CHADEMA: Tunaunga mkono uhuru wa Zanzibar

zanzibar huru

JF-Expert Member
May 28, 2012
218
108
Si serikali 1 au 2 au3

CHADEMA kama chama kinachotetea haki za wanyonge haiwezi kuwa na sera za unyanyasaji za ccm ndio maana inaunga mkono Wazanzibari kujiamulia kama wanataka kujitoa kwenye Muungano au la

sasa hizi propaganda za kutuambia kuwa CHADEMA ni chama cha wachagga na wakristo zimegonga mwamba

kama CHADEMA wamesimamia haki na wameamua kutounga mkono udhalimu wa Muungano huuu basi sioni sababu kwa nini CHADEMA wasichukue Zanzibar

Sasa tuambieni matawi tenu yako wapi huku bwe juu?
 
Sio kweli! Msimamo wa Chadema kama chama na kama ambavyo viongozi wake wa ngazi mbalimbali wamekuwa wakiwaeleza wananchi ni huu:

WANANCHI WAACHIWE WAAMUE WENYEWE AINA YA MUUNGANO WANAOUTAKA.

Huo ndio msimamo rasmi uliotolewa hata Bungeni na Waziri Kivuli wa Kambi Rasmi ya Upinzani Mh. Tundu Lissu. Kwa uelewa finyu wa wabunge wa magamba wakishirikiana na wale wa CUF waliishia kumzomea na kumtolea kashfa za kila aina. Huo ndio msimamo rasmi wa Chadema ninaoujua mimi labda kama wametoa mwingine mchana huu.
 
Umenichekesha kweli ' zanzibar huru'.....Zanzibar ikishakuwa huru, CHADEMA itaenda kufanya nini huko? Hayo matawi unayoomba ni ya nini mkishajitenga? Halafu, mbona mnachoma moto ofisi zao?
 
Sio kweli! Msimamo wa Chadema kama chama na kama ambavyo viongozi wake wa ngazi mbalimbali wamekuwa wakiwaeleza wananchi ni huu:

WANANCHI WAACHIWE WAAMUE WENYEWE AINA YA MUUNGANO WANAOUTAKA.

Huo ndio msimamo rasmi uliotolewa hata Bungeni na Waziri Kivuli wa Kambi Rasmi ya Upinzani Mh. Tundu Lissu. Kwa uelewa finyu wa wabunge wa magamba wakishirikiana na wale wa CUF waliishia kumzomea na kumtolea kashfa za kila aina. Huo ndio msimamo rasmi wa Chadema ninaoujua mimi labda kama wametoa mwingine mchana huu.

It makes a lot of sense. Angesikilizwa Lissu na ushabiki wa kisiasa kuwekwa pembeni, haya yote yanayoendelea Zenji yasingefika hapo yalipofika sasa.
Kwa kuwa tu alisema mpinzani, basi ikaonekana ni chachu ya uhai wa muungano.
Sidhani kama kuna mwananchi ambaye hapendi muungano, ila uwe ni muungano unaoleta manufaa kwa pande zote mbili na uwe muungano ulioridhiwa na pande zote mbili.
Muungano ulipo sasa unahitaji upate maoni na mapendekezo kutoka pande zote mbili. Kama hakuna maridhiano na upande mmoja hauridhiki, TUPILIA MBALI kuliko kutaka kukaribisha umwagaji damu usio na maana yeyote kwa kuung'ang'ania.

Aliyesema Muungano usiingiliwe wala kujadiliwa sambamba na ukusanyaji maoni ya katiba mpya, ndiye aliyeleta hii tafrani yote.(kama sikosei aliyenena haya ni mkuu wa kaya). Sasa UAMSHO wameamka (sijui walilala wapi)
 
Watanzania wenzangu amini nawambia kuwazui WA zanzibari kutowa maoni halita tusaidia
 
Si serikali 1 au 2 au3

chadema kama chama kinachotetea haki za wanyonge haiwezi kuwa na sera za unyanyasaji za ccm ndio maana inaunga mkono wazanzibari kujiamulia kama wanataka kujitoa kwenye muungano au la

sasa hizi propaganda za kutuambia kuwa chadema ni chama cha wachagga na wakristo zimegonga mwamba

kama chadema wamesimamia haki na wameamua kutounga mkono udhalimu wa muungano huuu basi sioni sababu kwa nini chadema wasichukue zanzibar

sasa tuambieni matawi tenu yako wapi huku bwe juu?
Sijaelewa hapo
 
Kero namba moja ya Muungano huu ni 'kuendelea kuwepo kwa muungano', and the best solution ya kero hii ni ku-terminate muungano huu. Serikali zote mbili zinajua hili. Kinachoendelea sasahivi huko Zenj ni matokeo ya muungano huu kuendelea kuwepo. Kwa maoni yangu mimi, sioni kama kuna haja ya kuwaachia wananchi eti waamue ni aina gani ya muungano wanaouhitaji wakati upande mmoja wa muungano huu (ie Zanzibar) unaonyesha wazi kwamba nguvu ya wanainchi wasioutaka muungano ni kubwa kuliko ile ya wanainchi wanaopenda muungano.
 
Hivi watanganyika(Azania) hivi ya nn kulazima muungano ili hali upande mwingine wana-disagree?! Sioni sababu ya kuwa na muungano kama huu na hapa napingana na msimamo wa chama changu CDM kuhusu serkal 3, hapa hamna haja ya serkali 3 wala muungano cha myhimu ni kuwaachia hao midebwedo na tuone kama watakula karafuu 2´.
"LET ZANZIBAR GO, LET THEM EAT THEM"
 
Back
Top Bottom