Chairman na Mfumo Dume

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Siku hizi katika vikao, semina, Kongamano na matukio mengine ya aina hiyo kumekuwa na hali ya wanawake kutopendelea sana kutumika jina Chairman kwa maelezo kuwa jina hilo linaashiria mwendelezo wa mfumo dume; badala yake jina Chairperson ndilo haswa hupendelewa kutumika kumwita mtu aliyechaguliwa kuongoza tukio hilo. Binafsi bado sioni mantiki ya malalamiko haya kwani nionavyo mimi hakuna tofauti ya kutumia jina Chairman na Chairparson. Hebu angalieni mchanganuo huu hapo chini:

Chairperson.....ukivunja neno person linakupa Per-Son ambalo sehemu ya mwisho inamaanisha mtoto wa kiume (Mvulana),
Chairman------Chair-Man: hapa huwa wanakataa sehemu ya mwisho ambayo humaanisha mwanamume ijapo kwa waingereza wenyewe pia inamaanisha mtu,
Human------Hu-Man,
Woman-----Wo-Man,
Mwanaadam---Mwana-Adam,
Binadam-------Bin-Adam.

Ukiangalia haya maneno, kama itatumika staili ya kuvunjavunja kama ile ya kwenye Chair-Man unaona kwamba hakuna namna ambayo wanawake wanawweza kukwepa kumjumuisha mwanamume. Nadhani hii yawezakuwa ni kwasababu imeandikwa kwenye vitabu vitakatifu kuwa mwnamke alitoka kwenye mwili wa mwanamume. Na kwa mantiki hiyo hakuna sababu ya kutolitimia neno Chairman kwenye vikao.

Wadau mnasemaje?? nauweka wazi mjadala

Ukiangalia haya
 
Back
Top Bottom