JOASH MUSSA
JF-Expert Member
- Oct 2, 2011
- 515
- 199
Siku za hivi karibuni kumejitokeza wimbi la wabunge wa cdm kufanya mikutano ya hadhara sehemu nyingi za nchi, nakubaliana na ukweli ya kwamba cdm imepata umaarufa hasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.
Ninachoaasi viongozi cdm na wafuasi wao ni kwamba binadamu yoyote ana hulka ya kukosa hamasa na kitu chochote hasa baada ya kuwa na mazoe na kitu husika, rai yangu ni kwamba hii mikutano ya hadhara mnayofanya imeanza kuwachosha wananchi na sitashangazwa na cdm kukosa kabisa wasikilizaji ama wahudhuriaji wa mikutano yao 2015.
Chadema inafanya kazi ya siasa na matunda ya kazi zake yanaonekana, kila kukicha inavuna wanachama hasa toka CCM tena wanachama wenye nyadhifa zao ndani ya chama, na kama ilivyo ada mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine,
we kereka lakini Chadema inachanja mbuga huku tunasubiri Nape atangaze sasa CCM ina wanachama Elfu 20 Tanzania nzima