CHADEMA yazidi kuitesa CCM Arusha

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
244
HARAKATI za mabadiliko zinazoendeshwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kaulimbiu ‘Vua Gamba Vaa Gwanda' imezidi kushika kasi mkoani hapa baada ya wanachama 70 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Arumeru kuamua kukikimbia.

Wanachama hao walipokelewa jana na Katibu wa CHADEMA mkoani hapa, Amani Golugwa kwenye ofisi zao za mkoa zilizopo maeneo ya Ngarenaro, ambapo viongozi mbalimbali wa mkoa walishiriki hafla hiyo, akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Ephata Nanyaro, Mwenyekiti wa BAVICHA, Ceccilian Ndossi na Mwenyekiti wa CHADEMA, Arumeru Magharibi.

Walipatiwa kadi za uanachama huku kiongozi wao, Vivian Lebulu akikabidhiwa katiba ya CHADEMA na bendera ambapo mwenyekiti wa BAWACHA alimvisha skafu yenye rangi za chama hicho.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Lebulu alisema kuwa wameamua kuachana na CCM baada ya kuona kwa kipindi kirefu imekuwa madarakani, huku ikishindwa kutatua kero za wananchi, akitolea mfano kwenye jimbo lao ambako asilimia 35 ya wanafunzi wa shule za msingi hukaa chini kwa kukosa madawati.

Alisema waliamua kujiunga CHADEMA, ili kushiriki kikamilifu harakati ya kuing'oa madarakani CCM kupitia sanduku la kura mwaka 2015 kutokana na imani kubwa waliyonayo kuwa chama hicho makini kina sera nzuri za kuwakomboa wanyonge.

Kwa upande wake, Katibu wa CHADEMA Mkoa, kabla na baada ya kuwapatia wanachama hao kadi, aliwasomea haki na wajibu alionao mwana-CHADEMA popote alipo huku akiweka msisitizo umuhimu wa kupinga uonevu na kupigania haki na kulinda utu wa watu wote kwa gharama yoyote.

Aidha, alisema operesheni hiyo itahamia wilayani Monduli Juni 24, wanakotarajia kuvuna wanachama wengi, hasa kutokana na maombi ya muda mrefu ya wananchi wa maeneo hayo.


Source: TZ Daima

Mzee EL kaa tayari M4C iko mlangoni kwako....
 
Aidha, alisema operesheni hiyo itahamia wilayani Monduli Juni 24, wanakotarajia kuvuna wanachama wengi, hasa kutokana na maombi ya muda mrefu ya wananchi wa maeneo hayo.
hapa tunasubiri kwa hamu sana

 
Back
Top Bottom