Channel Ten na Lusekelo watakeni Radhi Wahehe

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,596
1,071

Nimekasirishwa na kutiwa kichefuchefu na ushuhuda wa Bw. Lusekelo (a.k.a Mzee wa Upako) alipowahubiria wasikilizaji kupitia kipindi chake cha Channnel Ten wakati wa X-mass wiki hii. Disgusting!

Eti alipokwa akiishi Mbalamaziwa Iringa alikuwa akimwona mzee wa Kihehe akibadilisha kuku wawili kupata mzoga wa mbwa aliyegogwa na gari ili akamle. Na kuwajumuisha wahehe kama ndio jadi yao.

Amelizalilisha kabila hili shujaa linaloheshimika Tanzania, atafakari maneno yake na kuwataka radhi Wahehe.

Pia TV iliyorusha kipindi yapaswa kuwataka Wahehe na Wasikilizaji radhi. Si vyema kurusha kila ujinga unaosemwa na wateja.

TCRA na MCT - Tume ya maadili ya vyombo vya habari waadabisheni hawa.
 

Attachments

  • Hehe2.png
    Hehe2.png
    10.1 KB · Views: 1,342
  • Hehe.jpg
    Hehe.jpg
    10.5 KB · Views: 1,358
Tatizo lipo wapi? Yeye si ameeleza ukweli? Ndio nyinyi kama serikali ya Tanzania na Mapunk ya Mwanza!
 
Haijawahi kuwa mila ya wahehe kula mbwa...isipokuwa wahehe maharage ni dogi hili jina ndo watu walikuja kutafsiri kuwa wahehe wanakula mbwa....hakuna sehemu hata moja ambapo wanakula mbwa labda iwe tabia ya mtu mmoja mmoja.....kama ni watani wamesema hivyo haina shida ila kama siyo watani kwa kweli watutake radhi
 
Mzee wa upako amekulia iringa ata lugha yao anaijua vizuri
.tatizo lenu watanzania hampendi kuambiwa ukweli.
 
Haijawahi kuwa mila ya wahehe kula mbwa...isipokuwa wahehe maharage ni dogi hili jina ndo watu walikuja kutafsiri kuwa wahehe wanakula mbwa....hakuna sehemu hata moja ambapo wanakula mbwa labda iwe tabia ya mtu mmoja mmoja.....kama ni watani wamesema hivyo haina shida ila kama siyo watani kwa kweli watutake radhi
 
wahehe wengine wanaweza kuona wamepewa sifa kwa kupenda kitoweo chao cha asili, wewe unaona umezalilishwa! Kazi kweli kweili!
 
Mzee wa upako na wahehe si watani?

Tatizo ni ujumbe gani unapeleka kwa watoto na jamii isiyojua huo utani, kwamba Wehehe na Watanzania wanakula mizoga ya mbwa.

Utani unaweza kuwa backwardness nyingine mbele ya ustaarabu. Hapa Ujerumani sijaona Wahehe na Wamatumbi wakiwatania Wajerumani kwa kuwa walipigana vita. Patachimbika!

Utani ulikufa na waliopigana vita vya makabila. Kamumwagie maji mtani msibani kama hutaondoka bila meno
 
Wahehe si mila yao kula mbwa,haijawahi kutokea...japo watani wa wahehe uwahusisha wahehe na ulaji wa mbwa,Mtani wa mhehe ni Mngoni na Mmanda si Mnyakyusa,Lusekelo achunge matamshi yake.
Wahehe chakula chao kikubwa ni ugali wa kiwerege,nyama na matofu(viazi mviringo),kinywaji chao ni ulanzi na komoni...haikuwahi kutokea mhehe kufuga mbwa kama kitoweo.
Mbwa hufugwa kama mlinzi na msaidizi machungoni,wahehe wana miiko ktk vyakula(lusilo) kulingana na ukoo,wapo wasiokula kanga(ndege),bandama,nyopolwa(ndama),moyo wa ng`ombe,firigisi n.k n.k!!
Ktk maisha yao ya kijamii wahehe huwatenga watoto wa kike na wa kiume,baba hukaa mbali na watoto wa kike,haikutokea watoto kujua au kuchangia choo na baba,wala watoto walikuwa hawajui kama baba huenda chooni,baba akijisikia haja,hubeba kajembe kake na kupiga mruzi kuita mbwa wake na kutokomea porini...hali hii iliwafanya watoto waamini wakubwa hasa baba haendagi chooni wala kujisikia ”kupumua”,ndio maana wahehe wana msemo wanasema ”mvina siafula= mkubwa hajambi(asha kumu si matusi“
Kwa asili wahehe hawataili,si mila yao kwenda jando,baadae baada ya muingiliano na wamisionari ndio wakaanza kutahiri,huoa mitala,ni fahari kuwa na wake zaidi ya mmoja.Ni wakulima wazuri ktk kipindi chote cha mwaka...nyakati za kiangazi hulima ktk ”finyungu“ mazao ya mbogamboga.Wameathiriwa na dini ya kikristo ktk dhehebu la Katoliki,na hasa baada ya ujio wa wamisionari wa Benedictin ktk maeneo ya Tosamaganga,na baadae ujio wa wamusionari wa Consolata.Uislamu kwa asili upo ktk eneo Kalenga na Pawaga, na maeneo ya Pawaga lilifikiwa na Waarabu kutokana na uwindaji wa Pembe za Ndovu kandokando ya iliyokuja baadae kuwa mbuga ya Ruaha...si ajabu wahehe waislamu wengi hutoka maeneo haya.
Eneo la Uhehe ndio liliokuwa tishio kivita,liliwatisha wavamizi wa kigeni na wenyeji..'uzuri wa jeshi la kihehe analijua kiongozi wa wasangu na wabena,kutoka nje adhabu aliyoipata Jemedari wa kijerumani Zelewisky kwa kuuwawa na askari wa kihehe imebaki mpaka kesho ktk vitabu vya historia vya Wajerumani.
Wanawake wa kihehe ni wachapakazi,wachamungu na waadilifu sana,wameumbwa na utii na hofu kwa wanaume,sio wahuni lkn wana huruma kila waombwapo...wao huamini ktk hofu ya Mungu,ndio mana ukiwaomba watakujibu ”vee niangusage elaa ulyee,isambi sa kwako“....yaani we niangushage ule,zambi za kwako.Ni wachapkazi ndio maana wadada wengi wa ndani hutoka Iringa.Tatizo lao ni hasira,wana hasira sana...ukimuuzi hataki tabu,anakuachia dunia kwa kujinyonga ili wewe uishi kwa amani.
Wana uwezo wa kuongoza lkn si hawana spirit ya ”ubepari“,i.e aggressive in investment,lkn wakipata mtu wa kuwaongoza ni wasimamiaji na watekelezaji wazuri sana ktk uwekezaji.
Tatizo lao ni pombe,kukuta muhehe hanywi ni nadra sana,kukuta hana hasira ni nadra,lkn wanajua kupenda na kumjali mwanamke.
Mzee wa Upako awaombe radhi wahehe,wahehe hawali mzoga...wala hawali mbwa,sbb wahehe watani wao ni Wamanda na Wangoni,basi huyu Mnyakyusa Mzee wa Upako aliyekulia mitaa ya Ilala Iringa inabidi aombe radhi,mana ujanja wote kaupatia Iringa,mana hata kwao Mbeya hakujui.
 
