Chakula cha Taifa letu ni kipi?

JS

JF-Expert Member
Sep 29, 2009
2,064
499
WanaJF za masiku??

Nimekuwa nikitafakari suala hili nikajikuta nakosa majibu sawa.

Hivi chakula cha taifa letu (national food) ni kipi? kwa mfano kwa Uganda ni matooke i.e. ndizi za matoke zilizopondwa kama ugali zinaliwa na mboga yoyote. na kama ni mgeni ni lazima uonje angalau kijiko kimoja

sasa kwa tanzania ni kipi ni ugali au??
 
ugali. ila mboga itategemea ulipo. ila kila uendapo kutakuwa na ugali kwenye vyakula vyao
 
....... ugali na mboga aina yoyote naona kila kabila linakula, japo kuna vyakula vingine vinaliwa zaidi kikabila.
 
Kaugali wajameni. wengine tunakala kutwa mara tatu huku kwetu maeneo ya Ugayambelele
 
watu wa mwambao...wali kwa dagaa/kauzu.
watu wa bara .....ugali kwa maharage

Hivyo hapo juu ni chakula cha kitaifa kwa walalahoi.

watawala....nyama choma,kitimoto,ugali
kuku, wali
 
watu wa mwambao...wali kwa dagaa/kauzu.
watu wa bara .....ugali kwa maharage

Hivyo hapo juu ni chakula cha kitaifa kwa walalahoi.

watawala....nyama choma,kitimoto,ugali
kuku, wali

ila siku hizi hata wanymwezi wakija pwani hawataki ugali ni wali,wali,wali mtindo mmoja (natania tu bagosha!)
 
Back
Top Bottom