SANA CHEYO WEWE NDO MPINZANI UNAESEMA KWELI KWAJILI YA TAIFA SIO WALE WANAODHOFISHA NA KURUDISHA JUHUDI ZA SERIKALI BAADALA YA KUWA PAMOJA NA KUENDELEZA NCHI YETU WANAFIKIRI MAUMIVU YA UCHAGUZI WA MWAKA JANA,WAPINZANI WANAMNA HIYO HAWAFAI NANI MZIGO.MAADUI WA MAENDELEO YA NCHI YETU NI:-1.MARADHI,2.UMASKINI.3.UJINGA 4.UKAWA(UKUTA).
 
Nashangaa, yeye ana chama, anasifia vya wenzake, huyu ana akili kweli. Sawa na Mrema anamkampeinia Magufuli wakati chama chake kilikuwa na mgombea. Huyu ana akili kweli? Njaa za vipi mbona muda wa kuishi umeshafika ukingoni anahangaika na nini kujidhalilisha
Hahaha eti mrema alisema amefanya biashara yenye faida
 
Ukiacha umri kumtupa mkono , lakini tuache masihara Huyu mzee ameugua sana hapo kipindi cha nyuma kidogo .
 
Nashauri huyu mzee apewe ukatibu wa bodi ya parole.
 
Back
Top Bottom