Chadema: Lipumba amefilisika kisiasa na kisera

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
KATIBU wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoani Tanga, Benson Mramba. amemweleza Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Professor Ibrahim Lipumba kuwa ni mwanasiasa aliyefirisika kisiasa na kisera.
Mramba pia amemtaka Profesa Lipumba, asome alama za nyakati ili kujua umuhimu wa mabadiliko kwa Watanzania, badala ya kuwa wakala wa CCM. Alikuwa akijibu madai ya Profesa Lipumba, kuwa yoyote anayeamini kuwa Chadem itatawala nchi, ni mgonjwa na anapaswa kwenda kwa Mchungaji Ambikile Masapila, kupata kikombe cha dawa.
Mramba alisema Profesa Lipumba, anajidanganya na kwamba Chadema ni taasisi na si chama kinachotegemea umaarufu wa mtu mmoja, kama ilivyo CUF. Alisema kwa msingi huo, chama hicho kitashika dola bila wasiwasi. Alimataka Mwenyekiti huyo kupumzika katika duru za kisiasa kwa kuwa hana jipya la kuwaambia wananchi.
Chadema inajiamini na ipo kwa ajili ya kuwakomboa wananchi wa Tanzania.
SOURCE: Mwananchi Machi 31, 2011
 
.....aibu kwa mwanazuoni Lipumba ku-bow kwa CCM kwa kutekeleza ule mfano 'if you can't beat them, join them'. Yaani yeye anaamini CCM haiwezi kutoka madarakani so bora ajikombe pengine anaweza kupewa ulaji huko mbele then hana haja ya kuwa mpinzani.
 
cdm wanatakiwa wasimjibu kibaraka huyo wanampa jina tu mtu mwenyewe anahutubia vichochoroni
 
CDM kweli wamezidi, yaani mpaka Tanga kiongozi ni Mchaga!!!?
 
Lipumba ni dalili aliye choka na yuko sokoni kunadi bidhaa mbovu inayotia ukakasi masikio ya wateja.
Cuf kwa kuwananga Cdm wakati walisha jigamba kuwa wao ni wapinzani inajionyesha wazi kuwa sasa CUF ni CCM B na hakuna shaka juu ya hilo.

Wapenzi wa cuf wakae na kutambua kuwa wao ni sehemu ya Ccm kwa kutekeleza sera na mikakati. Maalimu kule Znz anatekeleza ilani ya Ccm na Lipumba huku bara anashambulia chama kikuu cha upinzani kama inavyofanya CCM.

Lipumba anasumbuliwa na mchoko wa kisiasa ambao umesha ongeza kasi ya kukidhoofisha chama hicho kwa huku bara. CUF iliyowahi kujitambulisha kama chama ngangari leo hii kimegeuka chama mdebwedo na mlenda kwa kukubali kutumiwa na CCM na wao kujikuta wameingia mtegoni na sasa wao kama wanandoa wana hami unyumba wao usitetereke.

Cdm ndio ninao amini kuwa ni wapinzani wa kweli na watetezi walio beba matumaini ya watanzania.

.....aibu kwa mwanazuoni Lipumba ku-bow kwa CCM kwa kutekeleza ule mfano 'if you can't beat them, join them'. Yaani yeye anaamini CCM haiwezi kutoka madarakani so bora ajikombe pengine anaweza kupewa ulaji huko mbele then hana haja ya kuwa mpinzani.
 
CDM kweli wamezidi, yaani mpaka Tanga kiongozi ni Mchaga!!!?

Kwahiyo ulitaka awe Mwislamu mwenzako ndio ungelizika? by the way huyo kiongozi wa ngazi ya mkoa ndio wa hadhi ya Profesa Pumba, hana hadhi ya kujibiwa na viongozi wa ngazi ya kitaifa wa CHADEMA. wana majukumu mengi ya kitaifa.
 
Nitarudia tena na tena ushauri wangu kwa CHADEMA

CDM msijibishane na mbwa (read CUF) jibishanane na mwenye mbwa (read CCM) ndiyo saizi yenu.

Acheni mbwa kwa mbwa (CUF, TLP, NCCR, UDP etc) zibweke kum-impress master wao (CCM), huenda zikatupiwa mfupi.
 
Lipumba sasa hivi ningeshauri arudi tu akafundishe, chuo kinaweza kumkubali kurudi lakini sina hakika kama wanafunzi watakubali kuingia kwenye lecture yake. Ukishawasaliti watanzania inakuwa tabu wananchi kukuamini. Unawaambia watanzania kuwa Chadema wanahatarisha amani kwa kile ambacho na wewe unakihubiri leo kwenye majukwaa.

Lipumba hawezi kupata nafasi yoyote ya kupigiwa kura na wananchi tofauti na ndani ya chama chake. Hata ndani ya chama chake wanatumia tu hila Lipumba kuendelea kuwa kwenye nafasi hiyo. Waendeshe uchaguzi huru waone kama atabaki.
 
hii kali ya mwaka, sasa nathani cdm ndio chama kikubwa kuliko vyote tanzania kwa sababu kinapigwa vita na vyama vyote tz. ninawakumbusha cdm, cuf, nccr, tlp, udp sio saizi yenu achaneni nao. pambaneni na chama cha zamani ili mkiondoe madarakani 2015.
 
Ilikuwa haina haja huyu mramba kusema kuwa lipumba amefilisika mbona hiyo ipo wazi sana alete habari zingine bwana atakaye bisha kuchoka kwa lipumba anamatatizo yake!
 
Nitarudia tena na tena ushauri wangu kwa CHADEMA

CDM msijibishane na mbwa (read CUF) jibishanane na mwenye mbwa (read CCM) ndiyo saizi yenu.

Acheni mbwa kwa mbwa (CUF, TLP, NCCR, UDP etc) zibweke kum-impress master wao (CCM), huenda zikatupiwa mfupi.
Nimeipenda!
 
Tena helcopter/chopper ikishuka zone ya kusini,sijui kama hata utafikisha kura laki 1,2015
 
Zaidi ya miaka 20 bila kufanya research wala kuandika paper akafundishe nini darasani kwa vijana dotikom??????????

Lipumba sasa hivi ningeshauri arudi tu akafundishe, chuo kinaweza kumkubali kurudi lakini sina hakika kama wanafunzi watakubali kuingia kwenye lecture yake. Ukishawasaliti watanzania inakuwa tabu wananchi kukuamini. Unawaambia watanzania kuwa Chadema wanahatarisha amani kwa kile ambacho na wewe unakihubiri leo kwenye majukwaa.

Lipumba hawezi kupata nafasi yoyote ya kupigiwa kura na wananchi tofauti na ndani ya chama chake. Hata ndani ya chama chake wanatumia tu hila Lipumba kuendelea kuwa kwenye nafasi hiyo. Waendeshe uchaguzi huru waone kama atabaki.
 
CDM kweli wamezidi, yaani mpaka Tanga kiongozi ni Mchaga!!!?
Kama wenyeji wamelala ni muhimu kuzinduliwa hata wakoloni walikuja kutugongagonga vichwa ili tuamke ingawa bado hatukuzinduka natamani warudi tena.
 
kwa mwendo huu CDM itakuwa inakaba sana...matamko kaya ya Li-pumbav inabidi yajibiwe na vijana kama hawa, na yasijibiwe na kamati kuu toka juu..akina <Mbowe na Slaa) . Hii mbinu inatumiwa sana na CCM na yakibumburuka wanasema hayo ni mawazo ya vijana.
 
Back
Top Bottom