CHADEMA walishana yamini, kwa udi ama uvumba, maandamano kupigwa kona zote nchi

sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
1,662
Ikiwa bado chadema wapo katika Operation ya pamoja daima katika maeneo mbalimbali ya nchi sasa imegundulika main goals za hii operation. Watu wamekuwa wakiuliza ni nini msingi wa hii operation lakini kwa kufuaatilia hotuba za viongozi na makada wa chadema Dr Wilbroad Slaa, mh Mnyika, Tundu lissu, Godbless Lema, john Heche, joseph mbilinyi kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti wamekuwa wakisema wazi wazi kuwa kama daftari la kudumu la wapiga kura halitarekebishwa tanzania itaingia barabarani kulidai.

Godbless Lema amesema hayo akiwa tabora, john mnyika nae amesikika jana mjini bukoba akisema haki ya kupiga kura haitaombwa, itapiganiwa, na ndugu tundu lissu akiwa sombetini alisema umma ndio mamlaka ya mwisho katika hili taifa, akaapa lazima daftari la kudumu la wapiga kura lirekebishwe laa sivyo maandamano yatapigwa kona zote za taifa.

Kanakwamba hiyo haitoshi ndugu Heche,mwenyekiti bavicha jana kusema chadema itatumia chopa kumi kuongoza maandamano angani wakati wapiganaji wengine watakuwa ardhini hii ni kama daftari la kudumu la wapiga kura halitarekebishwa

My take.
Siasa za chadema utafikiri hii nchi bado inatawaliwa na wakoloni, ninafuatilia sana kwa ukaribu aina ya matamshi ya viongozi wa chadema kwenye hii mikutano wanahibiri chuki dhidi ya serikali, wanawalisha sumu kali wananchi,kama tutaendelea kuilea chadema ipo siku watatugeuka na kutula nyama. Tukikataae hiki chama kwa nguvu zote.
 
Nchi bado ipo chini ya Mkoloni Mweusi. Tena huyu wa sasa ndio hatari. Nyerere katika harakati kupitia TANU haijawahi kuzushiwa tuhuma za Ugaidi
 
..

...M4C - OPD... KAZINI Hapa tupo njombe !!!!


hii kitu watu wamepata pressure ..
.
blogger-image-1888611968.jpg

 
Hiyo ndiyo kauli mbiu ya wananchi. Kwanini unaogopa kauli ya kurekebisha daftari la wapiga kura? Ni swala la msingi kwa serikali kufanya hivyo,ili kila mtu apewe uhuru wa kupiga kura kuchagua viongozi halali. Miaka zaidi ya mitano inahitaji updates,na ukiangalia vijana wengi bado hawajaandikishwa. Itazame vizuri kauli yako. Angalia,nini kinafanyika Ukraine na sababu zake kabla ujalaumu kauli za wenzio
 
Nchi bado ipo chini ya Mkoloni Mweusi. Tena huyu wa sasa ndio hatari. Nyerere katika harakati kupitia TANU haijawahi kuzushiwa tuhuma za Ugaidi

No wonder Kikwete aliwahi kunena hiki sii chama cha siasa, ni kikundi cha wanaharakati
 
..

...M4C - OPD... KAZINI Hapa tupo njombe !!!!


hii kitu watu wamepata pressure ..
.
blogger-image-1888611968.jpg


Ni kweli ilikuwa 2010 hii mwambia Dr Sla aende hapo leo asipohutubia watoto watakaoenda kushangaa chopa
 
Kosa lipo wapi ndugu watu kudai haki yao ya kupiga kura na kwanini Bomani alivyosema daftari liboreshwe amkumuita muhaini? Tuwe wakweli ccm ndio wanaleta matatizo nchini mwetu
 
Ikiwa bado chadema wapo katika Operation ya pamoja daima Watu wamekuwa wakiuliza ni nini msingi wa hii operation lakini kwa kufuaatilia hotuba za viongozi na makada wa chadema Dr Wilbroad Slaa, mh Mnyika, Tundu lissu, Godbless Lema, john Heche, joseph mbilinyi kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti
Ukiangalia hayo majina Dr Wilbroad Slaa, mh Mnyika, Tundu lissu, Godbless Lema, john Heche, joseph mbilinyi jibu ni CRUSADE.
 
Back
Top Bottom