CHADEMA yajitosa kwa kupigwa risasi Sheikh Ponda

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume huru yenye nguvu ya kimahakama kwa ajili ya kuchunguza vifo, mauaji na mateso yaliyowahi kufanywa na vyombo vya dola kwa raia wasio na hatia badala ya kamati zisizo na manufaa. Kauli hiyo ya chama hicho inatokana na tukio la kupigwa risasi kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kauli hiyo ya CHADEMA ilitolewa Jumanne wiki hii na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Profesa Abdallah Safari, wakati alipozungumza na wanahabari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam. Msomi huyo wa masuala ya sheria, alisema matukio ya watu kuuawa na kuteswa yamekuwa yakiongezeka na kauli ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa polisi wawapige wanaoleta vurugu, inaonyesha kuwa kuna mkono wa serikali kwenye matukio hayo.

"Hatuna imani na kamati iliyoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza tukio la Ponda inayoongozwa na Isaya Mungulu. Huyu bwana ametumwa katika maeneo mengi kuchunguza matatizo na hadi sasa hakuna taarifa yoyote aliyowahi kuitoa. "Iundwe tume huru ya kimahakama au kijaji kwa ajili ya kuchunguza vifo, mauaji na mateso yanayofanywa na vyombo vya dola. Matukio ya kuchunguzwa na tume hiyo ni kama mauaji ya mwandishi Daudi Mwangosi, mateso ya Absalom Kibanda, Mwembechai, Bulyanhulu, kuteswa kwa Dk. Stephen Ulimboka na tukio la Arusha," alisema.

Akizungumzia suala la Ponda, Safari aliweka wazi kuwa kwa utaalamu wake wa kisheria, Polisi walidhamiria kumuua Sheikh Ponda na wala si kumjeruhi ili kumkamata kwa urahisi. "Nimesimamia kesi nyingi za mauaji, Sheikh Ponda amepigwa katika bega la kulia karibu na kifua kisheria mtu anapopiga maeneo ya kifua amedhamiria kuua, hiyo inakuwa ni kesi ya kuua na wala si kukusudia kuua ‘manslaughter' laiti Sheikh Ponda angefariki basi polisi wangekuwa na kesi ya kujibu.

"Nilikuwa Morogoro wiki hii nimekutana na watu waliokuwepo kwenye eneo la tukio na hata ndugu yake Sheikh Ponda alipokuwa Muhimbili pale Taasisi ya Mifupa - MOI alizungumza wazi kuwa polisi walihusika kumjeruhi kwa risasi kiongozi huyo katika harakati za kutaka kumkamata," alisema profesa huyo. Aidha msomi huyo aliwaeleza wanahabari kuwa ushahidi uliotolewa na madaktari juu ya jeraha la Sheikh Ponda kutokuwa la risasi si wa kuzingatiwa sana kwani kisheria ushahidi wa kitaalamu ni ushahidi wa pili baada ya ule wa mtu aliyekuwepo eneo la tukio.

Alihoji kuwa kwanini serikali inang'ang'ania kuchukua ushahidi wa madaktari wakati Sheikh Ponda hakujeruhiwa chumbani. Wakati polisi wanafika eneo la mkutano kulikuwa na watu wengi sana wanatosha kuwa mashahidi. "Wakati Jeshi la Polisi likijikanganya kwa kujaribu kuficha ukweli wa tuhuma zinalolikabili za kumpiga risasi kiongozi huyo wa dini, kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, RPC Faustine Shilogile amenukuliwa na vyombo vya habari vya nje ya nchi (Uingereza) akikiri kuwa jeshi hilo linahusika kumpiga risasi Sheikh Ponda katika harakati za kutaka kumkamata," alisisitiza Profesa Safari.

Mbali na CHADEMA, Chama cha Wananchi (CUF) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba kimelaani tukio hilo na kutaka kuitishwa kwa uchunguzi huru. Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) pia ni miongoni mwa taasisi zilizolaani tukio hilo na kumtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile kujiuzulu ili kupisha uchunguzi huru wa tukio hilo -

See more at: Raia Mwema - CHADEMA yajitosa kwa Sheikh Ponda
 
Sheikh Ponda anasema serikali hii inaongozwa kwa mfumo kristo! Swali kwa Chadema ni nini kauli yao kwa mahubiri haya Sheikh Ponda kabla ya kuanza kumtetea,Chadema inasemaje juu ya MoU kati ya kanisa na Serikali???? Haya ndio mambo ya kuwekewa msimamo na Chadema kabla ya kugeuza jambo hili kwa siasa nyepesi nyepesi!
 
CHADEMA si msemaji wa Serikali,CHADEMA si msemaji wa Wakristo hivyo haiwezi kuwa na Opinion juu ya MoU ya Kanisa Ingawa ina wanachama ambao ni wakristu,Waislamu,wahindu,wenye dini za asili na wasiokua na dini.CHADEMA kitakuaje msemaji katika haya uliyotaka?
 
Chadema wanatania au wanamaanisha mbona majanga ,

leo chadema inamtetea shehe ponda kweli siasa sanaa tena ya kupindukia kabisa.
 
Kumbe siku hizi unaweza kufungwa gori halafu ukashangilia wakati umefungwa menyewe.
 
CHADEMA si msemaji wa Serikali,CHADEMA si msemaji wa Wakristo hivyo haiwezi kuwa na Opinion juu ya MoU ya Kanisa Ingawa ina wanachama ambao ni wakristu,Waislamu,wahindu,wenye dini za asili na wasiokua na dini.CHADEMA kitakuaje msemaji katika haya uliyotaka?

