Chelsea 2-3 Kanu: Siku ambayo Kanu alianza rasmi kudeka klabuni Arsenal

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
IMG_6643.jpeg
ZIKIWA zimesalia dakika 15 tu mchezo kumalizika, huku washabiki wa Arsenal wakiachia viti walivyokuwa wameketi juu yake na kuanza kutafuta ilipo milango ya kutoka nje ya Dimba la Stamford Bridge lililopo magharibi mwa London hatimae anaibuka shujaa asiefikiriwa wala kuimbwa, kisha anawarudisha vitini washika mitutu hao walokuwa wamekatishwa tamaa kwa kuwa tayari walikuwa nyuma kwa magoli 2-0.

Akiwa na miezi isiozidi minne tu tangu asajiliwe klabuni Arsenal, tena kwa usajili ambao haukuwa na baraka za watu wote wa Gunners, eti kwa kuwa Nwankwo Kanu alikuwa amebalaswa huko klabuni kwa wacuta bange Inter Milan alikokuwa, baada ya kukutwa na matatizo kwenye Moyo, hatimae kijana huyu kutoka katika viunga vya Owerri ndani ya jimbo la Imo kusini kabisa mwa Naijeria anatumia muda wa robo saa kusawazisha magoli mawili na kufunga goli la ushindi, na hatimae kuwaacha washabiki wa Chelsea midomo wazi huku wameshika vichwa.

Ilikuwa ni Jumamosi ya tarehe 23 mwezi wa kumi mwaka 1999, ndipo Nwankwo Kanu kijana mreefu na mwenye sifa ya uvivu awapo uwanjani, tena asievaliana Viatu na mchezaji yeyote yule katika kikosi cha the Gunners, kwa kuwa alikuwa anavaa kiatu saizi namba 15 hatimae anavuruga sherehe ya washabiki wa Chelsea ambao tayari walijuwa kazi wameimaliza.

Chelsea wakiwa nyumbani huku wakiwa na moto kwelikweli kwakuwa walitoka kuwashikisha adabu na kuwabamiza magoli 5-0 klabu ya Manchester United katika mchezo uliopita wa ligi, walianza vizuri mchezo na kufanikiwa kupata magoli mawili yaliofungwa kwa njia ya vichwa kutoka kwa Tore Andre Flo na Dan Petrescu.

Ikumbukwe tu magoli haya yalifunngwa mnamo kipindi cha kwanza, na mpaka tunakwenda mapumziko Chelsea walikuwa mbele kwa magoli 2-0.

Ama kwa hakika hii ni moja ya mechi kabambe ya mahasimu wa jiji la London, hivyo pale kati ilikua inaongozwa na mwamuzi mahiri kipindi hicho Alan Wilkie ambae ndani ya dakika 3 tu tangu kuanza kwa Mchezo alimzawadia kadi ya njano mlinzi wa Arsenal Lee Dixon baada ya kumkwatua mchezaji wa Chelsea Graeme Le saux.

Kadi hio ya njano, tena ya mapema hivyo iliwachanganya mno Arsenal, kadhalika kadi hio ilikuwa ni ya 50 kutolewa katika mechi 7 za mwisho walizokutana miamba hawa yaani klabu za Chelsea na Arsenal.

Hali ya hewa nayo ilikuwa ni ya tofauti kwani Mvua kubwa ilinyesha siku hio, na mpira ulikuwa wa ubabe kwa vipindi vyote, huku timu zote zikikosa wapishi wao muhimu kabisa.
Chelsea walimkosa Mtaliano Gianfranco Zola ambae hakukuwa na taarifa za moja kwa moja je kwanini alianzia benchi na upande wa Arsenal ulikosa huduma ya Mholanzi Dennis Bergkamp.

Kipindi cha pili klabu ya Arsenal ilianza vyema na kutawala vilivyo mpira.
Na hapa ndipo matendo makuu ya kimiujiza ya kijana Nwankwo Kanu aliezaliwa mnamo tarehe 1/8/1976 yalipoanza kuonekana.

