Huu ni ushauri wa bure kwa CHADEMA na Wanaharakati (wote ndani na nje), ikiwapendeza, waungwana kabisa.
Kutoka kwa mwananchi, mdau.
Kwenu waheshimiwa, niwasalimu kwa jina la solidarity: "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu."
Tulikuwa tuko vizuri. Tulikuwa wamoja. Tulikuwa tukitembea vifua mbele kuelekea kwenye nchi ya ahadi. Nchi yenye asali na maziwa. Shetani gani katupitia, ghafla tushindwe kuelewana?
Wanasema waswahili, ndugu wawili wakigombana, chukua jembe ukalime. Siku wakipatana, chukua kapu ukavune. Misahafu inasema, heri wapatanishi kwa maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Tusikubali kufarakanishwa kirahisi. Tusikubali kufarakana kirahisi. Tunajenga nyumba moja. Pamoja, tuko vizuri zaidi.
Kulikoni kutowafikiria viongozi wa dini au hata na waungwana wengine, wa ndani na nje ya vyama au hata ndani na nje ya nchi, ili kuwezesha kusaka mapatano?
Kulikoni kutowafikiria waungwana kama TEC, KKKT, Waislam, madhehebu zingine nk au hata na wasomi, wakiwamo nguli? Hawawezi kutuangusha watu hawa. Wengi wao wamekuwa nasi katika dhiki hizi za mapambano.
Fikiria akina Sheikh Ponda, Askofu Bagonza, Askofu Niwemugizi, Prof. Shivji, Askofu Mwamakula (pole zake kwa msiba) nk, nk, kwenye jopo kama hilo?
Kwamba wengine tumelazimika kupiga kelele hivi, tukisisitiza kutafuta mapatano bila kujali changamoto zote zilizotukabili, ni kwa sababu tukiamini Tanzania ya namna hii:
Ilikuwa karibu zaidi katika umoja wetu kuliko wakati mwIngine wowote. Fikiria Tanzania hiyo. Kizuizi gani Ya-Rabi kiwepo njiani hapo, kitushinde kukiondoa kwa ajili ya ushindi huu ulio karibuni na dhahiri hivyo?
Kulikoni tusiweke yoyote binafsi pembeni, tukajaribu kutafuta mapatano? Ikishindikana, basi ikawe imekuwa bahati mbaya. Kwamba haikuwa riziki, ila kwa dhati yetu kabisa, tulijaribu?
Wakulima wanasema majembe yaliyopo pamoja kukwaana, hutokea. Tutafute mapatano nafasi hii ya dhahabu tulipo, isituponyoke kirahisi.
Kutengana kwa makundi mawili haya ni hasara kubwa kwa yote. Hali ni faida kubwa mno kwa mahasimu wetu wasiopenda katu, tuelewane.
Wanasema waswahili, "Wagombanao, ndiyo wapatanao." Tumtangulize Mola mbele. Palipo yeye hakuna lisilowezekana. Penye nia, pana njia.