G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Hatimaye yale madai kuwa rasimu ya katiba iliyokuwa ikijadiliwa bungeni ilitoka CCM yameanza kubainika ukweli wake.
Leo saa saba mchana mwenyekiti wa kamati ya uandishi wa rasimu ya katiba mpya Andrew Chenge amebainisha kuwa rasimu mpya ya katiba ilitungwa na CCM kipindi cha uchaguzi wa mabaraza ya katiba.
Aidha Chenge amethibitisha kuwa rasimu hiyo ilisambazwa kwenye mabaraza yote nchini na walitakiwa kutoa maoni yao kwa kufuata muongozo waliopewa, jambo ambalo tume ya Warioba ililibaini na kuyatupilia mbali maoni ya mabaraza hayo ambapo Chenge amesema kuwa taswira ya rasimu ya pili ya Warioba ingekuwa sawa kabisa na taswira ya rasimu ilyopelekwa bungeni na kamati yake kama wangezingatia maoni ya mabaraza hayo ambapo kimsingi yalitoka kamati kuu ya CCM kupitia ndugu Asharoze Migiro na ndugu Evodi Mmanda ambao waliyaratibu.
"Hata hii sisi tuliyotunga muongozo wake tuliupata kutoka CC ya CCM" alisema bwana Chenge.
Chenge aliyasema hayo wakati alipobanwa na baadhi ya waumini waliotoka kwenye ibada ili kujua ukweli wa mambo.
Aidha katika utafiti nilioufanya nimebaini kuwa vigogo wengi wa bunge maalum la katiba ambao waliingia kupitia taasisi mbalimbali ni makada waandamizi na wajumbe wa kamati kuu ya CCM ambao waliiandaa rasimu hii mapema sana na kwa kutumia sayansi ya hali ya juu kisha kuipenyeza kwenye mabaraza ya katiba jambo ambalo liligundulika na Chadema na tume ya Warioba.Pia makada hao wameongoza kamati zote zenye maamuzi juu ya rasimu hiyo.
Aidha Chenge alibaini kuwa kuzomewa kwa Warioba alipowasilisha rasimu bungeni ulikuwa mkakati wa mwanzo wa CCM kuikataa rasimu ya tume yake.
Cha kushangaza ni kuwa Chenge alisema CCM imefanya hivyo kwa nia njema ya kuliokoa taifa!