Chadema yawasha moto Mkoa Mpya wa NJOMBE

Mngendalyasota

Senior Member
Jan 22, 2011
171
48
WanaJf, juzi nilikuwa Njombe, Tarafa ya Mdandu nilichoshuhudia huko ni kwamba makamanda Thomas Nyimbo na Alatanga Nyagawa(viongozi CHADEMA wilaya) wanafungua matawi vijijini na mwitikio wa wananchi ni mkubwa sana. Watu wanaona fahari mnoo kwa sasa kutundika bendera za Cdm ktk vijiji mbalimbali isipokuwa kijiji cha Igwachanya ambapo ndo makao makuu ya wilaya mpya ya Wanging'ombe.
 
WanaJf, juzi nilikuwa Njombe, Tarafa ya Mdandu nilichoshuhudia huko ni kwamba makamanda Thomas Nyimbo na Alatanga Nyagawa(viongozi CHADEMA wilaya) wanafungua matawi vijijini na mwitikio wa wananchi ni mkubwa sana. Watu wanaona fahari mnoo kwa sasa kutundika bendera za Cdm ktk vijiji mbalimbali isipokuwa kijiji cha Igwachanya ambapo ndo makao makuu ya wilaya mpya ya Wanging'ombe.
Hizi ni habari njema sana, maana Njombe ni moja mikoa ambayo imekuwa nyuma sana katika harakati za kujikomboa kutoka katika makucha ya CCM. Big up kamanda Nyimbo na Nyagawa.
 
Hiyo nimeipenda, safi sana makamanda wetu. Pigeni kote kote, hata wazee wetu vijijini sasa wanatuelewa maana mwanzo tulikuwa tukitengwa kwa imani kwamba kuwa opposition parties tunajitakia vita, hali ni tofauti.
Nendeni hadi Ilembula,Kipengere,Makoga, Ulembwe, Lugenge,Luponde,Uwemba,nk watu wanahitaji elimu kidogo tu wafanye maamuzi sahihi. Tupo pamoja, nami sifanyi mchezo ktk maeneo yangu. Ukipata elimu mpe na mwenzako.
 
Big up. Kitendo cha CDM kukaa KIMYA wadau wanapotafuta bendera itaonekana vilevile CDM wanatabia ya CCM ya kuchekelea matatizo.
Mkuu sielewi what is happening there, juzi kuna kamanda wa Same Makanya aliomba kadi 500 akapelekewa 25 tu, kweli iliniuma sana.
 
safi sana ila naomba tusaidiane nawote maana huu mkoa hata mama yetu chausiku (spika) anatokea hukohuko so nyimbo ni jembe anaweza nmi naenda ijumaa kujoin
 
Niliiona hiyo, ni kweli mwitikio umekuwa mkkubwa sana sasa,vjana nilikuta wametundika bendera za cdm kwenye vijiwe vyao
 
katibu wa mkoa wa iringa tunakupo chadema tunakupoponge kwa kuingiza wanachama wapya mia moja na kumi eneo la kitanzini
 
Kwa nini Igwachanya hawataki ukombozi??!
Mleta mada kama una maelezo katika hili itakuwa vyema kama ukiyatoa! Yatasaidia wadau kupanga mikakati!
 
Igwachanya panatawaliwa na ukoo mkubwa wa matajiri wanaitwa Kilamlya, hawa kutokana na biashara zao hawapendi sana kuonyesha influence yao kisiasa.Lakini pia ni ukoo ambao haukwenda shule. Pia ndiyo ngome ya NW wa maji Mh Gerson Lwenge (ccm) hivyo watu wengi wanashindwa kuamua kwa sasa wakisubiri lolote la kimaendeleo kutoka kwa huyu naibu waziri.Mbali na hivo Igwachanya ilivurugwa sana na siasa za 2010 ambapo yeyote aliyeshabikia CDM alifuatwa na viongozi wa serikali ya kijiji na kuhumiwa na victims hawakujua nini cha kufanya baada ya hapo. Hata Thomas Nyimbo mgombea wa ubunge 2010 CDM alinyimwa mahali pa kufanyia mikitano mara 3.
 
Si ndio kwao TUNTEMENKE HUKO??

Nadhani jamaa anatamani kunywa sumu ya panya!!

M4C, Bila Huruma!
 
sawa..go ahead

Kama ID yangu invyojieleza, Igwachanya ndo home. Nilikuwa huko a month ago. Hakika kuna-class dogo tu linalotakiwa kuwa written off pale kijijini ili mambo yaende, akiwemo Diwani. Nilijitahidi sana kuelimisha na kuhamasisha watu hasa kundi la vijana. Kiukweli, tatizo kubwa ni uelewa wa watu kwani ukiongea nao wanaonekana kuvutiwa na M4C.

Chamsingi, uongozi wa wilaya wa M4C lazima uweke mikakati endelevu katika kuhakikisha tawi la CHADEMA linakuwepo likiongozwa na watu makini. Aidha, Igwachanya ni kijiji chenye ushawishi mkubwa ktk wilaya mpya ya Wanging'ombe. Hivyo, kuwekeza nguvu Igwachanya kutarahisisha kuzoa vijiji vyote kama kusukuma mlevi vile! Hata hivyo, viongozi wa M4C wapo ingawa wanajitolea tuu. Nao ni Dickson Kiswaga-Katibu na mama Luvanda-Mwenyekiti.

Sasa ushauri wangu kwa M4C, wajitahidi ku-organize mkutano mkubwa wa ukombozi ukiongozwa na watu makini kama akina Rev. Msigwa, Sugu, V. Nyerere, Zitto, Mnyika, nk. mbona hadi mabalozi manyumba kumi watajivua magamba! Pia, kuwe na inspiration endelevu, tusiwatelekeze wale watakao kuwa wamejivua magamba!

Baada ya magamba kugundua potentiality ya kijiji hiki, kwenye uchaguzi wa 2010 Bibi Kiroboto, Riz 1, na uongozi wa CCM Mkoa na wilaya walifanya kufuru ya kumwaga hela kwa wenyeviti wa vijiji na mitaa na kutishiwa kuwa endapo jimbo lingeenda upinzani basi nao wangeadhibiwa kwa kupoteza vibarua vyao. Kwa kuhitimisha, Igwachanya ndo moyo wa M4C kama tunataka siasa za jimbo hili ziwe za manufaa kwa taifa.
 
.....ni vizuri kama Nyimbo na Nyagawa wanafanya kazi hiyo kwa roho moja....nasema hivyo kwani kuna kipindi uongozi mzima wa CDM-njombe walikuwa wanasigana kisa nafasi ya mwenyekiti wa chama jambo ambalo lilionekana kutaka kuwavunja moyo wanachama wanaopenda chama hasa vijana. Sasa kilichobaki ni kuendelea kukaza buti ili waweze kungoa visiki vyote vya CCM vilivyojibanza kila kona hususani hapo Njombe mjini, Ramadhani Kihesa na Maeneo yote ya Nazareti na Mjimwema.
 
Back
Top Bottom