CHADEMA yatangaza kuanzisha Operesheni Maalum nchi nzima kwa Mwaka Mzima bila kukoma

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,428
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza Operesheni kabambe ya kuzunguka Nchi nzima kuelimisha na kuamsha wananchi Nchi nzima.

Operesheni hiyo ambayo Jina lake linahifadhiwa kwa sasa imetangazwa na Mwenyekiti wa Chama hicho , Freeman Mbowe alipokuwa anaongea na Waandishi wa Habari Jijini Arusha.

Mh Mbowe amesema kwamba Operesheni hiyo ni matunda ya Kikao cha Kamati Kuu kilchoketi Mjini Iringa kwa siku 2 kabla ya Mikutano ya hadhara ya Kanda ya Nyasa, ambako amedai kwamba Pazia la Operesheni hiyo litafunguliwa rasmi mwisho wa mwezi huu huko Mkoani Kigoma, na hatimaye kuvuruga kanda ya ziwa Victoria hadi kanda ya Serengeti.

Ikumbukwe kwamba baada ya kuanza operesheni hiyo haitasimama kwa mwaka mzima, ambapo imepangwa kufika kwenye Mikoa, Wilaya, Kata, Vijiji , Vitongoji na Mitaa yote iliyoandikishwa Nchini Tanzania.

Malengo Makuu ya Jambo hili la gharama kubwa ni kuhakikisha kwamba Moto wa kudai KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI unawafikia watu wote wa kada zote Nchi Nzima.

Mungu ibariki Chadema.

FB_IMG_1672921103951.jpg
 
Kwa wale wasiojua ni operesheni kuhusu nini naomba niwafafanulie... ni operesheni ya kuhakikisha Mama Samia anashinda kwa kishindo mwaka 2025. Kimsingi tarehe kamili ya kuanza operesheni ni tarehe 08/03/2023 mkoani Kilimanjaro kwenye mkutano wa BAWACHA. Ushahidi usiotia shaka kuhusu hiki ninachowaambia ni Mama kualikwa kama mgeni rasmi kwenye mkutano huo.

Nawasihi watanzania wote kwa sasa tumuunge mkono Mheshimiwa Mbowe kwasababu anaupiga mwingi. Hata hizi kauli tata za Lema ni mkakati wao maalum wa kumuongezea Mama kura. Tunawashukuru sana. Mimi nimeshamwelewa Mbowe na Lema hivyo tuwaunge mkono wanatusaidia 2025.
 
Back
Top Bottom