CHADEMA nawashauri muanzishe kitengo cha uwekezaji hasa katika ardhi

fige

JF-Expert Member
Jul 4, 2010
376
61
ni jambo lililo wazi kuwa wenzenu ccm wamepora maeneo mengi sana ambayo kimsingi yalikuwa ni ya umma.mfano wa maeneo hayo ni viwanja vya michezo.

Nionavyo ni kwamba hata chama kingine kikiingia madarakani na kutaifisha hizo mali hakutakuwa na uwezekano wa kugawana, kwa msingi huo basi nawashauri uwepo mkakati madhubuti wa kupata maeneo ya kiuwekezaji ya chama hasa upande wa ardhi ili kujiimarisha kiuchumi na kukifanya chama kiwe na miundombinu endelevu.

Nawasilisha

 
Siasa na uwekezaji ni vitu wiwili tofauti kabisa. ebu tufungue macho, Miradi waliokuwa nayo ccm ilikuwa katika misingi ya chama kimoja
ambapo hata wewe raia una share yako mle kwa kuwa ulikuwa unatoa mchango wako kuanzia tanu mpaka leo ccm.
na michngo ilikuwa ni ya lazima kuanzia mashuleni mpaka maofisini. sasa basi ccm wapo katika kujisahau kwa kuendelea kupora
viwanja vya wazi mpaka kujiingiza katika mabiashara makubwa, Huo ni ufisadi. Sasa hivi ccm inatakiwa irudishe viwanja vyote vya
wazi ilivyotaifisha ardhi, majumba na viwanja vya michezo. na isisitishe miradi yote iliyokuwa nayo, kwani hivyo vinawagusa watanzania
wote, na ukiangalia sasa ni kinyume na mfumo wa vyama vingi. Na sio hilo tu bali hat nyumba za NHC zinatakiwa zote ziludishwe kwa
wenyewe na zilizokosa wenyewe ziuzwe. Kwa sababu nyumba hizo zilitaifishwa wakati wa siasa mbovu ya Ukomunisti. Serikali ni kuongoza
nchi na sio kuwa na miradi. Kwa sasa jambo muhimu ni katiba mpya kwani mapungufu yote hayo yanahitaji kuwemo katika katiba mpya.
 
Kuwekeza zimo kwa watu ila chama kazi yake siasa; CCM ndio maana watakwenda na maji na chadema haiwezi kuingia mtego huo; kwani individually biashara si watu wanafanya???
 
Back
Top Bottom