Kanu sambamba na pikipiki ya kidachi Marc Overmars walianzisha msako langoni mwa Chelsea kiasi kwamba washabiki wa Chelsea walisahau nyimbo zao ghafla na kutulia kwenye viti vyao, Kanu na Overmars waliliandama vilivyo lango la Chelsea.

Msako uliendelea kuwa mkubwa, Msako ulipitia njia kuu mpaka vichochoro vilivyoelekea golini mwa Chelsea.
Arsenal hakika waliliandama lango la Chelsea na kupoteza kabisa mbinu za Chelsea za kuweza kulinda ushindi wao huo wa magoli mawili walioupata mapema tu.

Wakati hayo yakijiri, klabu ya Arsenal ilifanya mabadiliko.
Hii ilikuwa ni mwendo wa dakika za 60 ambapo Mfaransa alieshindwa kung’aa kwenye klabu ya Juventus na hatimae kuja kuwa mfalme wa klabu hio Thiery “TH14 vava vava vooo” Henry aliingia uwanjani.

Hii ilionekana na kuthibitika wazi kuwa Arsenal walikwenda vitani na Kisu, lakini sasa wameongeza silaha imara zaidi, kwa kifupi Arsenal waliongeza kombora la maangamizi.

Hata kufikia hapo ukuta wa Chelsea ukiongozwa na Malcel Desailly ulionekana kumomonyoka.
Kiungo cha Chelsea kilichotawala mcheza kipindi cha kwanza kilipasuka vipande vipande kiasi kwamba hapakuonekana tena Denis Wise akicheza soka lake la undava na rafu za kila Dakika, wala hapakusikika jina la Mfaransa Didie Deschamps aliesifika kipindi cha kwanza kwa kupiga pasi nyoofu zilizofikia walengwa bila kashda ya aina yoyote toka kwa wachezaji wa Arsenal.

Msako ulioanzishwa na Davor Suker, Freddie Ljungberg, Marc Overmars, Nwankwo Kanu na kisha Thiery Henry hatimae ulianza kufanikiwa mnamo dakika ya 75 pale Nwankwo Kanu alipoutumbukiza Mpira kimiani na kuhesabu goli la kwanza.

Mpaka hapo magoli kwenye runinga yalisomeka Chelsea 2-1 Arsenal.

Wakati washabiki wa Arsenal waliokuwa wamekata tamaa na kuanza kuondoka uwanjani wakijuwa kuwa wameshakubali kibano toka kwa watani zao wa jiji la London, hatimae wakaanza kugombea kurudi uwanjani kwa kuwa waliamini sasa lolote laweza kutokea.
Viti vikajaa tena.

Washabiki wa Arsenal wakarejea uwanjani na mpaka zikiwa zimesalia dakika 10 mchezo kumalizika klabu ya Arsenal ilitawala mechi kuanzia uwanjani mpaka jukwaani huku washabiki wao wakiwa wanaimba nyimbo za kuwapa mioyo wachezaji wao.

Chelsea walipoteana kabisa na walicheza mpira ambao ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa ndio waliofundishwa.
Celestine Babayaro akawa uchochoro, kadhalika Graeme Le Soux pia.
Kipa Edy de Goey aliokoa michomo mingi na kuonekana mara kwa mara akiwafokea mabeki zake mpaka ilifika muda ikamladhimu tu anyamaze na kuomba mpira uishe.

Kwa kifupi si Petrescu wala Leboeuf aliemuona mwenzie.
Hata Gustavo Poyet pia hakuwa na nguvu tena ya kupiga majalo ambayo yangemfikia Tore Andre Flo ambae angepiga kichwa na kufunga kama alivyofanya kipindi cha kwanza.

Usiku wa deni hauchelewi na ilipojiri dakika ya 83 Nwankwo Kanu tena akapachika nyavuni goli la pili na kufanya mchezo kuwa sare.

