Chama cha madaktari (MAT) hakina uwezo wa kisheria kuitisha migomo

Hawa Madaktari ni wanyama mmetaka mganga mkuu na katibu mkuu wa wizara waondolewe serikali imefanya hivyo. Saizi mnapa tena amri rais nyie kweli makanjanja wala hamna huruma na binadamu wenzenu.

Tusiangalie upande 1 2 pia tunatakiwa tuheshim madai yao na makubaliano yaliokua yamefikiwa na pinda na madactary hao.kuanzia waziri mpaka mganga mkuu walitakiwa kuondolewa tangu mwanzo pinda aliwafukuza hawa walio ndan ya uwezo wake.na akasema wazir na naibu wake hawa mpaka rais mwenyewe kwakua wako nje ya uwezo wake.madactar walikubali lakn pia walipeana muda wakutimiza hayo.ule muda umepita bila serikali kutekeleza hata 1 chaajabu hata wale waliofukuzwa wapo kazini.hilo kosa lamadactary lilo wapi?na kama kiongoz ameshindwa kusimamia wizara yake vizuri ipo haja gani ya serikali kumkumbatia?au inamaana hatuna wat wengine wenye uwezo wakusimamia wizarahiyo?tusitumie tumbo kufikiri
 
Umeshndwa kupanua mawazo yako kidogo tu, hujaangalia demands za madaktari kiumakini umelalia kwao na kuibeba serikali, moja ya madai ya madaktari ni kuboreshewa vifaa ili waweze kuwahudumia ipasavyo wagonjwa!
 
Kuwepo au kutokuwepo kwa MATI haibatilishi madai yao. MAT ni maandishi tu na waliogoma ni binadam(drs.) Jamani propganda hazisaidii tatueni zengwe hilo kwanza
 
Madaktari bingwa wananufaika zaidi na mgomo huu. Zahanati zao na hospitali zao zinatengeneza pesa kwelikweli kipindi hiki. Nilipita Tumaini na TMJ jana kulikuwa kumependeza sana. Sisi wengine tuendelee tu kushabikia hali hii kama mazuzu! Mgomo ungekuwa ni kwa MASLAHI ya NCHI hakuna DAKTARI hata mmoja angeenda kazini hata wale wa hospitali binafsi.
Tumia akili kidogo tu kufikiri kabla ya kuchangia thread...maDaktari waliogoma ni wa taasisi za serikali, unajua lakini hata kwa juu juu tu madai yao? 1. Maslahi bora, 2. Kuboreshwa kwa mazingira ya kazi pamoja na vitendea kazi ili kuweza kutoa huduma bora.

Kwa akili ya haraka haraka...unaona daktari anayefanya kazi private (TMJ, Aga Khan, Hindu Mandal, Tumaini etc..) ana madai kama hayo? kama huko anakofanya kazi analipwa maslahi bora anayoridhika nayo agome ili iweje? Kama huko anakofanya kazi kuna mazingira bora ya kazi, ana vitendea kazi muhimu vya kumuwezesha kutoa huduma bora agome ili iweje?

Uashaona daktari wa hospitali hizo amebong'oa au kachuchumaa anamuhudumia mgonjwa aliyelala kwenye sakafu? Ushamuona daktari wa hospitali hizo anatoa hela yake mfukoni kumsaidia mgonjwa kununua dawa fulani au kifaa fulani cha matibabu kwa sababu tu vimeisha hospitalini na mgonjwa hana hela ya kununulia?
 
Kama ungekuwa unajua unachokiongea...hayo uliyoandika hapo juu ungeupeleka kwa msajili...sio JF!
Kwani wewe ndio mwenye kumiliki JF?JF iko free kwa kila mtu mwenye mawazo yakoe mradi hatukani mtu.
 
TAZARA nao wamegoma. Wanataka Omar Nundu ajiuzulu. Nadhani watafuata Walimu, watataka Dr Shukuru Kawambwa ajiuzulu. Watakuja Polisi na askari Magereza, Mh Shamsi Nahodha aondoke. Wanajeshi nao watatafakari. Watakumbuka yale mabomu. Watagoma, Mh Hussein Mwinyi aondoke. Haya mambo ni sawa na kula nyama ya mtu.
Baadaye nitakuja mimi na Watanzania wenzangu kuingia barabarani kupinga Tume ya Taifa ya uchaguzi kumtangaza mtu aliye shindwa aongoze nchi, na mbaya zaidi nchi inamshinda kila kukicha.
 
Haya tumekuelewa ila sisi tunaliendeleza libeneke..peleke hii habari kwa Pinda anaonekana ajaifahamu vyema.
 
Lots of people are well misinformed! Vichwa vya habari gazeti la Uhuru na habari Leo ni aibu
 
Umenena vema, maana umeainisha sekta zenye matatizo zaidi. Na kumbuka hukukaa uka-google ili kupata hiyo info, ni self-evident. Sijui kama ulikusudia ama la kusema ulichosema, but your internal self admits to this fact. So what does this tell us? YOU HAVE UNCONSCIOUSLY ADMITTED TO THE FAILURE OF THE ENTIRE GOVERNMENT! Thank you very much!
Malaika wa kuziongoza wizara hizi wako wapi? Tunakoelekea agenda halisi za madai haya zitajulikana tu. Ninazo mbili lakini ngoja nisubiri hatua za Pinda leo.
 