Wahehe si mila yao kula mbwa,haijawahi kutokea...japo watani wa wahehe uwahusisha wahehe na ulaji wa mbwa,Mtani wa mhehe ni Mngoni na Mmanda si Mnyakyusa,Lusekelo achunge matamshi yake...... adhabu aliyoipata Jemedari wa kijerumani Zelewisky kwa kuuwawa na askari wa kihehe imebaki mpaka kesho ktk vitabu vya historia vya Wajerumani.
.

Umekuwa Mwalimu wetu Mzuri. ila la jinsia naliweka shakani

Wangekuwepo hapo Ubungo wangemwambia Lusikelo Swela.. yaani ---Ipendeze isipendeze ......
 
Kuna mzee mhehe alikuwa (jina nalihifadhi) alikuwa anaishi Mselesele kijiji cha Masimbwe kule Ludewa alikuwa anawatafuna mbwa sijapata kuona.
Unajua alikuwa anafanyaje? Anamchukua mbwa, anatafuta gunzi la mahindi kisha analichomeka kwenye *148*01# ya mbwa.
Kwa maelezo yake alikuwa anasema akichomeka huko kwenye namba ya maajabu basi yule mbwa anaumka maradufu na na nyama yake inakuwa nzuri hujapata kuona na kama wewe ni mgeni akikupa hiyo nyama, hakika hiyo siku ustaarabu utauweka pembeni kwa jinsi utakavyojilamba vidole mithili ya mtoto wa darasa la kwanza kwa huku ukianzia kidogo mpaka gumba tena kwa kurudia rudia.
 
Kuna mzee mhehe alikuwa (jina nalihifadhi) alikuwa anaishi Mselesele kijiji cha Masimbwe kule Ludewa.
Unaambiwa mzee alikuwa anawatafuna mbwa sijapata kuona.
Unajua alikuwa anafanyaje? Anamchukua mbwa, anatafuta gunzi la mahindi kisha analichomeka kwenye *148*01# ya mbwa.
Kwa maelezo yake alikuwa anasema akichomeka huko kwenye namba ya maajabu basi yule mbwa anaumka maradufu na na nyama yake inakuwa nzuri hujapata kuona na kama wewe ni mgeni akikupa hiyo nyama, hakika hiyo siku ustaarabu utauweka pembeni kwa jinsi utakavyojilamba vidole mithili ya mtoto wa darasa la kwanza kwa huku ukianzia kidogo mpaka gumba tena kwa kurudia rudia.
 
Nina Uhakika Naninacho Kiandika Ckwasababu Mm Ni Muhehe Tu Ila Kauliiyo Niyaudhalilishaji Hatakama Wapowatu Wanaokula Mbwa Lakin Cio Mizoga Labda Tuchunguze Majirani Zetu Wanyakyusa?
 
Kuna mzee mhehe alikuwa (jina nalihifadhi) alikuwa anaishi Mselesele kijiji cha Masimbwe kule Ludewa.
Unaambiwa mzee alikuwa anawatafuna mbwa sijapata kuona.
Unajua alikuwa anafanyaje? Anamchukua mbwa, anatafuta gunzi la mahindi kisha analichomeka kwenye *148*01# ya mbwa..

Kama ni kuchafuia hali ya hewa ,, ni hapa.. Janga la Div 5
 
Back
Top Bottom