Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,640
- 697,994
Jamii forums imetoa uhuru wa kutumia utambulisho bandia kwa akili ya kulinda maslahi binafsi ya mwanachama.. Lakini kupewa huo uhuru haina maana uwatweze wengine kwa vile tu hujulikani utambulisho wako halisi
Ndani ya huu mtandao kuna mwanachama wa aina mbili au tatu
1. Wanaotumia utambulisho halisi
2. Wanaotumia utambulisho bandia
3. Wanaotumia utambulisho halisi na bandia
Watu wanakutana hapa hawafahamiani lakini kutokana na mahitaji ya kimaisha na maslahi ya kila mmoja ama ya upande mmoja watu hufikia hatua ya kufahamiana zaidi nje ya huu mtandao
Kuna wajinga wachache wenye uono kimo cha mbilikimo wanaodhani kwa kutumia utambulisho bandia basi wanaweza kufanya lolote na wasijulikane popote bila kujua ya kwamba maandishi hayafitiki.. Ni kupitia maandishi yako ya jana ama hitaji lako la mbeleni unaweza kujifunua na kubaki uchi kabisa
Heshimu sana maandiko ya wengine hasa wale ambao unaishia kuwaona jukwaani lakini hamjawahi hata kuonana.. Hata kama maandiko yake hukubaliani nayo kosoa kwa adabu kosoa kwa heshima..Kosoa kwa hoja jadilifu na si vioja, kashfa, dharau au kejeli!
Heshima muda wake aliotumia kuandika hiyo mada, kifurushi chake, ujumbe na maudhui yake..! Si lazima ukubaliane naye.. Hivyo mpinge kwa hoja zenye mantiki ama mpotezee.. Sometimes kuna kipengele cha kukubaliana kutokubaliana na kinyume chake!
Ukiona mada imeruhusiwa kuwa hewani na kupata wachangiaji... Iheshimu sana kwa maana ina kibali cha kanuni na sheria za jukwaa! Kwa maana ya kwamba imekidhi vigezo vyote vya kuruhusiwa kuwepo hai.. Watu wanaweka mada na hazichukui round zinaliwa kichwa na kutupwa jalalani..
Mada inayoachwa hewani iheshimu sana kulingana na jukwaa lake husika..kitendo cha kuiita ya kipuuzi ama ya kipumbavu si kwamba umemtusi na kumkejeli mtoa mada tu, bali hata wachangiaji wengine na hata walioiruhusu iwepo hewani
Unapokuwa mwanachama mgeni (sio multiple ID) Unakuwa mkweli sana.. Unaongea maisha yako unajitambulisha uhalisia wako na kuomba ushauri hapa na pale. Unapokuwa mzoefu unaanza kuvimba kichwa na kujisahau wewe ni nani uko wapi na unafanya nini.. Unasahau hata background yako na kudhani hujulikani..
Usiwe ndezi kiasi Hicho una background that can be traced to the maximum... Maandishi yako mwenyewe ya awali yanaweza kuwaongoza watu mpaka ulipo na wakakufikia bila shida na wakakufanya chochote watakacho hasa kama hawana hofu na Mungu aliye hai
Kikubwa unapotumia utambulisho bandia usidhani ndio umeyawezea maisha.. Kumbuka bado unaishi na shida hazikomi.. Lakini pia kumbuka una background ambayo kwa namna iwayo yote huwezi kuifuta na watu wanayo mkononi..
Ni hayo tuu