CHADEMA njaa kali, kuanzia leo siwaamini tena, wapo kimaslahi zaidi

Tunawauliza nyie Chadema na viongozi wenu nani kawapa ridhaa ya kuwasamehe na kuwasafisha mafisadi kwa niaba ya Watanzania?Mtoto wa haramu hata mkimtia kwenye chupa atatoa dole. Nyie ni watu hatari sana. Na wewe Lissu usituletee huku mambo ya kesi za mahakamani ambapo mwizi anakuambia wewe wakili "mimi kweli nimeiba nitetee nisifungwe" wewe wakili unapotosha hata kudhulumu aliyeibiwa na hata kumhonga hakimu asimfunge mteja wako. Sasa wewe unatuletea dhuluma zenu za mahakamani kumsafisha fisadi,lol. Mlaaniwe. Hapa iliyofisadiwa ni taifa sio chama wala mwanasiasa. Dhambi itawatafuna.
 
Ukweli ni huu..
Lowasa alisema aliwasiliana na ''mamlaka ya juu'' ili avunje mkataba...kwa sababu anauzoefu na kuvunja mkataba wa City Water..
''Mamlaka ya juuu'' ikamwambia ''usivunje''..
Walio agiza mkataba uvunjwe ni kamati ya bunge... ambayo ilikuwa na wapinzani ndani yake..kama Eng. Mnyaa..!
A%20S-rap.gif

Duhh,aisee ,Maana Engineer Mnyaa hana Jimbo kwa sasa,maana Jimbo lake limeishaondolewa.
Hahahah,inabidi achomoe mtu au awe mpole
 
Pesa ni sabuni ya Roho. Hata wewe ungepewa robo ya hicho kiasi ungekaa kimya. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.
 
CCM nani aliwapa kibali cha kufuga mafisadi?meremeta,deep green,epa,richmond,escro kwa uchache.
 
Aliyetupa ruhusa ndiye aliyekunyima busara ya kuwafundisha maadili, huku ni kama kanisa tunasamehe tu tunasonga mbele.
 
Kweli magamba wanakazi! Wale waliochota escrow walishafukuzwa ccm, au mnaongea kwa kua mlipewa midomo
 
Watu wanajita majina yoote kumpaka rangi Samaki.

ACT ndio habari ya mjini kwa upinzani wa ukweli kwa Tanzania Bara,ZITO aliliona hili zamaniiiii
ADC ndio habari ya Mjini kwa Zanzibar,Hamad Rashid aliona hilo Zamaniiii,kwamba kuna watu piga uwa huwatoki madarakani

Wapo kimyaa,Watizameni kama mnavyowaona halafu kuna siku mntawasoma,ndio mtajua wapo kwenye Chama na wapi kwenye NGO
 
Mwenyekit wenu WA ccm mwenye mpgiga deal(simba trust), mbona amjawai kuwakemea..ccm n wanafik
 
CHADEMA wamefanha makosa mabaya. Waliijenga CHADEMA kwa hoja zenye nguvu. Mwangwi wa hoja zao mpaka sasa ungali hewani. Watanzania wakaanza kuwaamini. Hata kama uchaguzi huu wasingeshinda ni wazi wangetuongezea wabunge ambao wangewasilisha sauti za watanzania. But sasa wameachana na kujenga chama kwa hoja wanataka kujenga chama kwa kutumia sura ya mtu. Huyo mtu akishinda chama kitapata shida ya jehanamu, akishindwa chama kitayeyuka, akifa chama kitakufa na kusahauliwa.YETU MACHO TUOMBE UHAI.

Tunawauliza nyie Chadema na viongozi wenu nani kawapa ridhaa ya kuwasamehe na kuwasafisha mafisadi kwa niaba ya Watanzania?Mtoto wa haramu hata mkimtia kwenye chupa atatoa dole. Nyie ni watu hatari sana. Na wewe Lissu usituletee huku mambo ya kesi za mahakamani ambapo mwizi anakuambia wewe wakili "mimi kweli nimeiba nitetee nisifungwe" wewe wakili unapotosha hata kudhulumu aliyeibiwa na hata kumhonga hakimu asimfunge mteja wako. Sasa wewe unatuletea dhuluma zenu za mahakamani kumsafisha fisadi,lol. Mlaaniwe. Hapa iliyofisadiwa ni taifa sio chama wala mwanasiasa. Dhambi itawatafuna.
 
Aliyedhalilishwa hajalalamika; wewe kinachokuuma hasa ni nini?!

Kwani Lowasa ni mpumbavu kiasi kwamba haelewi akidhalilishwa?!

Mbona alishasema umesau "nimedhalilishwa sana,nimeaibishwa sana,nimeiba sana..hivyo nimeamua kujiuzuru uwaziri mkuu".....
 
I don't believe if you have good understanding
Kwani waliomchafua Lowassa ni Chadema au CCM? mwenyekiti wa tume ya Bunge alitoka Chadema au CCM? makamu wake pia alitoka Chadema? asilimia kubwa ya wabunge waliopitisha azimio ni Chadema au CCM? Lowassa aliposema kwamba kinachotafutwa ni uwaziri mkuu alikuwa anamaanisha kwamba Chadema ndio watakaopewa huo uwaziri mkuu au la.Just think at least for few minutes you will have good comments to share.

Mwakyembe alipokuwa anatoa ripoti alisema kwamba kama wangeeleza mambo yote serikali ingeanguka unajua maana yake? think before you say anything
 
CHADEMA imeuzwa kwa bei ya bil. 10 kwa mfanyabiashara maarufu Edward Lowassa na maswahiba wake.
Huu ni uchafu wa hali ya juu, ambao hata CCM tunaowaita mafisadi hawajakuwa nao. Ni uchafu wa historia kutanguliza matumbo, hadi kukiuza chama kwa wafanyabiashara kwa sharti la kuwa wagombea urais.

Naona baada ya Uchaguzi, iwapo atashinda urais, kitu ambacho ni kama ndoto vile, kitakachofuata ni kuiwekeza nchi na wananchi wake kwa mabeberu wawekezaji. Inasikitisha.

Mbowe kama mfanyabiashara hana uchungu na W atanzania, ametanguliza pesa mbele. Ameuza CHADEMA tuliyoipenda, tuliyoiamini kuwa itatuletea ukombozi. Amefanikisha kufifisha ndoto ya ukombozi wa Mtanzania.

Ushauri kwa Dr. Slaa, usirudi kwenye uchafu huu. Ni afadhali uchukue likizo ndefu zaidi wakati ukitafakari hatima yako ndani ya siasa.
 
Back
Top Bottom