Chama kipya cha nguvu ya umma kuanzishwa.

richone

Senior Member
Apr 3, 2012
146
35
Taarifa nilizozipata ni kuanzishwa kwa chama kipya cha nguvu ya Umma ambapo inasadikika viongozi wake ni mbunge aliyetimuliwa kutoka NCCR mh. kafulila. maana ya kukiita nguvu ya umma ni kwasababu ya kutaka kuuteka ama kuwachanganya wanachadema kwani hii ni kauli mbiu ya chadema
 
mbona mnawafanya wananchi ni mbumbumbu kihivyo?hivi unadhani watu wanashindwa kutofautisha chadema na chama kingine?
 
Mtu mzima adanganyiki mpaka aamue mwenyewe adanganyike.Vyovyote itakavyokuwa chadema itabaki kuwa chadema.Achanganywi mtu hapa labda watoto tu.
 
Taarifa nilizozipata ni kuanzishwa kwa chama kipya cha nguvu ya Umma ambapo inasadikika viongozi wake ni mbunge aliyetimuliwa kutoka NCCR mh. kafulila. maana ya kukiita nguvu ya umma ni kwasababu ya kutaka kuuteka ama kuwachanganya wanachadema kwani hii ni kauli mbiu ya chadema

Kafulila arudi tu CDM. Bado anaweza siasa. Ni umri tu unamsumbua.
 
Huu utitiri wa vyama usiokuwa na msaada kwetu ni wa nini badala ya hawa viongozi kuamua kutusaidia kukabiliana na mfumuko wa bei badala yake wanafikiria kuanzisha vyama ambavyo vinanufaika na ruzuku zinazotokana na kodi zetu na kuzidi kutunyonya
 
Kafulila kwa sasa hujawa na nguvu ya kusimama mwenyewe ukapeleka mambo nikupe ushauri wa bure we rudi Chadema ukuze kipaji chako. Angalizo kuwa makini na siasa utafutika na utasahulika ebu rudi kundini, fuata upepo.
 
Hivi huyu kafulila si alishapewa jina na waliokuwa viongozi wake kuwa ni sisimizi
 
Back
Top Bottom