CHADEMA, Lissu, wanaharakati na wapenda haki wengine lini mtafungua kesi kupinga Tundu Lissu kuvuliwa ubunge?

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Muda unazidi kwenda baada ya jimbo kutangazwa kuwa wazi. Mchakato wa kumpata mrithi umeshatangazwa na baadhi ya vyama vya siasa vimeanza harakati za kuliwania jimbo lililokuwa linashikiliwa na Lissu.

Katibu Mkuu wa Chadema Mashinji katika press release yake alieleza kuwa, ameagiza kurugenzi ya Chama chao cha Chadema kufungua kesi mahakamani kupinga hatua ya jimbo kutangazwa kuwa lipo wazi.

Pia katika video mojawapo kati ya video nyingi za Lissu, Tundu Lissu alionekana na alisikika akieleza kuwa atakwenda mahakamani ili mahakama iweze kusema iwapo Spika wa bunge hajui mahali Tundu Lissu yupo na pia mahakama itamke kama ni kweli jimbo lipo wazi.

Mpaka sasa naona jiiiiiiiiiii....kiza totoro. Ukimya umetawala. Nini maana yake?

*Kama Chama/wanaharakati/wapenda haki wengine, mmeridhika na hatua ya Spika wa Bunge kutangaza jimbo lipo wazi/mmekosa hoja?

* Mmekubali yaishe na kuamua kumuachia/Kumhukumia Mungu? Au

* Bado mnatafakari?
 
Back
Top Bottom