Well said....!

Tatizo: Je, umeeleweka kweli au ndo umewachanganya zaid?
 
Sheikh Ponda anasema serikali hii inaongozwa kwa mfumo kristo! Swali kwa Chadema ni nini kauli yao kwa mahubiri haya Sheikh Ponda kabla ya kuanza kumtetea,Chadema inasemaje juu ya MoU kati ya kanisa na Serikali???? Haya ndio mambo ya kuwekewa msimamo na Chadema kabla ya kugeuza jambo hili kwa siasa nyepesi nyepesi!

Itendee haki Chadema yenye mamilioni ya wafuasi wa dini zote. Sio dini zote zina interest na mambo ya MoU.
Ponda anatetewa na Chadema kama vile Chadema inavyotetea wananchi wanyonge wa kijijini kwenu pasi na kuuliza imani zao
 
Chadema ni chama kinachofuata upepo tu.

Wameona msururu wa watu wameenda kumuona Ponda hospitali wakagundua kumbe Ponda anaweza kuwa mtaji kwao kisiasa.

Chadema ni chama kinachoendeshwa kwa misingi ya kilaghai...
 
Sheikh Ponda anasema serikali hii inaongozwa kwa mfumo kristo! Swali kwa Chadema ni nini kauli yao kwa mahubiri haya Sheikh Ponda kabla ya kuanza kumtetea,Chadema inasemaje juu ya MoU kati ya kanisa na Serikali???? Haya ndio mambo ya kuwekewa msimamo na Chadema kabla ya kugeuza jambo hili kwa siasa nyepesi nyepesi!
pamoja na hayo uliyosema haialalishi polis kuua au kujeruhi sheikh ponda!
 
Kila raia ana haki ya kulindwa bila kujali itikadi yake,dini au kabila lake! Chadema wako sahihi!
 
CHADEMA si msemaji wa Serikali,CHADEMA si msemaji wa Wakristo hivyo haiwezi kuwa na Opinion juu ya MoU ya Kanisa Ingawa ina wanachama ambao ni wakristu,Waislamu,wahindu,wenye dini za asili na wasiokua na dini.CHADEMA kitakuaje msemaji katika haya uliyotaka?

Acha kujibizana na Vilaza, hata hiyo Mou hawajaielewa wao wamehubiriwa na vilaza wenzao wameishia kukariri
 
Sheikh Ponda anasema serikali hii inaongozwa kwa mfumo kristo! Swali kwa Chadema ni nini kauli yao kwa mahubiri haya Sheikh Ponda kabla ya kuanza kumtetea,Chadema inasemaje juu ya MoU kati ya kanisa na Serikali???? Haya ndio mambo ya kuwekewa msimamo na Chadema kabla ya kugeuza jambo hili kwa siasa nyepesi nyepesi!

Huo mfumo kristo unaongozwa na Waislam? Mi nina hakika hata nafasi zote wangepewa Waislam bado msinge acha kulaumu, Tatizo si mfumo kristo tatizo ni UELEWA na KUJITAMBUA
 
CCM walienda nao hospitalini?

Mkuu,

Juzi wewe na Ben Saanane mlikuwa mstari wa mbele kumuunga mkono Le Mutuz aliposema Ponda ni mtu hatari. Sasa leo chama chenu kimeona kuwa kumuunga mkono Ponda kuna maslahi kisiasa, mnamgeuka Le Mutuz.

Ebu chagueni upande mmoja ili msiwachanganye wanaowasoma.
 
Last edited by a moderator:
It is not about a person......rather it is about the "ACT" that was executed upon the person. It does not become right simply b'se some CDM follower are or are not supporting that person's ideology. The ACT done on Ponda is inhuman and unlawful...!!!! Period!! It does not matter which political side you are or which belief you have or your religion or tribe etc....IT DOES NOT MATTER!

Think a bit my dear!!

Chadema wanatania au wanamaanisha mbona majanga ,

leo chadema inamtetea shehe ponda kweli siasa sanaa tena ya kupindukia kabisa.
 
Chadema ni chama kinachofuata upepo tu.

Wameona msururu wa watu wameenda kumuona Ponda hospitali wakagundua kumbe Ponda anaweza kuwa mtaji kwao kisiasa.

Chadema ni chama kinachoendeshwa kwa misingi ya kilaghai...
Usiwe mjinga wewe...Chadema kimesimamia sheria, hawajaongelea matatizo ya ponda kwa jamii kwani ni obvious,ila Polisi walivyokwenda na walichofanya sivyo kisheria.Ktk sheria haki ni kwa wote hata mualifu.

hakuna cha kugundua, hata ulimboka,kibanda na unafiki wake, na wengine chadema kililaani na hadi leo wanasema bila woga.

Ni wewe na wengine wajinga tuu ndio mnaswing tuu ili muwe upande tofauti na cdm,ipo siku mtajikuta hakuna option.
 
CHADEMA si msemaji wa Serikali,CHADEMA si msemaji wa Wakristo hivyo haiwezi kuwa na Opinion juu ya MoU ya Kanisa Ingawa ina wanachama ambao ni wakristu,Waislamu,wahindu,wenye dini za asili na wasiokua na dini.CHADEMA kitakuaje msemaji katika haya uliyotaka?

Chadema wanatafuta sympathy vote za waislam kujifanya wanamtetea Ponda ni unafiki
 
Back
Top Bottom