CHADEMA: Tumejiandaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Chadema yasema imejiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa.

Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimesema kinajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu na haitosusia uchaguzi huo ili kukabiliana na hujuma mbalimbali zinazofanywa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chadema jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa chama hicho Dr Willbroad Slaa amesema kamwe hawatasusia uchaguzi huo kwani Tanzania ina vyama vingi vya siasa wao kama Chadema pekee hawawezi kusitisha utaratibu wa uchaguzi na kwa kufanya hivyo wataiachia CCM ushindi.
-
Naye mwanasheria mkuu wa chama hicho Tundu Lissu amesema chama chake kinaungana na baadhi ya taasisi na viongozi wa dini kulaani matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika mchakato wa katiba tokea hatua za awali mpaka upigaji wa kura unaoonekana kwenda kinyume, hivyo Chadema inajiandaa kuanza kampeni ya kuzunguka nchi nzima kuwaelimisha wananchi kuipigia kura ya hapana rasimu ya katiba iliyopitishwa na Bunge. Mia

Cjanzo: ITV
-
 
Kusema la ukweli Mimi bado sijakutana na hayo matayarisho yao.
CCM wanawatumia mabalozi wao kupita nyumba kwa nyumba ila ukawa siwaoni.
 
Back
Top Bottom