Hakukuwa na la ziada tena kwa wachezaji na washabiki wa Chelsea, zaidi tu ya kuomba mpira umalizike na waambulie japo tu hio suluhu na kapointi kamoja.
Hakuna alieamini kiwango cha kipindi cha pili walicho anza nacho Chelsea.

Ikumbukwe tu kabla ya Mechi hio, Chelsea walitoka kumenyana na Manchester United ambapo Chelsea waliibuka na ushindi wa magoli 5-0 Magoli ambayo aliyapokea mlinda mlango mpya klabuni Manchester kwa wakati huo Masimo Taibi.

Wanasema usikate tamaa kabla hujafa, kauli hio ilidhihirishwa na Nwankwo Kanu, kwani mnapo dakika 90 raia huyu wa Naijeria alifanikiwa kutumbukiza kimiani kamba ya 3 kamba iliowalegeza wachezaji wa Chelsea, kisha ikawatepetesha washabiki wa Chelsea na hatimae ikawawehusha wachezaji na washabiki wa Arsenal ambao waliamka upya na ari ya furaha isio elezeka.

Mpaka refa alipoitumbukiza filimbi kinywani na kumaliza mchezo, Chelsea wakawa wamepoteza mchezo kwa kuwa walishindwa kuyalinda magoli yao mawili walio yapata kipindi cha kwanza cha mchezo.

Chelsea ilishindwa linda ushindi huo zikiwa zimesalia dakika 15 tu ili mchezo umalizike.
Ilikuwa ngumu saana kwa washabiki wa ukweli wa Chelsea kukisamehe kikosi chao hicho kwa kile walichokiita “uzezeta ulio pevuka”.

Hadi mwisho wa Mchezo Chelsea 2-3 Kanu/Arsenal.

Tangu siku hio, mchezaji Nwankwo Kanu aliheshimika na kuhusudiwa vilivyo klabuni hapo. Kanu alideka. Kanu hakukaba tena wala kuhimizwa kufanya juhudi uwanjani. Kanu hakuwa tena mchezaji wa kukimbia huku na kule awapo uwanjani, bali kwa sasa Kanu alikuwa anazurura tu uwanjani huku akisoma mabango ya washabiki yenye jumbe za kila aina zinazo msifu na kumthamini.

Kwa kifupi Kanu alimaliza jukumu lake klabuni hapo, na kilicho endelea ni klabu ya Arsenal kulipa fadhila kwa Muafrika huyo.

Katika mchezo huo Chelsea iliwaanzisha: De Goey, Alberto Ferrer, Malcel Desailly, Frank Leboeuf, Celestine Babayaro, Dani Petrescu, Denis Wise, Didie Deschamps, Graeme Le Saux, Chris Sutton, na Tore Andre Flo.

Huku wachezaji wa akiba wakiwa: Hogh, Gustavo Poyet, Jorde Morris, Kipa Carlo Cudicini na Gianflanco Zola.

Wakati Arsenal walianza na: David Seaman, Lee Dixon, Martin Keown, Mkoba na nahodha Tony Adams, Silvio Silvinho, Ray Parlour, Freddie Ljungberg, Emanuel Petit, Mark Overmars, MOTM Nwankwo Kanu na Davor Suker.

Na kwenye dawati la wachezaji wa akiba walikuwapo: Nelson Vivas, Kipa Alex Manninger, Thiery Henry, Mathew Upson, na bwana mdogo Vernazza.
 
Amna kitu matakataka ninyi, arse8 ni lazima achezee kipigo hapo next week.
Pumbavu kabisa.
 
Tony Adams au Mr Arsenal ndiyo alikuwa na kitambaa cha Ukaptain kabla hajamwachia Super Pat. (Patrick Viera)
 
Pongezzi na Sifa kwa muandishi ,Big Up, Mwamba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom