CHADEMA sasa itakuwa na kadi za aina 5 za uanachama zitakazolipiwa viwango tofauti kwa mwaka

Endelea kuwavuta mkuu kwa vile na ww upo kwenye kundi la wapigaji basi hii ni habar njema kwako na kwa familia yako.
 
MUHIMU SANA : Pamoja na kadi hizo kuwa na viwango tofauti lakini hadhi ya wanachama wote ni sawa , viwango tofauti vimewekwa kwa ubunifu tu ili kuongeza mapato ya Chama yatayowezesha kijiendeshe bila kukwama
I support 100%. Ruzuku tuwaache wao wazitafune..

Chama makini - viongozi makini.
 
1.Kadi ya bluu (2500) kwa mwaka

2.kadi ya fedha (25,000) kwa mwaka

3.kadi ya dhahabu (50,000) kwa mwaka

4.Kadi ya Platnum (100,000) kwa mwaka

5.Kadi ya Almasi (200,000) kwa mwaka

Huu ndio mpango mpya utaowezesha chama kujiendesha kwa mapato yake chenyewe badala ya pesa za ruzuku ambazo Chadema ilishazikataa kitambo kwa vile hazikuwa za halali.

MUHIMU SANA : Pamoja na kadi hizo kuwa na viwango tofauti lakini hadhi ya wanachama wote ni sawa , viwango tofauti vimewekwa kwa ubunifu tu ili kuongeza mapato ya Chama yatayowezesha kijiendeshe bila kukwama .

Ombi : Chadema ituwekee utaratibu sisi wengine tulio na uwezo wa kulipa zaidi ya hivyo viwango vyao hata kwa kutuandalia risiti maalum bila hata kubadilisha viwango vilivyowekwa , Kwa mfano naweza kulipa milioni 3 lakini nikaomba nipewe kadi ya bluu ambayo ada yake kwa mwaka ni 2500/= tu

View attachment 1800416

Wasiweke wawe na hadhi sawa... ukishatenganisha viwango umeweka madaraja.. jambo la maana ni kusema madaraja hayo yanakuja na ujiko upi... Sasa kuna vitu ambavyo wote wanaweza kuwa sawa (kama kupiga kura, kuomba nafasi za uongozi, n.k) lakini kuna vingine mnaweza kuwawekea ujiko kidogo... kwa mfano uliotolea...

Kuwe na ngazi ya Wafadhili - wanaotoa 3,000,000 kwenda juu... na hawa wanapewa hata vyeti au alama fulani za kujionesha kuwa wao ni wafadhili...
 
Tokea nipate kadi ya Chadema 1999 nilipomaliza Chuo sikuweza kulipa ada ya mwanachama kwa upuuzi huu wa ruzuku.
Wawahi haraka ili chama kiendeshwe na wanachama wenye mapenzi.

Nimeshiriki kuichangia chama cha Demokrat ya USA kwasababu ya utaratibu wao.

Sasa Chadema iende hatua moja mbele ya kutengeneza platform ya kufanya tathmini ya wanachama walio hai kwani walishafanikiwa kuiweka chama kwa wananchi na ikafahamika sasa ni wajibu wa viongozi wa vitongoji na mitaa kueneza chama huku viongozi wa juu wakitengeneza sera na dira.
 
Hii Saccos ni shida tu!
Utajijua mwenyewe

20210526_175836.jpg
 
Wasiweke wawe na hadhi sawa... ukishatenganisha viwango umeweka madaraja.. jambo la maana ni kusema madaraja hayo yanakuja na ujiko upi... Sasa kuna vitu ambavyo wote wanaweza kuwa sawa (kama kupiga kura, kuomba nafasi za uongozi, n.k) lakini kuna vingine mnaweza kuwawekea ujiko kidogo... kwa mfano uliotolea...

Kuwe na ngazi ya Wafadhili - wanaotoa 3,000,000 kwenda juu... na hawa wanapewa hata vyeti au alama fulani za kujionesha kuwa wao ni wafadhili...
Umeanza vizuri ila umemaliza vibaya , wajionyeshe kwa manufaa ya nani na ili iweje ?
 
Wasiweke wawe na hadhi sawa... ukishatenganisha viwango umeweka madaraja.. jambo la maana ni kusema madaraja hayo yanakuja na ujiko upi... Sasa kuna vitu ambavyo wote wanaweza kuwa sawa (kama kupiga kura, kuomba nafasi za uongozi, n.k) lakini kuna vingine mnaweza kuwawekea ujiko kidogo... kwa mfano uliotolea...

Kuwe na ngazi ya Wafadhili - wanaotoa 3,000,000 kwenda juu... na hawa wanapewa hata vyeti au alama fulani za kujionesha kuwa wao ni wafadhili...
Mkuu mapendekeso yako yaweza kuwa ni mazuri ila chamsingi tu kusiwe na class - wote ni wanachadema aliyetoa 3m na aliyetoa 2500 - this is the key - ni muhimu sana sana!!

Usawa usawa usawa kwa wanachama wote.
 
Mkuu mapendekeso yote ni mazuri ila chamsingi tu kusiwe na class - wote ni wanachadema aliyetoa 3m na aliyetoa 2500 - this is the key - ni muhimu sana sana!!

Usawa usawa usawa kwa wanachama wote.
Hivyo ndivyo ilivyo , kumbuka wako watanzania wengi wanataka sana kuchangia ukombozi na wala hawataki kupanda majukwaani wala hawagombei chochote kile , wao ni wadau tu
 
Hiyo dhahabu ni material yake halisi au rangi ya dhahabu?
Binafsi siafiki utaratibu huu.
Itafikia wakati kwenye kugombea nafasi ndani ya chama watu watapeana kipaumbele kisa ada ya uanachama.
Chama kinataka kujiimarisha kifedha.na wanachama wapo tayari kuchangia.nadhani usiwaze kuuza kuku wakati hata mayai hayajaanguliwa.
 
Back
Top Bottom