Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Ubongo wa wananchi wengi wa Tanzania ni sawa nawa Rais,ambaye hajui nini matizo la umasikini wao. Watanzania wanajua wao ni masikini lakini hawajui kwanini wao ni masikini, hivyo hawajui dawa ya kuuondoa huo umasikini.Siku watakapojua kuwa wao ni masikini kwa sababu ya kuwa na vingozi wabinafsi,wezi waliokithiri,wala rushwa waliokithiri na wasiowajibika,CCM haitakuwa na chake. Kushindwa katika uchaguzi haimaanishi kuwa CCM si chama kilichosheheni kila aina ya ubadhilifu unaoiletea nchi hii umasikini.Wanashindwa kwa kuwa watanzania hawaendi kupiga kura ili kuleta mabadiliko ila kutimiza tu wajibu na haki yao ya kupiga kura.It is the matter of time
Kweli kabisa Nyangumi,
Na hiki ndicho ccm inaficha watu wasijue. Badala ya kuacha wananchi wajue kuwa wako masikini kutokana na wizi wa viongozi wa serikali ya ccm ambayo imeongoza nchi miaka yote hii!
Wao wanaelekeza blame kwa wengine huku magazeti yakitumiwa kuua wapinzani wa serikali au mgombea kisiasa. Unakumbuka kampeni chafu kuwa CUF ni chama cha kidini?
CCM iko responsible kwa umasikini wa Tanzania. Kama uko marekani utakubaliana na mimi kuwa uongozi wa nchi unachangia sana kwenye maendeleo ya nchi - Angalia tofauti kati ya utawala wa Clinton na wa huyu Joji Kichaka>