Haya nyie semeni hawana uwezo. Mbona wameongoza mgomo na wanagoma, sasa hapo utasemaje hawana uwezo?

Jueni kuwa serikali haina uwezo wa kuuzima mgomo huu kwa porojo isipokuwa imewaondoa Mponda na Nkya.
Mtaimalize Serikali yote. Jana nao TAZARA wanamtaka Nundu aondoke. Ngereja alishatakiwa aondoke , Mwinyi alishatakiwa aondoke na Mabomu ya Mbagala,Pinda kwa ajili ya posho za wabunge, na bado
 
Nilipoteza ndugu katika mgomo wa kwanza sitaki kusikia habari ya kugoma kwa njia hii ya kuweka rehani uhai wa binadamu.
 
Chama cha madaktari (mat) hakina uwezo wa kisheria kuitisha migomo

..."To promote the medical and allied sciences, to maintain the honour and interests of the medical professions and to uphold a high standard of medical ethics and conduct among its members. To act as representative body of the medical profession in Tanzania and to liaise with and advise the Government on health and medical matters. To ensure, maintain and safeguard the interests privileges and welfare of itsmembers....
Soma vizuri uelewe malengo ya hicho chama cha hiyari.
 
chama cha madaktari tanzania ni chama cha hiyari na si chama cha wafanyakazi ambacho kina uwezo wa kuitisha migomo. Kwa mujibu wa masharti ya usajili wa tma, hakuna kipengele kinachotoa mamlaka kwa mat kuitisha migomo. Kitendo cha kuitisha migomo ni sababu tosha kwa msajili wa vyama vya hiyari kukifuta chama hiki ambacho kinaenda nje ya majukumu yake kisheria. .......
hatua zinazostahili kuchukuliwa:

  1. msajili wa vyama vya hiyari afanye kazi yake na arejee usajili mat ili ajiridhishe kama mat bado inastahili usajili kama chama cha hiyari;
  2. kila daktari ana mkataba binafsi wa kazi. Asiyehudhuria kazini asilipwe mshahara mwisho wa mwezi huu. Kuhudhuria kazini sio kusani kitabu cha mahdhurio na kuondoka;
  3. mwanasheria mkuu wa serikali akaombe tamko la mahakama ya kazi kuwa mat hawana mamlaka kuitisha migomo na pia madaktari wanaotoa essential services wana utaratibu wa kugoma ambao haukufuatwa.
  4. madaktari kutoka nchi za nje wanaotaka kufanya kazi tanzania wakaribishwe na wapewe vibali vya kufanya kazi;
  5. hatua za kisheria zichukuliwe dhidi wa wafanyakazi wanaotoa huduma maalum (essential services) wanaogoma kinyume na sheria.

..........
Jamani, tuna tatizo la msingi katika hili. Na sidhani kama tatizo hilo la msingi ni MAT na usajili wake. Tuache haya masuala ya kutafuta mchawi, tutatue tatizo ili tusonge mbele
 
Madakatari walio katika mgomo wanahakikisha ndugu, rafiki na jamaa zao wanapata huduma za afya kipindi cha mgomo. Hivyo, madaktari si miongoni mwa waathirika wa mgomo ndio maana wanakosa huruma kwa wagonjwa ambao hawana hatia kwenye maslahi yao.
 
Hawa Madaktari ni wanyama mmetaka mganga mkuu na katibu mkuu wa wizara waondolewe serikali imefanya hivyo. Saizi mnapa tena amri rais nyie kweli makanjanja wala hamna huruma na binadamu wenzenu.
Kwanini usiwashauri ndugu zako au wewe mwenyewe ukasomee udaktari ili usaidie watanzania? Watanzania mnalalamika sana bila kutoa majibu.
 
Tumia akili kidogo tu kufikiri kabla ya kuchangia thread...maDaktari waliogoma ni wa taasisi za serikali, unajua lakini hata kwa juu juu tu madai yao? 1. Maslahi bora, 2. Kuboreshwa kwa mazingira ya kazi pamoja na vitendea kazi ili kuweza kutoa huduma bora.

Kwa akili ya haraka haraka...unaona daktari anayefanya kazi private (TMJ, Aga Khan, Hindu Mandal, Tumaini etc..) ana madai kama hayo? kama huko anakofanya kazi analipwa maslahi bora anayoridhika nayo agome ili iweje? Kama huko anakofanya kazi kuna mazingira bora ya kazi, ana vitendea kazi muhimu vya kumuwezesha kutoa huduma bora agome ili iweje?

Uashaona daktari wa hospitali hizo amebong'oa au kachuchumaa anamuhudumia mgonjwa aliyelala kwenye sakafu? Ushamuona daktari wa hospitali hizo anatoa hela yake mfukoni kumsaidia mgonjwa kununua dawa fulani au kifaa fulani cha matibabu kwa sababu tu vimeisha hospitalini na mgonjwa hana hela ya kununulia?
Hali ikoje na kwenye sekta nyingine za huduma NCHI hii? Chukulia mfano wa shule za msingi na sekondari za serikali uzilinganishe na za watu na taasisi binafsi. Madaktari wa hospitali za UMMA wakigoma peke yao bila kupata uungwaji mkono na wale wa TAASISI binafsi ambao wengi wao ni walewale tunaowaona Muhimbili na kwingineko inakupa picha gani?
 
Back
Top Bottom